Andrew Tate
JF-Expert Member
- Jun 28, 2020
- 4,503
- 6,861
Watoto ni viumbe wasiojielewa wala kujitambua wao ni kina nani na nafasi yao ni ipi kwenye jamii. Hawana maamuzi binafsi, either watafuata maamuzi ya wazazi ambao huwachukulia kama miungu yao. Na vilevile watafuata mkumbo. Hii ni phase ambayo wapo kwenye ulimwengu wao wa utoto, kwamba kila kitu ni fairytale. Huu unaitwa msingi wa maisha ya mtoto. Na ndio kitu kitakachokuja kumfanya awe nani akifikia umri wa kujitambua. Ni sehemu unayotakiwa kuwa nayo makini sana. Ili kupata mtoto bora na makini baadae.
Cha msingi zaidi kwenye maisha ya mtoto ni kuwa na uwezo wa kujitambua na kujielewa yeye ni nani kama binadamu na nafasi yake ni ipi kwenye maisha. Baada ya hapo dini sio muhimu sana kwake. Tatizo ni kwamba inachukua muda mpaka mtoto afikie hatua hiyo. Labda miaka 17-18. Na njia pekee ya kufikia huko ni kuwa na msingi bora wa maisha huku chini. Kuharibu msingi ndio mwanzo wa kupata watoto wa ajabu baadae.
Kikawaida watoto huwa na tabia ya kufuata mkumbo wa watoto wengine ili nao wajisikie normal na sio outcast. Kitendo cha wewe kuwakataza kufanya mambo yanayofanywa na kila mtoto hapo mnapoishi na shuleni. Na kuwapakazia ideology advanced zako za kiutu uzima zinazohitaji akili, wisdom na uwezo mkubwa kuzichakata na kuzielewa. Kutawachanganya akili zao za kitoto. Kutawajengea msingi mbovu wa maisha. Kwani watajiona wasio wakamilifu, waliotengwa na outcast kwenye jamii. Hilo ni tatizo kubwa sana kwenye akili ya mtoto. Litamjengea asili ya unyonge. Kwani akili yake bado haina uwezo wa kuelewa maamuzi ya mzazi wake. Hutomfanya ajitambue, bali utamfanya akuchukie na kukuwekea kinyongo hadi akifika huo umri wa kujitambua, kwani atadhani umemuharibia maisha yake. Umeharibu msingi.
Ili kuepuka hilo, ruhusu waende huko kama wakitaka, na wakifika umri wa kujitambua wataona wenyewe uhalisia wa maisha pale akili za utoto zikianza kuwatoka. Ni hatari sana kucheza na msingi wa maisha wa mtoto. Hatari.