Nimepiga marufuku watoto wangu kwenda kanisani

Nimepiga marufuku watoto wangu kwenda kanisani

Mkuu una tatizo kubwa la afya ya akili, na unahitaji tiba ya haraka sana kabla ya mambo kukuharibikia kabisa. Fanya hima utafute kwanza mshauri wa kisaikolijia.
Isije ukawa wewe ndie mwenye hayo matatizo.Unageuzwa fursa wewe unahisi unapelekwa mbinguni kaka malizana na mbingu yako hapa hapa kwa kufanya kazi kula vizuri na kulala pazuri na amani ya moyo.
 
Kwanza tu ile story ya bustan ya Eden ipo kifala fala sana eti Mungu aliwaumba Adam na Eva na akawapa maskani ya Eden then humo humo akatuhusu na li shetan liishi mbaya zaid udanganyifu unafanyika yeye sijui alikuwa kalewa kalala mpaka udanganyifu wa kula tunda unaisha na yeye eti anatokeza na kuanza kupanic na kurusha ma laaana eti nyoka utapondwa kichwa,mwanaume utatafuta kwa uchungu na mke utazaa kwa uchungu na dhambi ya asili ikazaliwa.Sasa najiuliza alikuwa na mpango gani kumleta shetani pale EDEN kama sio alitaka kutuchoma moto
My favorite part of that story

Ni pale ambapo shetani ambaye ndio msababishi mkuu wa hiyo laana akapewa muda wa kuishi milele mpaka siku ya mwisho

Huku binadamu akipunguziwa life span yake pamoja na kuongezewa mabalaa na laana za kumfanya ashindwe kufurahia maisha hayo mafupi aliyopewa.

Lakini shetani yeye aliendeleza ushkaji na Mungu na meetings za hapa na pale zikiendelea kufanyika hususan kupitia reference ya Ayubu.

Ila tunaambiwa binadamu aliyeshawishiwa na shetani hawezi kumuona Mungu kwasababu ya madhambi yake jinsi yaliyokuwa mengi.

Kwa mantiki hiyo ni kuwa sisi tunadhambi nyingi kumshinda shetani na ndio maana hatuwezi kumuona Mungu.

Na sisi tunadhambi nyingi kumshinda shetani na ndio maana ilikuwa ngumu kumshawishi Mungu aweze kutupa umri mrefu wa kuishi duniani kama alivyofanya kwa shetani.
 
watu hamuelewi mtaji wa kijamii vizuri

ni kama kuwa mwanaume halafu hufuatilii mpira vijiweni utakuwa unatoa macho tu

ndo dini sasa inakupa tiketi ya kuwa karibu na watu, haswa kwa watoto wadogo
Watoto wanaweza wakawa karibu na wenzao wakiwa shuleni sio lazima huko makanisani, kinachofundishwa shuleni kina mantiki zaidi kuliko hadithi za fimbo kugeuka nyoka zilizo kwenye Biblia,

Na pia watoto ubongo wao unahitaji kujazwa vitu vya maana zaidi usiruhusu mtoto ajazwe ujinga wa dini ni kheri atengwe na jamii kwa kuwa na mitazamo tofauti yenye mantiki, kuliko kupendwa na jamii kwasababu ya kusapoti upumbavu wa vijiweni na kujua stori za uongo za kwenye Biblia na quran.
 
Wapi nimesema linamuongezea kitu? Watu wenye akili tunafahamu dini ni utapeli tu, lakini lazima ukae kwenye mfumo wa dunia inavyotaka siyo unavyotaka, usidhani hizi serikali ni wajinga kukumbatia dini.

Dini ndio siasa namba moja kongwe duniani, kwahiyo huwezi kuishi kwenye dunia halafu upingane na mifumo ya dunia inavyotaka, hili ndio tatizo pia linawasumbuwa sana waislamu.
Mbona mfumo wa Dunia unataka watu wawe mashoga na wewe hujaamua kuwa shoga ?

Kwahyo mfumo wa Dunia ukiamua kitu chochote na wewe utakifuata tu kwa sababu ni mfumo wa Dunia ndo umetaka hivyo.
 
Kuna kijana namfahamu alikuwa anasomea udaktari, baada ya kumaliza kidato cha 6 mama yake kampeleka kwenye makanisa ya kilokole, kumbuka hii familia ni RC mama akahubiriwa akashukiwa roho mtakatifu akahamia huko, kiukweli kijana ana maadili ila kufika chuo ikawa ni kanisa na yeye yeye na kanisa akapewa na uzee wa kanisa, kilichotokea ni kufeli kadisco miaka yote 5, ada yote aliyolipiwa ni hasara maana hakuwa na mkopo, mama mtu yupo kumnanga mwanae aliyempeleka mwenyewe kwenye hayo makanisa.....

Kwahiyo mkuu upo sahihi umeshtuka bado mapema
 
Alikutana wapi na Mungu mpaka akakikiri na mimi nije?

Imani inaponya alafu yeye anatembea akiwa na mabodyguard


Being a spiritual person sio lazima uwe attached with DINI .

Muhimu make sure unawalea Junior na prince na princess kwa wao kutambua kuwa there's higher power ambayo inaendesha MAISHA yao.

Mfano you can teach them Kufanya gratitude, kuwa na compassion act like kufanya tithing ,charity n.k

Being a spiritual person is not about to pray in church but is to live in a good way .
 
Kuna kijana namfahamu alikuwa anasomea udaktari, baada ya kumaliza kidato cha 6 mama yake kampeleka kwenye makanisa ya kilokole, kumbuka hii familia ni RC mama akahubiriwa akashukiwa roho mtakatifu akahamia huko, kiukweli kijana ana maadili ila kufika chuo ikawa ni kanisa na yeye yeye na kanisa akapewa na uzee wa kanisa, kilichotokea ni kufeli kadisco miaka yote 5, ada yote aliyolipiwa ni hasara maana hakuwa na mkopo, mama mtu yupo kumnanga mwanae aliyempeleka mwenyewe kwenye hayo makanisa.....

Kwahiyo mkuu upo sahihi umeshtuka bado mapema

Hapo kilichotokea ni FAITH and believe

Huyo kijana hakuwa na FAITH bali believe maana ukiwa na believe unakuwa driven and not driver

So ukiwa na believe wewe na mshirikina mnakuwa mnatembea katika zone moja maana mnakuwa mnakosa kuendesha mambo Ila mnaendeshwa .

Unfortunately watu wengi wanakosea Sana wanakuwa karibu na dini ambayo huwapa believe na sio FAITH ukiwa na FAITH hauwezi kufika hiyo hatua.

To be blessed ni kuwa karibu na Mungu na sio karibu na dini.

Dini ni njia ya kukupeleka kwa Mungu Ila ikiwa unajua njia ya kufika Mungu basi usiwe deep Sana ktk dini weka balance.

Nimesikitika Sana to hear that info za huyo kijana
 
Poa, angalia mtoto anavyotekwa kiimani, anabatizwa akiwa mtoto, anafahamu nini? Muache awe mtu mzima aamue mwenyewe kama atakubali kudanganywa na hizi imani za kigeni.
Ukisema imani za kigeni... Hapo basi uache na vitu vyote... Ikiwemo technology na matumizi ya vitu kama simu. Issue ni kuchagua mazuri uache mabaya... Kuna mtu alisema ngono na mihadarati ni vizuri kwa sababu ngono ni tamu... Lakin wakati huo huo kuna mwenzetu kaanzisha thread anajuta... Just think mtoto wako akawa pornographer na anasema anaingiza pesa huku akifaidi utamu... Lakin in nature ukituliza akili unaona kabisa sio kitu kizuri...
 
Baada ya kuona ujinga mambo ya makanisani nimeona nipige marufuku watoto wangu kuwa brain washed na mambo ya kanisa na aina zote za imani badala yake nawafùndisha life manners mwenyewe.Kama wataamua kwenda kwenye imani yoyote wafanye baada ya kutoka kwenye himaya yangu.
Mke wangu kwa vile tulikutana ukubwani mi nimeachana nae aendelee kuwa nyumbu wa huu ujinga wa kuwa na matumaini ya kwenda mbinguni.
SERA YANGU:Mbingu yangu ni hii good life niliyo nayo kwa sasa nikifikwa na majanga basi itakuwa jahannam yangu.
KAMA UNAUNGANA NA MIMI GONGA LIKE TUJUANE
Sawa hayo ni maamuzi na mtazamo wako juu ya hili lakini lengo lako ni nini hasa? Ungewakataza watoto wako kwenda kanisani halafu ukapiga kimya bila mtu yeyote kujua ingekugharimu nini? Au ni shetani amekutuma huku kutafuta wafuasi zaidi?
 
Back
Top Bottom