Nimepiga marufuku watoto wangu kwenda kanisani

Watoto ni viumbe wasiojielewa wala kujitambua wao ni kina nani na nafasi yao ni ipi kwenye jamii. Hawana maamuzi binafsi, either watafuata maamuzi ya wazazi ambao huwachukulia kama miungu yao. Na vilevile watafuata mkumbo. Hii ni phase ambayo wapo kwenye ulimwengu wao wa utoto, kwamba kila kitu ni fairytale. Huu unaitwa msingi wa maisha ya mtoto. Na ndio kitu kitakachokuja kumfanya awe nani akifikia umri wa kujitambua. Ni sehemu unayotakiwa kuwa nayo makini sana. Ili kupata mtoto bora na makini baadae.

Cha msingi zaidi kwenye maisha ya mtoto ni kuwa na uwezo wa kujitambua na kujielewa yeye ni nani kama binadamu na nafasi yake ni ipi kwenye maisha. Baada ya hapo dini sio muhimu sana kwake. Tatizo ni kwamba inachukua muda mpaka mtoto afikie hatua hiyo. Labda miaka 17-18. Na njia pekee ya kufikia huko ni kuwa na msingi bora wa maisha huku chini. Kuharibu msingi ndio mwanzo wa kupata watoto wa ajabu baadae.

Kikawaida watoto huwa na tabia ya kufuata mkumbo wa watoto wengine ili nao wajisikie normal na sio outcast. Kitendo cha wewe kuwakataza kufanya mambo yanayofanywa na kila mtoto hapo mnapoishi na shuleni. Na kuwapakazia ideology advanced zako za kiutu uzima zinazohitaji akili, wisdom na uwezo mkubwa kuzichakata na kuzielewa. Kutawachanganya akili zao za kitoto. Kutawajengea msingi mbovu wa maisha. Kwani watajiona wasio wakamilifu, waliotengwa na outcast kwenye jamii. Hilo ni tatizo kubwa sana kwenye akili ya mtoto. Litamjengea asili ya unyonge. Kwani akili yake bado haina uwezo wa kuelewa maamuzi ya mzazi wake. Hutomfanya ajitambue, bali utamfanya akuchukie na kukuwekea kinyongo hadi akifika huo umri wa kujitambua, kwani atadhani umemuharibia maisha yake. Umeharibu msingi.

Ili kuepuka hilo, ruhusu waende huko kama wakitaka, na wakifika umri wa kujitambua wataona wenyewe uhalisia wa maisha pale akili za utoto zikianza kuwatoka. Ni hatari sana kucheza na msingi wa maisha wa mtoto. Hatari.
 
Unawafundisha watoto kutii kauli zako na ambazo zinaweza kuwa sio nzuri, kuna siku utawaambia wakaibe wakakutii ungewaacha tu maana sizani kama itawaletea madhara, vinginevyo watakuja kuwa na tabia mbaya, au kuna siku watajiuliza kuhusu akili ya baba yao kwanini aliwakatza kwenda kanisani. Umefanya makosa makubwa sana ujue dini inasaidia kulea watoto na kuwakuza katika maadili pia
 
Kwani kuzikwa lazima uzikwe na kanisa?
Hata kuzikwa sio lazima. Ni namna au jinsi ya kuondokana na limwili lako lisibaki kuoza na kutuharibia hali ya hewa kwa harufu mbaya. Akitupiwa mamba au wakitafuna fisi yote ni poa tuu au (Asante sana Kiranga)
 
Hongera Sana mtoa mada kwa kujua ukweli kuwa dini Ni hadithi za kale zilizotungwa na watu kama sisi.
Hakuna Mungu, mbiguni Wala moto wa milele.
Wafundishe elimu ya darasani, itawasaidia sana.
Sikubaliani na hilo hata kidogo.
 
Hata kuzikwa sio lazima. Ni namna au jinsi ya kuondokana na limwili lako lisibaki kuoza na kutuharibia hali ya hewa kwa harufu mbaya. Akitupiwa mamba au wakitafuna fisi yote ni poa tuu au (Asante sana Kiranga)
This logical fallacy is called "strawman argument".

Mimi nimeuliza kwani kuzikwa lazima kuzikwa na kanisa?

Hujajibu swali nililouliza, unaniletea habari zako tofauti na swali langu.

Swali langu halijajibiwa bado.

Kwani kuzikwa ni lazima uzikwe na kanisa?
 
Hako kamshahara ka milion kadhaa.. na virushwa na upigaji wa hapa na pale ndio unaokupa kibri.
We ambae unashinda kwenye mikesha na kufunga ukimanisha unamtukuza Mungu basi endelea baba tutakutana Mbinguni
 
Mtu mzm na akili yako yote unajua dini it's all about kwenda mbinguni, Dini ni zaidi ya fikra zako hzo kama haujui

Dini inakufanya uwe mwerevu pia ,ww ni moja ya madhara ya watu kukosa dini yani umetingwa na akili haiko timamu hauna amani ya moyo kbs.
 
Muda alioharibu kwenda kufia msalabani angeutumia kumuangamiza shetani tu. Alafu alishajua kabisa atafufuka, kwa hiyo hata kufa kwenyewe hakukuwa issue sana.
Umeona ee kwanza angetushirikisha namna aliyopanga kuuokoa ulimwengu? Si angetuulia shetani na kutuondolea njaa aone kama angetukosa peponi
 
Huwezi kujibu hoja pasina kutukana watu? Ndivyo mnafundishwa kwenye dini?
 
Sio lazima.
 
Mimi nina amani kuliko wewe ambae unaishi na kuogopa kitu ambacho hujawahi kukiona si ndo matatizo ya akili
 
Uko sawa kabisa,implicitly Mimi niliishaamua hi yo.Huwa namuomba Mungu wangu Mimi mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…