Nimepiga marufuku watoto wangu kwenda kanisani

Una hoja. Usikilizwe kidogo
 
subiri watoto wako wafundishwe na shetani wawe mashoga, wasagaji, wauwaji na vibaka ndio utastuka.
 
Mfano wewe una uhakika kuwa mama yako mzazi ndie huyo kuwa labda walikuokota jalalani baada ya kutelekezwa na mama yako halisi

Au una uhakika gani kama huyo baba yako ndie mwenyewe ?
Yanafananaje haya maswali na topic yangu?
Umekula leo lakini?
 
watu hamuelewi mtaji wa kijamii vizuri

ni kama kuwa mwanaume halafu hufuatilii mpira vijiweni utakuwa unatoa macho tu

ndo dini sasa inakupa tiketi ya kuwa karibu na watu, haswa kwa watoto wadogo
 
Mkuu Billie binafsi nimekuelewa mno, kila la heri katika yote.
Kwa kweli tunaenda kuwajaza watoto mataka taka yasio na ulazima vichwani mwao bila sababu ya msingi.
GB za mtoto wa Kiafrika anajazwa yakikushinda hapa duniani komaa na mchongo wa kwenda peponi ukaonane na Yesu alafu mchina anampika mtoto wake katika kuaminia matumizi sahihi ya ubongo na crafts mbalimbali ili baadae awe producers na mvumbuzi we huoni sisi tunatengeneza kizazi cha watu wavivu.Mfano hao Gen Z wametandikwa na umasikini mpaka wanahisi ahueni yao inapatikana kwa kumtoa rais madarakan maana swala la BILL rais alipiga chini kusaini ila bado wanaandamana.
Njoo Tz nyumbu zimetingwa na life zimejazana kwa Mwambosa ahueni ya life hawaioni japokuwa wamemsogelea Mungu.
Tuliogundua mchongo tupo tunapiga ma businesses na maisha yanasonga kwa speed nzuri muda wa ibada si tupo tunapush mizigo tu kwa nini tusiwapite kwa muonekano,hela na hata utajiri
 
Kwani kanisa likimzika kuna kitu linamuongezea?
unadanganywa kuwa maombi ya viongozi wa dini yana mantiki yoyote kwenye mazishi
Wapi nimesema linamuongezea kitu? Watu wenye akili tunafahamu dini ni utapeli tu, lakini lazima ukae kwenye mfumo wa dunia inavyotaka siyo unavyotaka, usidhani hizi serikali ni wajinga kukumbatia dini.

Dini ndio siasa namba moja kongwe duniani, kwahiyo huwezi kuishi kwenye dunia halafu upingane na mifumo ya dunia inavyotaka, hili ndio tatizo pia linawasumbuwa sana waislamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…