Acha ujinga fazaaa. Dem umeona video analiwa ndio unataka amuoe?
Wewe ndio Fala wa kwanza hapa Tz
Mimi nimecheka sana kwa comment yako baada ya kugundua najibishana na kijana wa rika gani.
Hii dunia inatulazimisha tunavyozeeka tutumie busara kwa kila jambo hata kama katika ujana wetu nasi tulikuwa ni wahuni na tunajua kila kitu.
Ukitaka uende sawa, katika mambo yote ambayo watu wamekwazana na kuhitaji busara zako ili kusuluhisha jambo, jiepushe kusikiliza maneno ya upande mmoja na kufikia kutoa maamuzi kama ilivyo katika mada hii, je bibie tumemsikiliza, je akija hapa na kusema hizo ni fitina tu za kichuna wake, mambo hayo aliyafanya kabla ya uchumba?
Turudi kwenye agenda yetu sasa:
Mleta uzi ni kweli katoa tuhuma nzito juu ya mwenzake, katika baraza la usuluhishi wa mapenzi.
Hatuwezi kusimama na kutoa maoni ya kumuunga mkono bila kuwepo na utetezi wa mlalamikiwa.
Mzee wangu, mapenzi yana mambo mengi chungu nzima na hisia zetu katika mapenzi binadamu tumetofautiana, kila mtu na yake.
Maamuzi yatoke utakapokuwa umewapima kwa maelezo yao kutokana na maswali utakayowauliza na kugundua udhaifu ulipo.
Bado jiweke refa usiyeegemea upande, hapo mambo utayapeleka sawa.
Utakapoona msimamo thabiti na usioyumba wa mlalamikaji ndipo nawe uunge mkono, tena kwa neno moja tu 'sawa' bila kuingiza maneno na misimamo yako ya kimhemko.
Sisi tulishaona si mara moja, watu mnashuhudia kabisa jamaa anachezewa rafu za kutosha hadi waangaliaji mnakasirika na kumwambia ukweli jamaa, lakini mtaona hawaachani, sasa hapo nyie mnakuwa kwenye fungu gani?
Mambo ya mapenzi huwa hatushauri kuachanisha bali kuunganisha.
Na mwisho wa siku maamuzi hubakia kwa wapenzi wenyewe.