Nimepigwa Tsh milioni 8 kwenye biashara ya uwakala kupitia mfanyakazi mzembe

Umeongea vizuri Nkamu.
Kwenye issue ya pesa lazima uwe makini, huyo wakala mwizi..!!

Kabla ya kufanya muamala lazima ujiridhishe kwa kupiga simu. Na kingine unawapa vipi simu yako au ya ofisi wateja?

Hata namba za simu kuna pen na karatasi unapewa uandike km huwezi kuzitaja. Yote hiyo kuepuka ujanja ujanja wa wezi..!!
 
Achana na matapeli na twende uzi wa Liverpool Saint Anne
 
Fanya ifuatavyo:
1.repoti polisi na kwenye hiyo mitandao ya simu ambayo fedha zilitolewa
2.Usimfukuze kazi huyo binti bali hiyo mil 8 iwe ni deni kwake,ambapo sasa ukubaliane nae jinsinya kumkata mshahara,muondoe kwenye kazi hizo za pesa na umpe kazi za usafi
3.weka mtu mwingine hapo kwenye nafasi ya huyo dada,ila weka sheria zako kwa maandishi na uzibandike ukutani.
 
Mi mkinga aisee kwenye issue ya pesa sitaki hata mazoea wala kujuana na mtu..!!

Huyo Binti hajatenda kosa la jinai kwa hiyo polisi siyo sehemu sahihi.

Aliyetenda jinai ni huyo aliyetumiwa pesa. Katenda kosa la udanganyifu, personification.

Binti ni agent wa boss/principal. Na boss ndiye katendewa kosa, kama alivyosema kwenye uzi hapa kwamba 'kapigwa'.

Kwa hiyo Binti hapo ni shahidi namba moja na siyo mtuhumiwa namba moja.

Mnakosaga haki kwa kukurupuka.
 

Kitu kizito hicho
 
Sawa
 
Kwanza convo za tajiri si zinakuwepo pale kwenye meseji.
Ukifungua utaona convo za nyuma.

Iweje achat na majina yaliyoseviwa kwa majina ya tajiri
Na haoni convo za nyuma
Wampe namba hadi anatuma miamala yote kweli!
Yaani haiwezekani.
Huyu amekula njama na wezi.
 
Ukute anatumia kiswaswadu
 
Ukute anatumia kiswaswadu
Aisee
Chats za tajiri ni muhimu sana kutunza maana matajiri bwana
Kuna muda anaamka na wenge anakuja kukudai pesa ambazo alishachukua.
Bila kutunza kumbukumbu lazima upate stress.
Hutakiawi kufuta meseji za tajiri..
Na hata akichukua hela unamsainisha ili mbele ya safari tusije kurukana.

Hata kama ni simu ndogo,,aliwezaje kumtumia mtu pesa na majina hayatokei ya tajiri?
Namba siyo ya tajiri.
Hebu kuweni serious,, hata kama walibadili majina.. yaani usiijue namba ya tajiri?
 
Ninachoweza sema Pole sana Mkuu,
 
Hizo sheria zako kaungane na mawakili wa Lissu mtusaidie kumtoa..!!

Ila kwenye pesa zangu hazifanyi kazi, ilishawahi kutokea na nilifanya hivyo alitandikwa mpaka aliongea ukweli na wazazi wake wakalipa pesa..!!
 
Inaonekana hujawahi kusingiziwa jambo hadi ukahisi kutetemeka kwa hasira 😊
Kusingiziwa na kuiba vitu viwili tofauti, huyo binti yeye hajasingiziwa coz miamala kafanya mwenyewe na akili zake timamu bila kushikiwa bunduki..!!
 
Baada ya uchunguzi wangu nimekuja kugundua Hawa watoto wa sasa hivi IQ yao iko chini sana, unaweza kuwa na kijana ukamuona Smart kwa muonekano lkn kichwani ni mweupe peee! Madogo wa sasa hivi sio watu wa kujiongeza hata kidogo, we chunguza rika gani linaongozwa kwa kutapeliwa na uzembe!

Ushauri wangu: kabla ya kumueka mtu yoyote asimamie biashara Yako ni vzr ukamchunguza sana hasa utimamu wake wa akili,maarifa, na namna anavyojiongeza hasa kwenye kutatua changamoto, ubunifu,uwajibikaji nk( Hawa madogo wa sasa hivi hizo sifa ni wachache sana wako nazo)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…