mandieta19
JF-Expert Member
- Sep 9, 2024
- 342
- 893
Hakuna kitu hatari kwenye uwakala kama kuleta mazoea na wateja. Kitu ambacho watu hawajui ni kuwa hao wateja wako ndio matapeli wenyeweUyo binti inawezkana hao watu ni watu waliokuja kimazoea na kumuachia vitipu vya hapa na pale sasa akawa kawazoea ndo maana hata simu akawaachia mpaka kutokea utapeli huo ila pole sana mkuu uyu binti kama inakupendeza msamehe tu muachie Mungu atakulipa zaidi
Hapana mkuuHaujaweka camera hapo ofisini kwako ili upate pakuanzia
Daah aiseeSio mzembe kulizwa kwenye hio biashara nje nje mkuu, mimi nilisha achana nazo hizo biashara za miamala
Hapo hata mkifatilia mnakuta mmiliki wa Hilo jina la kwenye laini ni mzee hata hajiweziDaah aisee
Pole,usimlaumu hua inatokea kutapeliwa,matapeli wana mbinu nyingiAisee siku ya Jana imekuwa mbaya sana kwangu mfanyakazi wangu amenitia hasara ni hivi Kwa mujibu wake huyu binti walikuja jamaa wiki Moja kabla wakamuambia awape simu waweke laini akawapa wakati nilishamkataza asimpe mteja simu kilichotokea kumbe walisave jina langu namba yao kwenye simu yake Jana wakaanza kumtumia meseji kwamba awatumie pesa na wakatoa namba nyingine yaani wanajifanya wao ni Mimi kwamba nimepata shida Sasa binti akawa anatuma mpaka ikafika milioni 8 ndipo alipoishiwa float
Sasa akawapigia wakawa hawapokei simu akafunga safari kuja nyumbani akamkuta wife aisee alivyomuambia wife ndio akanipigia kuniuliza kusema ukweli nilipigwa na shoti ya mwili ghafla nimetandika vibao huyu binti mpaka muda huu naandika huu.
Uzi sijui nifanyeje maana jamaa tulitaka kurudisha miamala kucheki washatoa muda mrefu
Naombeni mliopitia hii situation mlivukaje maana kichwa kinawaka moto leo
Wanaotapeliwa sio wendawazimu Mkuu,hio huo inatokea tuHutakaa ujue kama mfanyakazi wako ni mwendawazimu mpaka utakapokutana na tukio. Tena hawa graduates ndio ndezi kabisa.
Kuna mfanyakazi wangu mmoja alitapeliwa zaidi ya mil 8. Ni uwendawazimu kwa sababu mfanyakazi anafanya jambo la ajabu ambalo hata uwe na akili ya kenge huwezi kufanya jambo kama hilo.Wanaotapeliwa sio wendawazimu Mkuu,hio huo inatokea tu
We jamaa mbishi, haya nipe kazi kwenye kampuni yako basi..!! 😹Nipo na mothercity safaris na usafirishaji mizigo kutoka SA niombe kazi kwa nani tena mkuu siwezi kudhurumu masikini ili niongeze mali kwenye kampuni tunayowaachia watoto baadae wanashindwa kuendesha kampuni kumbe kulikua na hela za dhuruma ndani yake nimekwambia nina mifano ya watu kibao walikua na hiyo tabia mmoja jana nimemuona Kariakoo anaongea peke sisi huku ni Wakurungwa tunapotoa Elimu tuna mifano halisi.
Ndo atie hasara ofisi za watu?Mwanamke mwenzio
Ni mwizi apelekwe polisi km hajasema ukweli..!! 😹Ni mwizi kweli
Unatumaje pesa bila kuangalia jina?
Huyu ameshirikiana na wezi
Hela haina mzaha namna hiyo
Wewe kiboko yako Marry.Nakuheshimu sana mshangazi na ni vile hujuagi tu
Dada nlikuchek kweny ile thread yangu hujanichek tenaKwenye pesa hapana tucheke na mengine..!!
Hapo apelekwe polisi wazazi wake km wana pesa wamtolee kufidia hasara..!!
Mtu kakatazwa usitoe simu yeye katoa, hapo nitaamini vipi km hawako wote wameshirikiana?
Hata akisema amkate mshahara hatofanya kazi kwa ufanisi, atafanya bora liende mwisho ataiba tena kwa kujua atakatwa kwa kufanyishwa kazi..!!
Na huenda hakagui daily based transactionWewe mwenyewe mzembe haiwezekani umkambidhi million 8 kijana aisiye na akili timam