Nimepokea taarifa ya baadhi ya raia wa Afrika Kusini kuwataka wageni kuondoka nchini mwao

Nimepokea taarifa ya baadhi ya raia wa Afrika Kusini kuwataka wageni kuondoka nchini mwao

Nimepokea hivi karibuni voice note kutoka kwa Mtanzania anayeishi Afrika Kusini. Sauti hiyo ya Dudula Master ambaye ni mhamasishaju mkubwa wa Xhenophobia ametoa onyo dhidi ya wageni wote kuondoka Afrika ya Kusini kuanzia tarehe 02 Septemba 2022 hadi March 2023.

Nchi zetu hususan Tanzania zinapaswa kuhakikisha usalama kwa raia wao wanaoishi kule kihalali na ikiwezekana kuweka utaratibu wa kuwaondoa raia wake Afrika ya Kusini.

Matishio haya yamekuwa yakifanyika bila hatua zozote kuchukuliwa hivyo inawezekana baadhi ya watumishi wa vyombo vya dola vya Afrika ya Kusini ni wahusika wa hizi operesheni dhidi ya wageni Afrika Kusini.

Hatulipi ubaya kwa ubaya bali kumtenga mtu mbaya ni sehemu ya kumpa fundisho dhidi ya mtenda ubaya. Ni wakagi sasa wa nchi za SADC kuitenga Afrika ya Kusini na ikiwezekana Umoja wa Africa (AU) kuiwekea vikwazo Afrika Kusini mpaka watakapoondoa vitisho dhidi ya usalama wa wageni ndani ya nchi hiyo.
View attachment 2327764

View attachment 2327204
Nawaunga mkono wa South Africa nyie mnavamia nchi za watu kibaya zaidi mnajazana zaidi huko bila vibali mnafanya maovu kama kuuza madawa ya kulenya ,mauaji, wizi ,ubakaji ,ujambazi NK .
Mnachukua ajira za wazawa ,wao Wana Haki ya kupigania maslahi Yao pia , nyie mnashindwa kurudi na kusetle kwenye nchi zenu na kuziwajibisha serikali zenu kutengeneza mifumo Bora ya uendeshaji WA hizo nchi ili ziwe Bora ,
Shameful .
 
Wewe ni mpumbavu wa kwanza maana wa mwisho ana afadhali, wakati Raise akiwa Frederick De Cleck nilikuwa hapo, Mandela anapigiwa kura Niko hapo, Thabo Mbeki anaachiwa Urais na Mandela Niko hapo, nimetoka hapo kwenda Uingereza nimeruka Jan Smarts airport sasa hivi mnaita Oliver Tambo airport.

Tafuta watoto wenzanko wa kuwadanganya kuhusu hao "Primitive wanyama" nawajuwa kuliko ninavyowajuwa Watanzania.

Kama una akili timamu waeleze watu hapa ni kwa nini wazungu wote na watu weupe wote bila kujari ni RAIA au siyo RAIA wapo salama kuliko MTU mweusi mgeni?

Ni kwa nini waafrika wenzenu wanawaita jina la kibaguzi Makwelekwele?

Hao watu ni Primitive napigia mstari.
Jina lingine wanajulikana kama Machafuchafu na wengi wao ni watoto wa mtaani.
Ambao zamani kwenye miaka 1989 mpaka 1991 kipindi cha baridi walikuwa wanafanya mauaji mbele ya polisi ili aende jela kujificha Baridi.
Wabaya ni Wazulu sio wakosa kwani Wazulu ni wavivu wa kufanyakazi na kufikiti.
Binadamu gani anajisifia kuwa na namba kubwa ya mauaji ndio mjanja.
Yaani kuua ni ujanja au ujinga
 
Yap nakukumbuka mimi tulionana mara moja pale kwenye mjengo wako uliomwachia Chaa west woodstoke ulihamia sijui Rose bank muda mrefu sana pana rafiki yake Chaa akikua na roho mbaya balaa nae alikuja UK sijui aliishia wapi..enzi hizo Wasauzi wakimuona mgeni wanaweza kumtupa hata nje ya treni huku likiwa linatembea pana case moja iliniuzunisha jamaa alipanda juu ya treni akafa kwa kugusa umeme wa treni akikimbia asipigwe visu na wakhosa miaka hiyo leo hii anatokea mtu anakwambia mambo ya vibali ..
Group yetu wengi walitawanyikia UK wengine Switzerland hasa wazee wanyeupe, pale Golden Acre mall underground ndio tulikuwa foreigner wa kwanza kuthubutu kuchukuwa space to rent na kuweka Salon la kijanja.
 
Inasemekana wanawake wa kisouth ni wazuri balaa
South Africa kuna race 4, black, wazungu, makaladi na wahindi, hizo race zote kuna visu vya ukweli Ila makaladi the best ni kama vitoto vya kiarabu hivi lakini pisi za ukweli.
 
Mkuu Kuja hapa na kichwa cha Habari kama hiki sio vema wakati unajua kabisa kuwa huu ni UONGO, na elewa humu SIO wote ni mazuzu, guy's huu ni uongo, kinachofanyika sasa hapo SA,kwanza home affairs yao imeamua not to extend Zimbabwe special permit, hii permit iliwaruhusu wazimbabwe waishi SA kwa muda wa 4yrs each na ilikua renewable, mwaka jana wameamua kuterminate hizi permits na wamepewa miezi 12 ili waombe permits zingine (SA wana zaidi ya 15 different types of permits),effects ni kubwa maana wazimbabwe ndio wengi ndani ya SA, na la muhimu mno SA sio kwamba inazuia immigrants kuingia, isipokua wanakutaka uingilie MLANGONI sio kuruka ukuta, hata sisi hapa nchini mgeni aingilie pale border sio Kuja na njia za panya, ukikamatwa utapigwa vibaya mno(ili usirudie tena)then jela au fine na rudi kwenu,maana huna adabu huwezi Kuja nyumbani kwangu kwa kuingilia dirishani wakati mlango upo wazi;DUDULA ni movement ambayo inatia pressure kwa serikali ili I deal na illegal immigrants, wenye permits halali wapo safe for now;watu wa viwanja msikatishwe tamaa na hoja kama hizi, tembea katafute maisha, make sure una passport, pitia MLANGONI na ukipewa 90days za visa,ikiingia badilisha kupata long visit visa
Umevuta nini?

Mbona hoja zako ni tofauti na za mtoa mada? Au lengo ni kutujuza kuwa ushaishi south africa,

Tambua kuwa kinachoongelewa sio kigeni, kilishawah kutokea zaidi ya mara mbili.
 
Umevuta nini?

Mbona hoja zako ni tofauti na za mtoa mada? Au lengo ni kutujuza kuwa ushaishi south africa,

Tambua kuwa kinachoongelewa sio kigeni, kilishawah kutokea zaidi ya mara mbili.
Nope sijaishi huko nipo ruvuma huku,ila nakataa uzuzu, wapi source ya taarifa hiyo kuwa March 2023,Waafrika wote wahamiaji wawe wameindoka SA?,ni hilo tu au unaona ni ombi kubwa sana?
 
Ginehe bhabhaa??
Sipati picha ingelikua moja ya nchi za kiarabu yatokee haya ya "kufukuza wageni, hususani hapa bongo" i think wangejumuishwa waarabu wote ni makatili, magaidi, yanaroho mbaya, mashetani, hapo wenye udini nao wangelipuka balaa wakina fulani bhabhaa 😁😁 lakini kwakua ni wenzetu wasauzi itaonekana ni kawaida tuu bila kujumuishwa "waafrika ni makatili" 😁😁 inachekesha sana. Hebu tuwapende hawa ndugu zetu waarabu kama wanavyotupenda,, Na haitatokea wao kufukuza wageni, ni wakarimu mno bhabhaa.

Mleta uzi, ubarikiwe. Namuomba Allah SWT awajaarie hawa watanzania wenzetu na mataifa mengine warudi kwao salama, karibuni sana wananzengo, nawapenda sana.
 
Ginehe bhabhaa??
Sipati picha ingelikua moja ya nchi za kiarabu yatokee haya ya "kufukuza wageni, hususani hapa bongo" i think wangejumuishwa waarabu wote ni makatili, magaidi, yanaroho mbaya, mashetani, hapo wenye udini nao wangelipuka balaa wakina fulani bhabhaa 😁😁 lakini kwakua ni wenzetu wasauzi itaonekana ni kawaida tuu bila kujumuishwa "waafrika ni makatili" 😁😁 inachekesha sana. Hebu tuwapende hawa ndugu zetu waarabu kama wanavyotupenda,, Na haitatokea wao kufukuza wageni, ni wakarimu mno bhabhaa.

Mleta uzi, ubarikiwe. Namuomba Allah SWT awajaarie hawa watanzania wenzetu na mataifa mengine warudi kwao salama, karibuni sana wananzengo, nawapenda sana.
Nenda Zanzibar kaulize uzuri historia ya hao mashoga zako waarabu.

Halafu uliza jengo la Beit el Jaib limejengwaje?
 
Nenda Zanzibar kaulize uzuri historia ya hao mashoga zako waarabu.

Halafu uliza jengo la Beit el Jaib limejengwaje?

Matola acha kukariri babaa, halafu kwanini udhanie wao ni mashoga ilihali huna uhakika wa hicho!!

Mimi sio mzanzibari, na sio mwenyeji wa zanzibar. Anaeishi zanzibar atakuja na mrejesho.
 
Matola acha kukariri babaa, halafu kwanini udhanie wao ni mashoga ilihali huna uhakika wa hicho!!

Mimi sio mzanzibari, na sio mwenyeji wa zanzibar. Anaeishi zanzibar atakuja na mrejesho.
Ni mashoga zako na una mahaba nao, elewa kiswahili rahisi kabisa.
 
Hii hapana, inategemea na aina ya kazi, SA kitu tunaita CRITICAL SKILLS, hizi ni taaluma ambazo zina uhaba hapa SA.

Mfano, Waalimu wa Hesabu/Hisabati, Sayansi kama PHYSICS nk, Wahasibu wabobezi wenye CPA, CA, CISA, ACCA nk

Mainjinia, madkati bingwa, madaktari wa mifugo nk

Kuna kada nyingi sana ambazo hapa SA hazina watu makini hivyo Serikali kupitoa Home affairs waliweka utaratibu wa kupata visa kwa kuangalia hizo taaluma.

Pia unaruhusiwa kuwa mfanyabiashara halali na kwa vibali vyote bila shida yoyote.

Ni kweli kuna uhalifu mkubwa na hii ni kwa sababu ya sera zao za tangia ubaguzi wa rangi. Nchi hii walishindwa kucontrol silaha tangu awali, yaan hata baada ya ubaguzi wa rangi kukomeshwa bado watu weusi wengi walikuwa wanamiliki silaha na hadi leo limekuwa tatizo sugu.

Kuna sheria za umiliki wa silaha na maduka yake ila kuna utaratibu kama ilivyo hapo home TZ.

Operesheni DUDULA ikiongozwa na makundi mawili makubwa ila maaraufu ni lile la N. LUX ambao wao wanachokosea ni ile kutaka uwaoneshe vibali vya kuishi ingali wao sio mamlaka ya serikali inayohusika na vibali hivyo.

Changamoto za Watanzania wa huku.

1. Hawana umoja, wengi walikuja huku kihuni hvyo hawaba vibali vya kuishi, hawana Pasipoti nk. Mbaya zaidi wengi wambao wameingia bila utaratibu ndio wamejiingiza kwenye uhalifu hasa maeneo ya KWA ZULU NATAL - DURBAN, JOBURG na PRETORIA.

2. Wengi si waelewa hata ukiwaambia twende ubalozini ukaangalie namna bora ya kupata Passport wanakataa na kuhisi watarudishwa home.

3. Watanzania wapo wema pia ambao wengi wao wana maduka hasa JOBURG, DURBAN na PRETORIA, wanasaidia sana madogo wa TZ sema ndio hivyo madogo wengi ni miyeyusho na uhuni mwingi kiasi wanaweza hata kukuibia.

4. Watanzania wachache wapo miji kama PORT ELIZABETH, CAPE TOWN, BLOEMFONTEIN nk huko pia kuna mishe ila hakuna WATZ wengi sana nilivyoona hii miji ya huku kaskazini.

Nini kifanyike, binafsi natamani sana SERIKALI YETU ikae na Ya SA wakubaliane namna ya kuwachukua raia wetu wanateseka huku, magonjwa baridi kali, usalama nk. Ningekuwa RAIS ningeshusha MABASI KAMA 6 hapa sambamba na wanajeshi wetu kama 70 hivi, hawa wasaidiana na askari wa SA kupitia ubalozi wa TZ wasakwe mji mmoja hadi mwingine warejeshwe kwa lazima home lkn bila kufunguliwa mashtaka. Maana hilo ndilo vijana wengi huogopa.

All in All maisha ya SA ni rahisi kama unajituma na umejiepusha na maeneo hatarishi, na zaidi ukifanya kazi maeneo ya Wazungu wengi basi usalama wako unakuwa mkubwa kidogo, maana maeneo ya wazungu wengi kuna rate ndogo ya uhalifu.
Wengi hawataki kusikia ukweli kuwa watz wengi walizamia bila vibali
 
duuh habari mbaya sana kuna jamaa yangu yupo safarini anaelekea huko kutafuta maisha anapaspoti na fedha kidogo za kujikimu na hamjui mtu yeyote huko
 
Wageni wote. Hata walioajiriwa kihalali wanapaswa kuondoka na kuachia nafasi kwa Wasauzi.
V/note iliyowekwa, huyo mwanamama mtangazaji hajasema wenye vibali ama hapana, yeye kasema biashara zote za "wakuja" zifungwe period
 
Kinachowatafuna South Africa na kitakachoendelea kuwatafuna zaidi ni kuwaruhusu wakaburu kumiliki Ardhi wakati sio Wazawa.

Asilimia kubwa ya Ardhi inamilikiwa na wakaburu wazawa hawana Uhuru wa nchi yao hivyo basi mkaburu anao uwezo wa kufanya chochote hata kuwalipa mishara midogo na kuajiri watu kutoka mataifa tofauti atakavyo yeye.

Kitakachokuja kutokea ni Waafrika kuumizana wenyewe kwa wenyewe imagine msouth ni muafrika akimpiga mkenya au mtanzania haitasaidia chochote zaidi ya kupoteza uhai wa mwafrika mwenzako tu.

Robert Mugabe alikua anaonekana mbaya lkn alikua sahihi kutetea Ardhi ya Taifa lake lkn kwa mtu mwenye maono ya mbali Wazungu tuishi nao tu kama wawekezaji au watalii lkn suala la kumiliki Ardhi libaki kwa wazawa bado kuna vizazi vijavyo hivi aridhi ikiuzwa kwa wageni unategemea wazawa wataishi wapi? Wanaotamani sana Africaka yetu.
 
Warudi home kumenoga
Waje wakutane na bajeti 😁

images - 2022-08-18T093512.687.jpeg
 
Back
Top Bottom