Nimeshangaa kumuona Profesa mmoja maarufu wa pale UDSM akisali sala ya Bikira Maria

Nimeshangaa kumuona Profesa mmoja maarufu wa pale UDSM akisali sala ya Bikira Maria

Moja kati ya mambo ambayo yapo wazi kabisa katika biblia ni maelekezo ya namna maombi yanatakiwa kufanywa. Agizo la maombi lipo very open.
Biblia haiongelei maombi bali inatufunulia jinsi tunavyoweza kuishi ndani ya Mungu na Yeye ndani yetu. Maria ni kielelezo cha namna Mungu anaweza kuishi ndani ya binadamu. Kumtumia kama kielelezo ni hiyari yako na pia kujiona uko na hadhi sawa na Maria ni hiyari yako.
 
Sasa ulichoandika hapa ndio agizo kwamba muwe mnamwambia Maria awaombee? Mbona unaandika vitu dhaifu namna hii?

Biblia ilikuwa imeshakamilika tangu enzi za mitume na ikaja kuwa compiled na Jarome 382 AD. Wakatoliki waliongeza hivyo vitabu miaka ya 1500s AD baada ya kushindwa kujibu hoja za Luther.

Isome imani yako badala ya kukurupuka.
Hivi Jerome alikuwa dhehebu gani?
 
Madam pole naona nimekugusa pabaya. Mimi mtu akisema hiyo ni imani yake huwa namuheshimu sana maana imani ni suala binafsi na la kikatiba.

Uko tayari nikupe challenge? Mosi, mimi suala la kuomba maria awaombee watu silichukulii kama suala la imani bali ni jambo la ufahamu. Ni simple, je hilo ni agizo la biblia? Kama sio agizo wala fundisho la kibiblia basi mimi naliweka kando.

Lakini pili, kuna jambo la hatari sana mnalifanya pale mnapoomba Maria awaombee kwasababu mnamfanya yeye kuwa omnipresent. Kwamba yupo kila mahali dunia nzima akisikiliza maombi yenu na kuyapeleka kwa Yesu. Hii ni sifa ya Mungu peke yake. No wonder mnapenda kumuita mama wa Mungu wakati mnajua fika maria hakumzaa Mungu bali alitumika tu kutengeneza mwili.

Kuhusu salam maria naona tuu wanatimiza maandiko ya malaika "vizazi vyote watakuita mbarikiwa"
Kuhusu Bikira maria kuombea wakatoliki naona huwajui wakatoliki vizuri wanawatakatifu zaidi ya 10000 na wote huwa wanasema mtakatifu flani utuombee kuna kitu yao wanaiita litania ya watakatifu wote wakianza kusema utuombee utachoka.

Nachoona huenda huwajui wakatoliki na mapokeo yao kuhusu watakatifu au ni prejudice against Mariam.
 
Ngoja niweke kapicha cha kusindikizia uzi , watu wanaacha kuabudu Mungu wa kweli Kazi kuabudu viumbe wenzao #InadikitishaSanaView attachment 2465677

Nb: Huyo picha siyo mtajwa katika uzi bali ni mfano tu jinsi gani watu wanavyoabudu kivyao kama content ya uzi unavyosema.
Dah!..
 
Kuna jambo la hatari sana mnalifanya pale mnapoomba Maria awaombee kwasababu mnamfanya yeye kuwa omnipresent. Kwamba yupo kila mahali dunia nzima akisikiliza maombi yenu na kuyapeleka kwa Yesu. Hii ni sifa ya Mungu peke yake. No wonder mnapenda kumuita mama wa Mungu wakati mnajua fika maria hakumzaa Mungu bali alitumika tu kutengeneza mwili.
Ni kuulize swali, ile stori aliyosimulia Yesu ya Lazaro na tajiri, tajiri akiwa motoni akiongea na Ibrahim na Ibrahim kumjibu mambo aliyofanya duniani na hali ya Lazaro ilivyokuwa duniani maana yake Ibrahim ni Mungu? Maana how alijua habari za tajiri na Lazaro duniani?

Mbinguni watakatifu wanaishi na Mungu, ukaribu na Mungu na kwa mapenzi ya Mungu mwenyewe wanapata uwezo huo. Hata hapa duniani zipo cases za ukweli za mtu kama Padre Pio akiwa hai kuonekana sehemu zaidi ya moja kimiujiza! Anatoa huduma sehemu moja na sehemu nyingine pia kwa wakati mmoja kimiujiza!

Kwa Mungu hakuna linaloshindikana, tatizo mnapenda kumuwekea Mungu mipaka! Nikupe mfano mwingine, kasome Ufunuo 6:7 roho zilizochinjwa chini ya madhabahu mbinguni zilimlilia Mungu "hata lini utatulipia kisasi juu ya walio juu ya nchi?" Jiulize hizo roho zimejuaje walio juu ya nchi hawajapata hukumu? Hizo roho ni Mungu sababu ya hiyo sifa ya omnipresent?


Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Nani amefundisha kuomba kwa Bikira Maria? Tunaomba atuombee kama ninavyoweza kuomba wewe uniombee. Nikiomba wewe uniombee maana yake umechukua nafasi ya Yesu?
Warumi 8:26 "kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, Lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa ".
 
Warumi 8:26 "kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, Lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa ".
Ni kweli lakini kwavile kuna hilo andiko maana yake wewe huwezi kuniombea? Sisi kuombeana maana yake tumeondoa nafasi ya Roho Mtakatifu?

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Hakuna tatizo kuombeana, Ila kumuomba mwanadamu aliyekwisha kufa kitambo (Maria) awaombee ninyi mlio hai ndio tatizo.
Mungu mwenyewe anasema "Mimi ni Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo, Si Mungu wa wafu bali walio hai". Je Ibrahim, Isaka na Yakobo sio wafu? Why Mungu aseme wapo hai?

Ndugu, kama wewe ni Mkristo tumaini kuu ni kuishi milele! Wafu kibiblia ni waliokufa ktk dhambi! Hata ukiwa hai duniani ukiwa dhambini ni mfu! Bikira Maria yu hai mbinguni pamoja na watakatifu wengine!



Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Kumshangaa MTU anamwabudu mama maria mtakatifu ni sawa kumshangaa MTU anamsujudu Muhammad aliyekuwa na totoz kibao.Mi naona kila MTU asimamie imani yake
Mwambie aende India ambako prof anamsujudia ng'ombe na kule north korea ambako wanamsujudia mnyazi aitwae kisayansi CHOLECYTOKININ PANCRYOZYMIN na msaidizi wake Pseudocanthotermes militaris
 
Wewe unamjua Mungu wa kweli?
Ndio , ni Muumba mbingu , Ardhi vilivyomo na viumbe wote hana mshirika , hafanani na kitu wala kiumbe chochote ndiye muangalizi na muendaeshaji wa ulimwengu wote.
 
Mwambie aende India ambako prof anamsujudia ng'ombe na kule north korea ambako wanamsujudia mnyazi aitwae kisayansi CHOLECYTOKININ PANCRYOZYMIN na msaidizi wake Pseudocanthotermes militaris
Achana nae mjuaji huyu
 
Hii nayo kali,kwamba Mungu naye ana mama kama sisi wanadamu?
Tunakosea sana kumuomba Maria.
Hapo Kitaalamu angekuwa mmatumbi huyo Mungu wanayedai ana Mama angekuwa asubuhi Mungu anamuamkia Mama yake "Shikamoo Mama"
 
Mi nadhani kila mtu a-mind his own business mimi nadhani hilo halikusaidii kitu
 
Mungu mwenyewe anasema "Mimi ni Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo, Si Mungu wa wafu bali walio hai". Je Ibrahim, Isaka na Yakobo sio wafu
Kutoka 3:15 " Tena Mungu akamwambia Musa waambie wana wa Israel maneno haya, Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu,Mungu wa Isaka,Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu, hilo ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote"

Hili jina ni utambulisho wa Mungu ili Waisrael wa enzi hizo wafahamu yeye ni nani....

Ndio maana tunapoomba hatusemi Ibrahimu, Isaka na Yakobo watuombee maana hata wao walikuwa wanadamu tu na walishakufa kama ilivyo kwa Maria.
 
SWALI: Je, Kuna muislamu yeyote anayekubali kuwa anaweza kuingia PEPONI bila kumkiri mtume Muhammad?, Kama yupo huyo hamwabudu MUHAMMAD.
Kama hayupo, basi wote wanamwabudu mtume MUHAMMAD..
- Kitendo Cha kuona kuwa wewe huna uzima wa milele bila mtume MUHAMMAD, wewe tayari umemwabudu mtume MUHAMMAD ( Inamaana kuwa, maisha yako hayana maana yoyote kama hukumkiri mtume MUHAMMAD. Kufanya hivyo tayari ni kuabudu).
NB:
Maisha ya binadamu ya Duniani na Peponi yanamtegemea MUNGU peke yake.
Muislamu yeyote lazima ampende mtume MUHAMMAD, amwamini mtume MUHAMMAD na amtumaini mtume MUHAMMAD ( kwa sifa hizi tayari, mtume MUHAMMAD ameabudiwa).
Hujui maana ya kuabudu, hakuna Muislamu anayesoma

1. "ewe Muhammad naomba uniondolee shida zangu "

2.Ahsante Muhammad nimefaulu mtihani

3.Muhammad mkubwa leo mvua imenyesha .

4.Ewe Muhammad naomba unisamehe zambi zangu.

5.Nk

Bali maombi yote yanaelekezwa kwa Mola mlezi muumba wa vyote mwenye hekima bila kumshirikisha na kiumbe au kitu chochote.

Nb: Muhammad (upon him be peace and blessing of Allah) yeye alikuwa kama mwalimu tu na mjumbe hana mamlaka ya kuombwa chochote kusujudiwa , kuabudiwa ,kumpa mtu madhara wala kumuondoshea mamlaka hayo ni ya Mwenyezi Mungu pekee.

Nakala moja iende kwa To yeye
 
Moja kati ya mambo ambayo yapo wazi kabisa katika biblia ni maelekezo ya namna maombi yanatakiwa kufanywa. Agizo la maombi lipo very open.

Yesu Kristo alisema mara nyingi sana kwenye injili ya Yohana kwamba tuombe kwa jina lake. Mtume Paulo ameandika tufanye yote katika jina la Yesu Kristo.

Sasa profesa ambaye ameandika paper kibao na amefanya literature review za kutosha ameshindwa kusoma biblia kufahamu tunapaswa kuomba kwa jina gani?

Hakuna sehemu hata moja mitume waliomba kwa jina la Maria. Yule Maria mama wa Yesu alikaa pamoja na mitume na walijazwa Roho Mtakatifu pamoja na wakanena kwa lugha.

Maria alimzaa Yesu lakini hakumzaa Mungu. Kuna tofauti kati ya Yesu na Kristo. Maria sio mama wa Mungu bali ni mama yake Yesu. Yesu ni mwanadamu na Kristo ni Mwana wa Mungu.

Hivyo Yesu Kristo ni Mungu na mwanadamu kwa wakati mmoja. Asomaye na afahamu.
Unashangaaa nini? Unashindwa kushangaa maprofesa wengi hapo udsm hawali nguruwe ety kwy izo dini zao wamedanganywa na watu ambao hawakuwa na hata elimu ety nguruwe ni dhambi.

Na kuna wengine wanadanganyana kwamba nyama ambayo haijachinjwa na dini Fulani siri na wakati Kila siku anatandika vibudu kwy mabucha ya uswahili na mishikaki ya vibudu anatandika vizuri
 
Kutoka 3:15 " Tena Mungu akamwambia Musa waambie wana wa Israel maneno haya, Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu,Mungu wa Isaka,Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu, hilo ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote"

Hili jina ni utambulisho wa Mungu ili Waisrael wa enzi hizo wafahamu yeye ni nani....

Ndio maana tunapoomba hatusemi Ibrahimu, Isaka na Yakobo watuombee maana hata wao walikuwa wanadamu tu na walishakufa kama ilivyo kwa Maria.
Umesema sawa kabisa kwenye ufafanuzi wa utambulisho wa Mungu lakini mimi nimenukuu kuwa Mungu anawataja hao akina Ibrahim kama walio hai si wafu! Kwanza nilitaka tukubaliane Watakatifu wapo hai alafu ndio tujadili habari za wao kuweza kutuombea! Kama bado hujaelewa kuhusu hili naweza kuleta maandiko mengi kuonesha Watakatifu wapo hai mbinguni.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom