Nimeshangaa kumuona Profesa mmoja maarufu wa pale UDSM akisali sala ya Bikira Maria

Nimeshangaa kumuona Profesa mmoja maarufu wa pale UDSM akisali sala ya Bikira Maria

Nilidhani unashangaa professa kusali kabisa.

Yani mtu amesoma halafu bado anaamini akifumba macho kuna invisible man hewani huko juu ya mawingu anamsikiliza na atakuja kumsaidia???

Kweli sisi bado tuna unyani fulani ndani yetu.
Ndomaana wanasema DNA ya Binadamu na ya nyani vinapishana 2% tu
Kwa mlinganisho huu nilitegemea nyani ndo wawe na hizi imani kwa hali ya juu ila sijawahi kuona popote nyani anasali
 
Hujui maana ya kuabudu, hakuna Muislamu anayesoma

1. "ewe Muhammad naomba uniondolee shida zangu "

2.Ahsante Muhammad nimefaulu mtihani

3.Muhammad mkubwa leo mvua imenyesha .

4.Ewe Muhammad naomba unisamehe zambi zangu.

5.Nk

Bali maombi yote yanaelekezwa kwa Mola mlezi muumba wa vyote mwenye hekima bila kumshirikisha na kiumbe au kitu chochote.

Nb: Muhammad (upon him be peace and blessing of Allah) yeye alikuwa kama mwalimu tu na mjumbe hana mamlaka ya kuombwa chochote kusujudiwa , kuabudiwa ,kumpa mtu madhara wala kumuondoshea mamlaka hayo ni ya Mwenyezi Mungu pekee.

Nakala moja iende kwa To yeye
Vizuri
 
Umesema sawa kabisa kwenye ufafanuzi wa utambulisho wa Mungu lakini mimi nimenukuu kuwa Mungu anawataja hao akina Ibrahim kama walio hai si wafu! Kwanza nilitaka tukubaliane Watakatifu wapo hai alafu ndio tujadili habari za wao kuweza kutuombea! Kama bado hujaelewa kuhusu hili naweza kuleta maandiko mengi kuonesha Watakatifu wapo hai mbinguni.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Wapo watakatifu walio hai na wapo pia waliokwisha kufa (kupumzika).

Ufunuo wa Yohana 14:13(b) "heri wafu wafao katika Bwana tangu Sasa, Naam asema Roho, wapate kupumzika baada ya tabu zao...."

Hao waliokwisha kufa hawawezi tena kukuombea maana hakuna ushirika kati ya walio hai na wafu..

Mhubiri 9:5 "kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana ijara tena, maana kumbukumbu lao limesahauliwa "..

Huyo asiye na uhai hawezi kukuombea tena.

Mathayo 22:32 (b) " Mungu si Mungu wa wafu bali wa walio hai"...
 
Yapo mambo mengi sana ukitumia logic za kibinadamu lazima uone ajabu lakini katika kuamini unafanya..
IMG_20221207_231408_457.JPG
 
Nimetunga na ninaimba wimbo wa MAMA MARIA MAMA WA YESU UTUOMBEE.

Huku duniani tupo tu ila hatuyajui mapenzi ya Mingu yako kwenye nini
Mapenzi yake huyajui? Refer.... Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani Kama huko mbinguni....
 
RC hata Amri kumi za Mungu zimebadilishwa kiasi, Biblia yao ina vitabu 72,Kiufupi wamechukua mafundisho ya Biblia wakachanganya na tamaduni za kirumi! Hili limewapa wafuasi wengi Sana Duniani
 
Kumshangaa MTU anamwabudu mama maria mtakatifu ni sawa kumshangaa MTU anamsujudu Muhammad aliyekuwa na totoz kibao.Mi naona kila MTU asimamie imani yake
Hivi kwanini nyinyi kwa nyinyi mkikabana shingo baadhi yenu hukimbilia kuwakejeli Waislam ambao hawahusiki?
 
Moja kati ya mambo ambayo yapo wazi kabisa katika biblia ni maelekezo ya namna maombi yanatakiwa kufanywa. Agizo la maombi lipo very open.

Yesu Kristo alisema mara nyingi sana kwenye injili ya Yohana kwamba tuombe kwa jina lake. Mtume Paulo ameandika tufanye yote katika jina la Yesu Kristo.

Sasa profesa ambaye ameandika paper kibao na amefanya literature review za kutosha ameshindwa kusoma biblia kufahamu tunapaswa kuomba kwa jina gani?

Hakuna sehemu hata moja mitume waliomba kwa jina la Maria. Yule Maria mama wa Yesu alikaa pamoja na mitume na walijazwa Roho Mtakatifu pamoja na wakanena kwa lugha.

Maria alimzaa Yesu lakini hakumzaa Mungu. Kuna tofauti kati ya Yesu na Kristo. Maria sio mama wa Mungu bali ni mama yake Yesu. Yesu ni mwanadamu na Kristo ni Mwana wa Mungu.

Hivyo Yesu Kristo ni Mungu na mwanadamu kwa wakati mmoja. Asomaye na afahamu.
Bora sana huyu kwa sababu ana uhakika wa uwepo wa Mungu, isipokuwa wewe na yeye tofauti yenu iko kwenye UFAHAMU wenu juu ya Mungu na si vinginevyo.

Nilishawawahi kusikia tetesi kuwa kuna mmoja ambaye hajui kama Mungu yupo na hivyo haamini kama Mungu yupo, ila anaamini kuwa Mungu hayupo. Ni tetesi lakini, sijawahi kumsikia mwenyewe kwa kinywa chake
 
Wapo watakatifu walio hai na wapo pia waliokwisha kufa (kupumzika).

Ufunuo wa Yohana 14:13(b) "heri wafu wafao katika Bwana tangu Sasa, Naam asema Roho, wapate kupumzika baada ya tabu zao...."

Hao waliokwisha kufa hawawezi tena kukuombea maana hakuna ushirika kati ya walio hai na wafu..

Mhubiri 9:5 "kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana ijara tena, maana kumbukumbu lao limesahauliwa "..

Huyo asiye na uhai hawezi kukuombea tena.

Mathayo 22:32 (b) " Mungu si Mungu wa wafu bali wa walio hai"...
Tusichanganye mambo, wewe ni Mkristo mwenye tumaini la kwenda mbinguni baada ya safari yako hapa duniani? Kama huna tumaini hilo imani yako ni bure ndugu yangu. Mbona nimekupa mfano ya waliohai mbinguni? Wametajwa wazee 24 kwenye ufunuo unawajua?

Nimetoa mfano wa Yesu juu ya razalo na tajiri ambako tumeambiwa lazaro yupo kifuani mwa Ibrahimu, huyu hayupo hai? Yesu alimuahidi yule mwizi pale msalabani kuwa leo hii utakuwa nami kwenye ufalme wa Mungu, hayupo hai?

Ukifa katika hali ya Neema unakwenda mbinguni, kule unaishi katika roho! Nimekupa mfano mwingine kutoka ufunuo ambapo roho za waliochinjwa zipo chini ya madhabahu mbinguni zimlilia Mungu juu ya hukumu kwa walio juu ya nchi, hawa hawako hai?

Nilitaka ukubali kuwa kinachokufa ni mwili ila roho inabakia hai na ikiwa mbinguni ndio Mtakatifu! Hapa sizungumzii kabisa watakatifu walio juu ya nchi maana ubishi ni watakatifu walio mbinguni.

Hebu tufunge mjadala wa uhai na kufa kama unakubali then tujadili how hao waliohai mbinguni wanaweza kutuombea.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Wapo watakatifu walio hai na wapo pia waliokwisha kufa (kupumzika).

Ufunuo wa Yohana 14:13(b) "heri wafu wafao katika Bwana tangu Sasa, Naam asema Roho, wapate kupumzika baada ya tabu zao...."

Hao waliokwisha kufa hawawezi tena kukuombea maana hakuna ushirika kati ya walio hai na wafu..

Mhubiri 9:5 "kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana ijara tena, maana kumbukumbu lao limesahauliwa "..

Huyo asiye na uhai hawezi kukuombea tena.

Mathayo 22:32 (b) " Mungu si Mungu wa wafu bali wa walio hai"...
Pia umeleta hoja mpya kuwa hatuna ushirika na watakatifu "waliokufa". Kanuni ya imani zote za mitume na ya Nicea mwisho tunakiri kuwa na ushirika na watakatifu! Sasa inawezekana Kanisa lako ni la juzi hata mambo ya kanuni ya imani huyafahamu na vile haipo kwenye biblia ndio kabisa ni giza!

Ila ngoja nikupe andiko kuonesha ushahidi wa ushirika wa watakatifu! Soma Waebrania 12 yote uelewe kwa kina ila mimi nakupa nukuu muhimu alafu uone sisi Wakristo tunavyoungana na Mungu, malaika na watakatifu...

22 Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,

23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,

24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
RC hata Amri kumi za Mungu zimebadilishwa kiasi, Biblia yao ina vitabu 72,Kiufupi wamechukua mafundisho ya Biblia wakachanganya na tamaduni za kirumi! Hili limewapa wafuasi wengi Sana Duniani
Hakuna kilichobadilika kwenye amri za Mungu. Hizo unazojua wewe na za RC ni zile zile na sio ubishi kati yetu tangu mwanzo wa uprotestant. Tafuta mchungaji aliyesoma theolojia akufundishe, kuna sehemu huchanganya wengi wakifikiri imebadilishwa.

Sasa biblia na tamaduni za kirumi ndio RC wakawa na vitabu 72? Hivi nyie mnafundishwa na nani? Hata wachungaji wenu wanaojielewa wanawashangaa! Hata Gwajima atakupa lecture tofauti na hii unayoamini.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Wapo watakatifu walio hai na wapo pia waliokwisha kufa (kupumzika).

Ufunuo wa Yohana 14:13(b) "heri wafu wafao katika Bwana tangu Sasa, Naam asema Roho, wapate kupumzika baada ya tabu zao...."

Hao waliokwisha kufa hawawezi tena kukuombea maana hakuna ushirika kati ya walio hai na wafu..

Mhubiri 9:5 "kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana ijara tena, maana kumbukumbu lao limesahauliwa "..

Huyo asiye na uhai hawezi kukuombea tena.

Mathayo 22:32 (b) " Mungu si Mungu wa wafu bali wa walio hai"...

Hakuna kilichobadilika kwenye amri za Mungu. Hizo unazojua wewe na za RC ni zile zile na sio ubishi kati yetu tangu mwanzo wa uprotestant. Tafuta mchungaji aliyesoma theolojia akufundishe, kuna sehemu huchanganya wengi wakifikiri imebadilishwa.

Sasa biblia na tamaduni za kirumi ndio RC wakawa na vitabu 72? Hivi nyie mnafundishwa na nani? Hata wachungaji wenu wanaojielewa wanawashangaa! Hata Gwajima atakupa lecture tofauti na hii unayoamini.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Nimekuwekea hapo chini, Amri ya pili kwenye Biblia inasema usijifanyie sanamu ya kuchonga (idol).

Kwa RC amri ya pili inasema usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako !
Kwenye Bible USIZINI ni amri ya Saba wakati kwa RC ni amri ya Sita. Naomba ufafanuzi wako
IMG_20230102_125907.JPG
 
Moja kati ya mambo ambayo yapo wazi kabisa katika biblia ni maelekezo ya namna maombi yanatakiwa kufanywa. Agizo la maombi lipo very open.

Yesu Kristo alisema mara nyingi sana kwenye injili ya Yohana kwamba tuombe kwa jina lake. Mtume Paulo ameandika tufanye yote katika jina la Yesu Kristo.

Sasa profesa ambaye ameandika paper kibao na amefanya literature review za kutosha ameshindwa kusoma biblia kufahamu tunapaswa kuomba kwa jina gani?

Hakuna sehemu hata moja mitume waliomba kwa jina la Maria. Yule Maria mama wa Yesu alikaa pamoja na mitume na walijazwa Roho Mtakatifu pamoja na wakanena kwa lugha.

Maria alimzaa Yesu lakini hakumzaa Mungu. Kuna tofauti kati ya Yesu na Kristo. Maria sio mama wa Mungu bali ni mama yake Yesu. Yesu ni mwanadamu na Kristo ni Mwana wa Mungu.

Hivyo Yesu Kristo ni Mungu na mwanadamu kwa wakati mmoja. Asomaye na afahamu.
Ukiwa haujui halafu unaconfidence kuwa unajua huwa inachekesha sana, nakumwelimisha mtu huyo ni ngumu sana, mwenyehekima unamwacha tu na elimu yake mbovu hakosi huko mbele akaumia maana hana namna nyingine ya kujifunza isipokuwa kuumia, uchungu huo utakuwa mwalimu tosha kuliko kuumpa elimu wakati shingo imeshupaa
 
SWALI: Je, Kuna muislamu yeyote anayekubali kuwa anaweza kuingia PEPONI bila kumkiri mtume Muhammad?, Kama yupo huyo hamwabudu MUHAMMAD.
Kama hayupo, basi wote wanamwabudu mtume MUHAMMAD..
- Kitendo Cha kuona kuwa wewe huna uzima wa milele bila mtume MUHAMMAD, wewe tayari umemwabudu mtume MUHAMMAD ( Inamaana kuwa, maisha yako hayana maana yoyote kama hukumkiri mtume MUHAMMAD. Kufanya hivyo tayari ni kuabudu).
NB:
Maisha ya binadamu ya Duniani na Peponi yanamtegemea MUNGU peke yake.
Muislamu yeyote lazima ampende mtume MUHAMMAD, amwamini mtume MUHAMMAD na amtumaini mtume MUHAMMAD ( kwa sifa hizi tayari, mtume MUHAMMAD ameabudiwa).
Nafikiri Mtume tumuache hapa hahusiki. Waislam wanamuheshimu sana Mariam na Wakatoliki pia. Hivi vidhehebu vya siku hizi ndivyo havieleweki. Tuviache viwepo mpaka vitakavyoondoka kwa nguvu za Mungu. Tuhubiri upendo na Amani.
 
mtoa mada Ni mpumbavu...Kama hujui wokovu wa ulimwengu ulianza na hiyo Sala ya salamu Maria......
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanaye wa pekee ili kila amwaminiye (mwanaye) asipotee bali awe na uzima wa milele. Bishaneni lakini, msisahau concept nzima ni KUMUAMINI KRISTO
 
Nimekuwekea hapo chini, Amri ya pili kwenye Biblia inasema usijifanyie sanamu ya kuchonga (idol). Kwa RC amri ya pili inasema usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako !
Kwenye Bible USIZINI ni amri ya Saba wakati kwa RC ni amri ya Sita. Naomba ufafanuzi wako
Ndugu yangu, kabla ya hukumu ni vizuri kufanya hata utafiti uelewe. Amri za Mungu kwenye Biblia Mungu hakuzipanga kama zilivyopangwa leo. Kasome Kutoka 20 uone ilivyo. Mpangilio wa 1 hadi 10 kuna makanisa ya Protestant na Kanisa la Orthodox waliamua kufata mpangilio uliowekwa na Origen na Kanisa Katoliki na baadhi ya Protestants hasa Lutheran tumefuata mpangilio wa Mt Augustine.

Kwa jinsi amri za Mungu zilivyoandikwa hata mimi na wewe tungeweza kupanga amri hata 20 sio kumi tu. Ukiangalia logic ya Origen kutenga amri ya kwanza na ya pili haina maana sababu ujumbe mkuu wa Mungu ni kutaka aabudiwe yeye tu, sasa hiyo usifanye sanamu n.k ujumbe ni ule ule! Ndio maana Mt Augustine yeye huo ujumbe wote aliona unatosha kwenye amri ya kwanza.

Pia Mt Augustine ametenga usitamani mke asiye wako kama no.9 na usitamani mali ya mwingine no.10 wakati Origen amezichanganya kuwa amri moja no.10. Logic ya Mt Augustine ni kutochanganya kutamani mke na vitu vingine vilivyotajwa ambavyo ni mali na kuzipa amri tofauti.

Kasome kutoka 20 utaona ilivyoandikwa na kuelewa. Sitegemei mjadala kwenye hili kwa mtu muelewa labda iwe ubishi tu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Ngoja niweke kapicha cha kusindikizia uzi , watu wanaacha kuabudu Mungu wa kweli Kazi kuabudu viumbe wenzao #InasikitishaSanaView attachment 2465677

Nb: Huyo picha siyo mtajwa katika uzi bali ni mfano tu jinsi gani watu wanavyoabudu kivyao kama content ya uzi unavyosema.
Allah ndie aliwaaminisha watu masanamu yanakaa kwenye nyumba za ibada, akabadili masanamu mpaka sasa amebakiwa na li moja lipo Maka

Koran 34:13. Hao majini wakifanya atakacho Suleiman, kama misikiti kwa ajili ya ibada, na masanamu,....
 
Back
Top Bottom