Imalamawazo
JF-Expert Member
- Jul 27, 2021
- 1,343
- 3,269
Biblia haiongelei maombi bali inatufunulia jinsi tunavyoweza kuishi ndani ya Mungu na Yeye ndani yetu. Maria ni kielelezo cha namna Mungu anaweza kuishi ndani ya binadamu. Kumtumia kama kielelezo ni hiyari yako na pia kujiona uko na hadhi sawa na Maria ni hiyari yako.Moja kati ya mambo ambayo yapo wazi kabisa katika biblia ni maelekezo ya namna maombi yanatakiwa kufanywa. Agizo la maombi lipo very open.
Hivi Jerome alikuwa dhehebu gani?Sasa ulichoandika hapa ndio agizo kwamba muwe mnamwambia Maria awaombee? Mbona unaandika vitu dhaifu namna hii?
Biblia ilikuwa imeshakamilika tangu enzi za mitume na ikaja kuwa compiled na Jarome 382 AD. Wakatoliki waliongeza hivyo vitabu miaka ya 1500s AD baada ya kushindwa kujibu hoja za Luther.
Isome imani yako badala ya kukurupuka.
Madam pole naona nimekugusa pabaya. Mimi mtu akisema hiyo ni imani yake huwa namuheshimu sana maana imani ni suala binafsi na la kikatiba.
Uko tayari nikupe challenge? Mosi, mimi suala la kuomba maria awaombee watu silichukulii kama suala la imani bali ni jambo la ufahamu. Ni simple, je hilo ni agizo la biblia? Kama sio agizo wala fundisho la kibiblia basi mimi naliweka kando.
Lakini pili, kuna jambo la hatari sana mnalifanya pale mnapoomba Maria awaombee kwasababu mnamfanya yeye kuwa omnipresent. Kwamba yupo kila mahali dunia nzima akisikiliza maombi yenu na kuyapeleka kwa Yesu. Hii ni sifa ya Mungu peke yake. No wonder mnapenda kumuita mama wa Mungu wakati mnajua fika maria hakumzaa Mungu bali alitumika tu kutengeneza mwili.
Dah!..Ngoja niweke kapicha cha kusindikizia uzi , watu wanaacha kuabudu Mungu wa kweli Kazi kuabudu viumbe wenzao #InadikitishaSanaView attachment 2465677
Nb: Huyo picha siyo mtajwa katika uzi bali ni mfano tu jinsi gani watu wanavyoabudu kivyao kama content ya uzi unavyosema.
Ni kuulize swali, ile stori aliyosimulia Yesu ya Lazaro na tajiri, tajiri akiwa motoni akiongea na Ibrahim na Ibrahim kumjibu mambo aliyofanya duniani na hali ya Lazaro ilivyokuwa duniani maana yake Ibrahim ni Mungu? Maana how alijua habari za tajiri na Lazaro duniani?Kuna jambo la hatari sana mnalifanya pale mnapoomba Maria awaombee kwasababu mnamfanya yeye kuwa omnipresent. Kwamba yupo kila mahali dunia nzima akisikiliza maombi yenu na kuyapeleka kwa Yesu. Hii ni sifa ya Mungu peke yake. No wonder mnapenda kumuita mama wa Mungu wakati mnajua fika maria hakumzaa Mungu bali alitumika tu kutengeneza mwili.
Warumi 8:26 "kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, Lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa ".Nani amefundisha kuomba kwa Bikira Maria? Tunaomba atuombee kama ninavyoweza kuomba wewe uniombee. Nikiomba wewe uniombee maana yake umechukua nafasi ya Yesu?
Ni kweli lakini kwavile kuna hilo andiko maana yake wewe huwezi kuniombea? Sisi kuombeana maana yake tumeondoa nafasi ya Roho Mtakatifu?Warumi 8:26 "kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, Lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa ".
Hakuna tatizo kuombeana, Ila kumuomba mwanadamu aliyekwisha kufa kitambo (Maria) awaombee ninyi mlio hai ndio tatizo.Ni kweli lakini kwavile kuna hilo andiko maana yake wewe huwezi kuniombea? Sisi kuombeana maana yake tumeondoa nafasi ya Roho Mtakatifu?
Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Mungu mwenyewe anasema "Mimi ni Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo, Si Mungu wa wafu bali walio hai". Je Ibrahim, Isaka na Yakobo sio wafu? Why Mungu aseme wapo hai?Hakuna tatizo kuombeana, Ila kumuomba mwanadamu aliyekwisha kufa kitambo (Maria) awaombee ninyi mlio hai ndio tatizo.
Mwambie aende India ambako prof anamsujudia ng'ombe na kule north korea ambako wanamsujudia mnyazi aitwae kisayansi CHOLECYTOKININ PANCRYOZYMIN na msaidizi wake Pseudocanthotermes militarisKumshangaa MTU anamwabudu mama maria mtakatifu ni sawa kumshangaa MTU anamsujudu Muhammad aliyekuwa na totoz kibao.Mi naona kila MTU asimamie imani yake
Ndio , ni Muumba mbingu , Ardhi vilivyomo na viumbe wote hana mshirika , hafanani na kitu wala kiumbe chochote ndiye muangalizi na muendaeshaji wa ulimwengu wote.Wewe unamjua Mungu wa kweli?
Achana nae mjuaji huyuMwambie aende India ambako prof anamsujudia ng'ombe na kule north korea ambako wanamsujudia mnyazi aitwae kisayansi CHOLECYTOKININ PANCRYOZYMIN na msaidizi wake Pseudocanthotermes militaris
Hapo Kitaalamu angekuwa mmatumbi huyo Mungu wanayedai ana Mama angekuwa asubuhi Mungu anamuamkia Mama yake "Shikamoo Mama"Hii nayo kali,kwamba Mungu naye ana mama kama sisi wanadamu?
Tunakosea sana kumuomba Maria.
Kutoka 3:15 " Tena Mungu akamwambia Musa waambie wana wa Israel maneno haya, Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu,Mungu wa Isaka,Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu, hilo ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote"Mungu mwenyewe anasema "Mimi ni Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo, Si Mungu wa wafu bali walio hai". Je Ibrahim, Isaka na Yakobo sio wafu
Hujui maana ya kuabudu, hakuna Muislamu anayesomaSWALI: Je, Kuna muislamu yeyote anayekubali kuwa anaweza kuingia PEPONI bila kumkiri mtume Muhammad?, Kama yupo huyo hamwabudu MUHAMMAD.
Kama hayupo, basi wote wanamwabudu mtume MUHAMMAD..
- Kitendo Cha kuona kuwa wewe huna uzima wa milele bila mtume MUHAMMAD, wewe tayari umemwabudu mtume MUHAMMAD ( Inamaana kuwa, maisha yako hayana maana yoyote kama hukumkiri mtume MUHAMMAD. Kufanya hivyo tayari ni kuabudu).
NB:
Maisha ya binadamu ya Duniani na Peponi yanamtegemea MUNGU peke yake.
Muislamu yeyote lazima ampende mtume MUHAMMAD, amwamini mtume MUHAMMAD na amtumaini mtume MUHAMMAD ( kwa sifa hizi tayari, mtume MUHAMMAD ameabudiwa).
Unashangaaa nini? Unashindwa kushangaa maprofesa wengi hapo udsm hawali nguruwe ety kwy izo dini zao wamedanganywa na watu ambao hawakuwa na hata elimu ety nguruwe ni dhambi.Moja kati ya mambo ambayo yapo wazi kabisa katika biblia ni maelekezo ya namna maombi yanatakiwa kufanywa. Agizo la maombi lipo very open.
Yesu Kristo alisema mara nyingi sana kwenye injili ya Yohana kwamba tuombe kwa jina lake. Mtume Paulo ameandika tufanye yote katika jina la Yesu Kristo.
Sasa profesa ambaye ameandika paper kibao na amefanya literature review za kutosha ameshindwa kusoma biblia kufahamu tunapaswa kuomba kwa jina gani?
Hakuna sehemu hata moja mitume waliomba kwa jina la Maria. Yule Maria mama wa Yesu alikaa pamoja na mitume na walijazwa Roho Mtakatifu pamoja na wakanena kwa lugha.
Maria alimzaa Yesu lakini hakumzaa Mungu. Kuna tofauti kati ya Yesu na Kristo. Maria sio mama wa Mungu bali ni mama yake Yesu. Yesu ni mwanadamu na Kristo ni Mwana wa Mungu.
Hivyo Yesu Kristo ni Mungu na mwanadamu kwa wakati mmoja. Asomaye na afahamu.
Umesema sawa kabisa kwenye ufafanuzi wa utambulisho wa Mungu lakini mimi nimenukuu kuwa Mungu anawataja hao akina Ibrahim kama walio hai si wafu! Kwanza nilitaka tukubaliane Watakatifu wapo hai alafu ndio tujadili habari za wao kuweza kutuombea! Kama bado hujaelewa kuhusu hili naweza kuleta maandiko mengi kuonesha Watakatifu wapo hai mbinguni.Kutoka 3:15 " Tena Mungu akamwambia Musa waambie wana wa Israel maneno haya, Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu,Mungu wa Isaka,Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu, hilo ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote"
Hili jina ni utambulisho wa Mungu ili Waisrael wa enzi hizo wafahamu yeye ni nani....
Ndio maana tunapoomba hatusemi Ibrahimu, Isaka na Yakobo watuombee maana hata wao walikuwa wanadamu tu na walishakufa kama ilivyo kwa Maria.