Asante mkuu,Debora aliniuma mno kaonewa sana
Ni jina la kawaida kwa waelewa na wastaarabu ila kwa wale wakurupukaji wafia dini ni dhambi kubwa mno kwao hata kulitamka tu wakati sio dini yao wanaona unataka shari
Deborah alikosea na bahati mbaya alikutana na Waislam wajinga wenye jazba. Ni fundisho kuwa usifanye jambo la kijinga mbele ya Waislam wajinga wenye jazba, kiukweli watakuumiza.
Hilo jina sio baya, hujaelewa vizuri tu mkuu. Wanaofahamu kiarabu wanaelewa. Huyo mchezaji hilo jina lake la pili lililomchanganya muanzisha uzi ni عطية الله (‘Atwiyatullah) likimaanisha “Zawadi ya Allah” au “Kilichotolewa na Allah” Kimemchanganya namna lililovyoandikwa kwa herufi anazozielewa akadhani amepata hoja ya kuja kubishana hapa jukwaani. Ni kama عبد الله katika herufi za kilatini kuna wanaoandika Abdullah kuna wanaoandika Abd Allah. Sasa mleta mada akiona “Abd Allah” atasema huyo mtu kaitwa Allah. Haelewi.
Kilichokatazwa ni mtu kuitwa majina ambayo ni maalum kwa ajili ya Allah tu. Mfano haifai mtu kuitwa Allah au akaitwa Al-Ahad (Mmoja Pekee) au Ar-Razzaq (Mwenye kuruzuku) au Al-Khaaliq (Muumbaji) na mengine mfano wa hayo.
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimbadilisha mtu aliyesilimu aliyekuwa akiitwa Abul-Hakam (baba wa Hukumu) akimwambia kuwa Allaah Pekee Ndiye Mwenye sifa hiyo ya Al-Hakam, na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza kama ana watoto na majina yao, yule mtu akataja wanawe watatu, Shurayh, Muslim na 'Abdullaah. Basi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Kuanzia leo wewe ni Abuu Shurayh.” [Abu Daawuwd].
Lakini yapo majina ambayo ni sifa za Allah lakini pia ni ya Wanaadamu. Mfano jina Maalik (Mfalme). Hilo yafaa kumpa mtu.
Wanaopewa majina ya Allah hutanguliwa na “Abd” yaani “Mja”. Mfano Abdullah (Mja Wa Allah) au ‘Abdur Rahmaan (Mja wa Mwingi wa Rahma) au Abdur Razzaq (Mja wa Mwenye Kuruzuku) na kadhalika.