Nimeshindwa kwenda kumzika Mama haya maisha hayako fair naombeni msaada😭

Mimi nimehisi shida yake ni genuine ndio maana nikatoa kitu kidogo nilichonacho japokuwa kapuku, kama katutapeli basi bwana. Kama hukuguswa kumtolea chochote is understandable but kumsema mtu ni tapeli bila kuwa na evidence ni uonevu.
 

Chai.

Haiwezekani ndugu washindwe kukuchangia nauli ya kukufikisha huko hali ya kuwa wewe ndiye mlengwa mkuu .
 
Kwamba Dr umenifanyia diagnosis tayari? Kweli Tanzania ina madokta.

Haya tuendelee, wenye kutoa nauli kijana akamxzike mzazi tutoe, wenye kutaka kusubiri habari kamili ili wachangie tusubiri.

Kila mtu afanye kile moyo wake unamgusa kufanya.
 
Ombaomba wa mjini wale ni walemavu, usimfananishe na huyu ambaye ni mzima na ana nguvu zake.
Kitu kingine unapaswa kukijua David humu sio wote ni wazima, humu kuna walemavu wa viungo, walemavu wa ngozi, kuna viziwi, mabubu, kuna wagonjwa wa akili, kuna wagonjwa wa stroke, kuna watu waliofilisika, n.k usione tunakutana jukwaan ukadhani sote ni wazima hapana.
 
Kwamba Dr umenifanyia diagnosis tayari? Kweli Tanzania ina madokta.

Haya tuendelee, wenye kutoa nauli kijana akamxzike mzazi tutoe, wenye kutaka kusubiri habari kamili ili wachangie tusubiri.

Kila mtu afanye kile moyo wake unamgusa kufanya.
Na hili ulipaswa kulifahamu tangu mwanzo, "kila mtu afanye kile moyo wake unamgusa"

Umeona faida ya kumeza dawa kwa wakati eeh,
Uwe na asubuhi njema.
 
Na hili ulipaswa kulifahamu tangu mwanzo, "kila mtu afanye kile moyo wake unamgusa"

Umeona faida ya kumeza dawa kwa wakati eeh,
Uwe na asubuhi njema.
Ukisema hivyo manake hupaswi kuwa na argument humu, Dr wa wapi wewe usiyependa kuwa challenged? Wewe umeona kutoa bila kuhoji ni sawa, mimi nasema huyu anaweza kuwa muongo maana wengi humu wamekuwa waongo.

Unadhani nani kati yetu anahitaji dozi ndugu Dr wa mchongo?

Siku njema pia!!
 
Mimi nimehisi shida yake ni genuine ndio maana nikatoa kitu kidogo nilichonacho japokuwa kapuku, kama katutapeli basi bwana. Kama hukuguswa kumtolea chochote is understandable but kumsema mtu ni tapeli bila kuwa na evidence ni uonevu.
Upo sahihi Becky na nina uhakika umejisikia amani baada ya kumshika mkono, iwe muongo ama mkweli atajua yeye na nafsi yake, na kuna matukio humu ya nyuma watu walikuja kuomba misaada wakabezwa mmoja alikufa kwa kansa mwengine alijinyonga, watu walijilaumu sana juu ya watu wale, nadhani ibaki kua anayesaidia asaidie kwa amani ya moyo wake, asiyesaidia asisaidie kwa amani ya moyo wake pia kuliko kuitana majina bila ushahidi.
 
Tujitahidi kuwa kwenye vikundi vya kusaidiana mitaani tunamoishi haya maisha ya kujifanya private yatawamaliza , majanga hutokea ghafla bila kutarajia hata vikundi vya kuchangiana ukiwa na shida unakopa humo bila tatizo lolote
 
Jamaa ajakimbia hawezi kushika simu aingie Jf na yupo na majonzi ya kufiwa , ichukuliwe namba pale juu mpigie na uletwe mlejesho hapa watu watulie, ni rahisi kuongea na cm kuliko kuchat na upo msibani ,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…