View attachment 3689603
Mtu mzima anakuja JamiiForums kuomba elfu tatu (3,000) ya kula na familia yake! Hivi huyu mtu yuko serious kweli na maisha yake? Leo umepewa hiyo elfu tatu, umekula na familia yako, pesa imeisha. Sasa kesho mtakula nini? Na kesho kutwa je, utaendeleaje kuendesha maisha ya familia yako?
Shida nyingine ni kujiendekeza na kukubali kujivua utu wako mwenyewe. Maisha yana changamoto, lakini si kila changamoto unatakiwa kuikimbilia kwa kuomba omba bila kuwa na mpango wa kujikwamua.
Ukiendelea na huu uduanzi, ipo siku hata mkeo atakukimbia, kwa sababu unadhalilisha familia yako mwenyewe. Mwanaume mwenye familia anapaswa kufikiria namna ya kujikwamua kiuchumi na kujenga kesho bora, badala ya kuifanya familia yake iishi kwa kutegemea huruma za watu kila siku.