Nimeshuhudia mtu akiwanga, hili limenitisha

Asante naona umeongeza maelezo mengine ya ziada ambayo hayakuwepo kwenye andiko la mwanzo:
Labda nisaidie kunielimisha KUWANGA ni nini? na faida zake ni zipi kwa naefanya hivyo na hasara au madhara kwa anaefanyiwa ni yapi?
Kuwanga kwa tafsiri ya maana halisi sijui ila kunahusiana moja kwa moja na imani za kishirikina.
 
ID yako nilidhani location California au chicago

kumbe upo hapa kwetu ......hahahah pole mkuu I wish nione hicho kitu maana mpaka sasa

sina hofu na kifo maana kifo kipo sehemu yoyote ile
 
Uko salama.
 
Yaani unamuogopa binadamu anaechoma moto sehemu
Kama unamuamini bianadamu basi utahangaika sana kwenye maisha yako
Lakini kama imani yako iko kwa Mungu basi hutapatwa na kitu ila kwa uwezo wake

Hapo mimi ningemtokea na fimbo na kumcharaza kama akizingua
Usimuogope binadamu mwenzio
 
mikwara mingi ndugu yangu, hubishagi kwa hoja
 
Uko dar ni shda, mara ya kwanza nilishuhudia mtu akipasua nazi adharani huko, pia nilishuhudia kuku akinyofolewa shingo kwa mkono alafu damu inaelekezewa kichwani kwa binti mmoja, sijui ndio alikua anazindikwa!
 
Binadamu yeyote ana nguvu ya Mungu ndani yake mana ameumbwa kwa mfano wa Mungu.Ile nguvu ya Mungu iliyopo ndani yake inazuia ushirikina au uchawi/ulozi /uwanga kumuingia,mpaka yeye mwenyewe kwa kujua ama kutokujua afungue mlango kuruhusu uchawi/ulozi/ushirikina /uwanga huo umuingine.

Hii ni sawa na kusema Binadamu yeyote yule uchawi hauwezi kumdhuru kimpata mpaka yeye mwenyewe afungulie mlango wa kuruhusu kuingiliwa na uchawi kumpata.
Ni kwa namna gani basi binadamu huyu mwenye asili ya pumzi ya uhai kitoka kwa Mungu Roho ya Mungu yenye nguvu kubwa ndani yake pasipo hata yeye mwenyewe kujua nguvu aliyonayo anaweza kufungulia mlango kuruhusu kuingiliwa na uchawi kwa kifanya yafuatayo kwa kujua ama kutokujua....

1)HOFU,WASIWASI/WOGA ..mchawi au mwaga mshirikina mlozi huwa anakawaida ya kufanya vitendo vyake akishirukiana na roho chafu za majini anapokuja kuwanga kwako..anaweza akatoa sauti ya milioa ya KISHINDO kama nyayo za w
miguu ya watu wakitembea juu ya paa/dari ya nyumba/chumba chako,au SAUTI YA PAKA wanalia kama watoto wachanga ,au upepo mkali kimbunga chochote au kusikia watu wanatembea ndani au vyombo vinagongana au sauti za ajabu....LENGO la hivyo vyote ni ili wewe UPATE WASIWASI/HOFU/WOGA /UTETEMEKE....ukishaingia tu hofu woga wasiwasi kutetemeka ...TAYARI UNAKUWA UMESHAFUNGUA MLANGO wa yeye kupitisha ulozi na kukupata...mana utakuwa umeruhusu mwenyewe....BIBLIA IMEANDIKA NENO USIOGOPE ZAIDI YA MARA 366 sawa na siku za mwaka mzima ,ishi kila siku ya mwaka kwa miaka yote BILA KUOGOPA ...USIOGOPE....

2)njia nyingine ya kuruhusu kufungua mlango wa ushirikina kukupata ni kwenda kwa waganga wa jadi ..kuchanja chale,ibada za mizimu,matambiko,dawa za waganga wa kienyeji...kalumanzila..kupiga ramli ,kuoga ,kombe ,hirizi,wasoma nyota,kisomo kitabu cha yasin ,wapunga pepo....n.k
zipo nyingi acha niishie hapa..

HONGERA SANA KWA KUTOKUOGOPA umefanya vizuri sana,siku nyingine toka nje kwa ujasiri chukua jiwe piga hilo paka linalolia hapo kwenye dirisha lako ,kwa jina la Mungu piga bila hofu,kesho huyo paka mtu mchawi ataumwa yeye japo wewe uliona umepiga paka lakini umepiga mtu mwanga ,kesho ataugua na anaweza hata akafa.USIOGOPE.
Endelea kumwamini MUNGU sali kabla ya kulala,ishi maisha ya haki,toba ,jiepushe na dhambi,MUNGU ANATUSAIDIA.
 
Hujathibitisha chochote.
 
Naskiaga watu wanasema wachawi wakijua umewaona wanakuua ngoja tusubiri matokeo
 
Hizi story za mauchawi naona zimeanza kuota mzizi hapa JF siku hizi... haya bana... tunasubiri na we uje na episode ya pili
 
Huko kwenu ni wapi maana sisi wengine huo muda bado wauza chips na mishikaki wapo live na pilika za kusaka shekeli zinaendelea..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…