Nimesikitika baada ya kuona Nigeria ina GDP karibu mara tano ya Tanzania

Singapore,Israel, Switzerland, Taiwan, Luxembourg, Korea Kusini na Japan wametuzidi.
 
Wapo milioni 220 Nigeria, kumbuka kuwa wingi wa watu ni mtaji tosha.
Canada wako milioni 40, Korea Kusini million 50, Finland milioni 5 na yote haya ni mataifa bora sana

Pakistan wako milioni 230, Bangladesh millioni 170, Ethiopia milioni 120, DRC milioni 100 na yote haya ni mataifa ya hovyo tu.
 
Unabisha nini Sasa Mzee? Kulisha population kubwa kama hiyo unadhani wanahitaji uzalishaji kiasi gani? Automatically tuu GDP itakuwa kubwa.

Pili idadi hiyo ya watu inakuhakikiahia soko ambalo ndio kitu Cha muhimu kabisa
Haijawa automatically kubwa kwa DRC na Ethiopia.
 
Swala hapa sio ku reflect uhalisia wa Maisha Bali size ya uchumi ambayo inapimwa Kwa GDP.
South Korea, Ujerumani, Finland, Netherlands, Norway, Denmark na Canada zina uchumi mkubwa hadi kuwa donor countries zikiwa na population ndogo.
 
Huelewi kuwa UK uchumi wao wote umetokana na mali walizoiba dunia nzima, Tanzania ikiwemo?

Unafikiri walikuwa wanakaa bure kwa miaka 40 hapa?
Singapore, Canada na Korea Kusini waliotuzidi kwa mbali sana walimuibia nani??
 
Singapore, Canada na Korea Kusini waliotuzidi kwa mbali sana walimuibia nani??
Canada unauliza tena? Huelewi kuwa Canada mpaka leo hii ni nchi ya wahamiaji? Kama ilivyo USA na Australia. Hata Singapore ni nchi ya wahamiaji.

Korea Kusini ni vibaraka wa USA, makampuni makubwa yote huko yanamilikiwa kwa asilimia kubwa na USA.
 
Singapore,Israel, Switzerland, Taiwan, Luxembourg, Korea Kusini na Japan wametuzidi.
Hao Wametuzidi eneo la Teknolojia na ujuzi na maarifa Kwa rasilimali watu.

Nigeria inategemea rasilimali za Asili ambazo ni mafuta ndio Wametuzidi.
 
South Korea, Ujerumani, Finland, Netherlands, Norway, Denmark na Canada zina uchumi mkubwa hadi kuwa donor countries zikiwa na population ndogo.
Acha kukurupuka.

Germany & South Korea wana popn kubwa kuzidi Tanzania na Wametuzidi Uchumi.

Ukitoa Finland Nchi zilizosalia hapo ni Tajiri mkubwa wa gas na mafuta plus teknolojia na Skilled Labor

Harafu acha kulinganisha Nchi za Wazungu na Africa
 
Ukubwa wa DRC na population yake ni very sparsely populated

Ethiopia imetuzidi GDP na push Yao kubwa na population
Urusi wako milioni 144 na ndio nchi kubwa zaidi duniani, Canada wako milioni 40 na nchi kubwa karibia mara 5 ya DRC.
 
Canada unauliza tena? Huelewi kuwa Canada mpaka leo hii ni nchi ya wahamiaji? Kama ilivyo USA na Australia. Hata Singapore ni nchi ya wahamiaji.

Korea Kusini ni vibaraka wa USA, makampuni makubwa yote huko yanamilikiwa kwa asilimia kubwa na USA.
Hata Haiti, Jamaica, Honduras, Bolivia , El Salvador na Nicaragua ni nchi za wahamiaji.
 
Wala usisikitike mkuu, wizi na upumbavu ndio unatuweka kwenye kundi la masikini yaani hata wanyama wana milo mitatu

Nigeria wana export bidhaa nyingi sana na wana crude oil, wana mafuta na gas wanauza nje pia wana vyakula kibao wanauza nje mpaka cocoa
Sasa sisi wanaona bora mkulima wa machungwa wa Muheza aweke barabarani kama mlima na kusubiri mabasi yapite auze na mengine kuozea hapo ila hamuwezi kuleta hata Ulaya au Uarabuni

Halafu kuna watu wanauliza eti nani katuroga
Nani awaroge wakati kuna viongozi wanaona umasikini wenu ndio mtaji wao
 
Umenena vzr mkuu
 
Tatizo kwetu mpaka mwizi wa mabilioni amuombe tajiri mmoja awekeze kwenye fukwe au ajenge mahoteli ya kifahari nae akiwa mfadhili wa kujificha maana ni mwizi

Sasa unategemea nani atakubali kuzipokea hizo hela huku akijua kesho anaweza kugeukwa na huyo huyo mwizi atapofukuzwa kazi

Africa nchi nyingi ni magumashi hatutaki kufuata utaratibu wa haki
Ukiomba wewe hupati na utaambiwa una hela wewe

Ila roho mbaya wameona wale waliojenga vibanda kama mazizi ya mbuzi kwa miaka 30 wawaondoe leo na utakuta kuna jizi linawekeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…