Shida yetu ni zaidi ya uongozi, tuache kulaumu uongozi tu.
Nakubaliana nawe. Naelewa "Noblesse Oblige". Waliopewa talanta nyingi zaidi watadaiwa marejesho mengi zaidi, hata mwanafalsafa Yesu alituambia hili katika mfano wake.
Uongozi una lawama kubwa kabisa na za awali kabisa. Hilo halina ubishi. Lakini, uongozi haujiweki wenyewe. Watu wanaoongozwa pia wana sehemu ya lawama kwa kujiruhusu kuwa na uongozi huu. People get the leadership they deserve. Else they remove that leadership and put one that they deserve.
Kwa kila rais mmoja anayeiba kura, kuna maelfu na maelfu ya wasimamizi wa uchaguzi mpaka majaji walio katika tume ya uchaguzi wanaoshiriki wizi huu.
Kuna wananchi mamilioni wanaoona wanaibiwa kura lakini wanakubali kikondoo na kusema hewala heeala tu.
Kuhusu wingi wa watu;
Wingi wa watu kama hujajipanga kuwatumia hao watu kuzalisha ni tatizo.
Kwa maana utakuwa na watu wengi wa kuwalisha nankuwahudumia wakati hawazalishi.
Bongo watu wanamaliza chuo na kukaa miaka mitano mpaka kumi wanatafuta kazi. Yani hapo hata mtu akipata kazi, usomi ushapotea anabaki kuwa Mmachinga tu.
Sasa hapo wingi wa watu utasaidia nini?
Pia, kusema Tanzania tunawazidi Kenya kwa wingi wa watu , obviously Tanzania ni nchi kubwa, so kuongelea wingi wa watu tu unarudi kule kule kwenye kuongelea GDP.
What is the population density? What about arable land? How many people are employed? How many are in disguised unemployment? How many are productive (population minus children, the eledery, the infirm)
Unaweza kuwa na nchi ina watu wachache, lakini ina wazalishaji wengi na watoto/wazee/wagonjwa wachache, na unaweza kuwa na nchi ina watu wengi, lakini wqzalishaji wachache, wengi ni watoto/wazee/ wagonjwa.
So, wingi wa watu tu hautuoneshi kitu specifically hata kama unaweza kuwa indicator in similar countries under ceteris paribus.