Nimesikitika baada ya kuona Nigeria ina GDP karibu mara tano ya Tanzania

Nimesikitika baada ya kuona Nigeria ina GDP karibu mara tano ya Tanzania

Dhahabu nyeusi inaitajirisha Nigeria, japo raia wake wengi masikini.
Kumbe nchi yetu imezidiwa kiasi hiki na nchi yenye boko haram? Yaani kweli wao wanakaribia gdp ya bilioni 400 usd wakati sisi tupo kwenye bilioni 80s usd?
 
Kumbe nchi yetu imezidiwa kiasi hiki na nchi yenye boko haram? Yaani kweli wao wanakaribia gdp ya bilioni 400 usd wakati sisi tupo kwenye bilioni 80s usd?
Na ina watu wengi zaidi, wasomi zaidi, mafuta zaidi, ma professional wa soccer, basketball zaidi, Nollywood, TV stations zaidi, musical stars zaidi...
 
Kumbe nchi yetu imezidiwa kiasi hiki na nchi yenye boko haram? Yaani kweli wao wanakaribia gdp ya bilioni 400 usd wakati sisi tupo kwenye bilioni 80s usd?
Ujasikitika kuona Wanaija ni 200M+ na WATz ni 60M+
 
Vipi USA aliyetawaliwa na Mwingereza na GPD ya Califonia tu ni kubwa kuliko Mwingereza?
Uko sawa asilimia 100% na mpaka sasa Wamarekani asilimia kubwa yao ni Waingereza.Kwa kuendelea kwa Marekani kuliko Uingereza usishangae maana kule Marekani walienda Waingereza wenye akili kutafuta maisha na walipokuta Marekani haina watu wakajimilikisha kila kitu.
 
Wewe na mtoa mada mna matatizo makubwa sana.

Uache kushangaa Kenya,Angola na Ethiopia kutuzidi uje kushangaa Nchi yenye Uchumi mkubwa Afrika kutuzidi?

On top of that Nigeria ndio inaongoza Afrika Kwa mafuta Sasa hapo kipi Cha kushangaza maana wanatuzidi Kwa Kila kitu kuanzia Utajiri wa rasilimali Hadi idadi ya watu na Ukubwa wa Nchi.

Nchi inayoongoza kwa rasilimali ni DRC Congo, ikifuatiwa na Tanzania. Jikite kwenye kijielimisha.
 
Uko sawa asilimia 100% na mpaka sasa Wamarekani asilimia kubwa yao ni Waingereza.Kwa kuendelea kwa Marekani kuliko Uingereza usishangae maana kule Marekani walienda Waingereza wenye akili kutafuta maisha na walipokuta Marekani haina watu wakajimilikisha kila kitu.

Mkuu Naona unahamisha ‘goal post’ Sasa[emoji3] Issue ilikuwa mmoja kamtawala mwenzie kwa hivyo mtawaliwa GPD lazima iwe chini kuliko aliyemtawala lakini kwa Marekani siyo hivyo.
 
Rwanda hata hawatuzidi chochote kuanzia miji,vijiji,ng'ombe,mbuzi,kondoo,kuku,mayai,maziwa,misitu,mbuga,bahari,maziwa,mito,vijito,milima,vilima,watu,elimu,uchumi,siasa,utamaduni,utalii,mapato,fedha,michezo,raha,utawala bora,maendeleo,barabara,magari,meli,ndege,akili na ustaarabu.
We jamaa daah
Hadi kuku 😁😁😁
 
Kinachokusikitisha ni nini? 60% ya Uchumi wao unategemea Mafuta na hao ndio Wanaongoza Kwa mafuta Afrika unategemea nini?

Unadhani wangekuwa wanategemea mahindi na migomba na Madini ya kubahatisha bahatisha Kwa idadi Ile ya watu wangekuaje?

Mwisho mlaumuni Baba yenu wa Taifa Kwa ujamaa wake wa miaka 25 ambao hakuna Cha maana ulisaidia as far as economy is concerned.
Acha ushamba viwanda vingi vilivyouzwa na kubadilishwa kuwa stoo na Wahuni alivijenga Mwalimu Nyerere.Sasa nyinyi mnaotusomea makaratasi yenu na PhD zenu za kubumba hizo mmefanya kipi?[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ni sawa na sasa mnamponda Magufuli alafu mnaemsifia anatekeleza miradi iliyoanzishwa na Magufuli!
Unapojadili Uchumi wenu wa Madawa ya kulevya, bidhaa feki za Uchina,mikopo yenu ya kitapeli uwe unamuweka Mwalimu Nyerere pembeni maana yule alikuwa na akili kuzidi hao matapeli wa Msoga!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Kila siku 'alaumiwe Nyerere kwa kuharibu uchumi na sera mbovu ya Ujamaa'. Haya nyinyi aliowaachia nchi mmefanya lipi la maana hadi sasa?

Ndo maana hata nchi zilizoendelea ninatunanga tuache kulia lia eti Ukoloni umetusababishia umasikini. Sasa mko huru na bado hamuendelei.
Huyo mwehu hana analojua.Ukitembea hii nchi viwanda vingi vilivyokufa alijenga Mwalimu Nyerere Tena akiwa na Watanzania ambao siyo wasomi kama sasa.Sasa saizi hakuna lolote ni uwizi na utapeli tu!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Hii ni moja ya thread ya vilaza nimewahi kusoma.

Sikujua humu JF kuna idadi kubwa hivi ya vijana wasio na akili kabisa na shule duni, sad wanajadili uchumi😂😂 naona ChoiceVariable yupo na wenzie humu.
Wewe jamaa ni 'mweupe kichwani'. Hapa sasa umechangia nini zaidi ya kujidhalilisha? Una tofauti gani na hao unaosema hawana akili?
 
Kinachokusikitisha ni nini? 60% ya Uchumi wao unategemea Mafuta na hao ndio Wanaongoza Kwa mafuta Afrika unategemea nini?

Unadhani wangekuwa wanategemea mahindi na migomba na Madini ya kubahatisha bahatisha Kwa idadi Ile ya watu wangekuaje?

Mwisho mlaumuni Baba yenu wa Taifa Kwa ujamaa wake wa miaka 25 ambao hakuna Cha maana ulisaidia as far as economy is concerned.

Miaka 25 ya Nyerere outperforms miaka 38 ya marais wengine? Make it make sense.
 
Wewe jamaa ni 'mweupe kichwani'. Hapa sasa umechangia nini zaidi ya kujidhalilisha? Una tofauti gani na hao unaosema hawana akili?
Yaani naogeleaje kwenye dimbwi la maji machafu!!?? 😂 😂 unafikiri kuwa na kichocho ni sifa?😂

Undeleeni kuogelea.
 
Back
Top Bottom