Huu ni mwendelezo wa ile tabia ya kugeuza godoro baada ya kulikojolea badala ya kulitoa nje.
Nyerere ameshafariki,bibi yenu anauza kila anachoona kinauzika.mnaendelea kumlaumu nyerere!!
Si ni mkapa aliyeanzisha ubinafsishaji,miaka 20 leo tuliishaamua kushika njia zetu(sio za nyerere).bado taifa liko ugokoni.
Watu tanajazwa ujinga na viongozi wanaoliibia taifa Kwa kumlaumu Nyerere.
Kama SIO Nyerere WATANZANIA wangekua maskini sana.
Uchumi Wa Tanzania unawasidia WATANZANIA wenyewe Tofauti na Afrika ya Kusini. Wazingu ndio walioshika uchumi Wa nchi Huku waafrika wakibaki kuwa watazamaji.
Kama SIO vita ya Uganda iliyopiganwa Kwa Muda Wa miaka miwili Tanzania ingekua nchi Tajiri kama India, Indonesia na Hata China na Urusi.
Leo hii kuna Amani lakini uchumi unachechemea. Leo hii pakitokea Vita miaka miwili kwanza viongozi wote watakimbilia Dubai ikiwemo Wapinzani.
Wataiba Mali za umma na kuacha nchi kwenye janga kubwa sana na Hata kuigawa nchi vipande vipande .
Nyerere alifanya KAZI kubwa sana hakuna mhuni Wa kulinganishwa na Nyerere.
Leo hii WATANZANIA wengi wanamiliki ardhi na nyumba Binafsi mpaka vijijini.
Vijiji vyote nchini viña shule ya serikali na angalau dispensary.
Nchi nyingi Afrika hazina huduma vijijini na Ardhi kubwa inamilikiwa na Wageni na matajiri . Maskini nchi nyingi hawana Ardhi .
Kuna watu wameamua kurejesha Ardhi Kwa Wakoloni Karne hii Kwa Sababu ya chuki dhidi ya Mwalimu Nyerere. Wanadhani wanamkomoa Nyerere kumbe wanawapeleka watanzania kwenye utumwa.
Unamuuziaje mgeni Ardhi Karne Hii yenye wasomi na vyuo Vya kilimo na asilimia 80 ya watu ni wakulima na wafugaji?
Hao wauzaji Wana Nia njema kweli na vizazi vya WATANZANIA walio wengi au wanaangalia familia Zao na marafiki Zao huko nje Ili wajijengee MAISHA ya starehe?