Nimesikitika baada ya kuona Nigeria ina GDP karibu mara tano ya Tanzania

Nimesikitika baada ya kuona Nigeria ina GDP karibu mara tano ya Tanzania

Mkuu ulinganishi wa Nigeria yenye population ya 213 milll na Tanzania 63 mill..automatically GDP yao itakuwa kubwa .mahitaji na uzalishaji wao ni mkubwa kwa hiyo pupolutaion...halafu mambo ya wazungu kutuletea GDP kama kipimo cha uchumi imepitwa na wakati maana haileflect maisha halisi ..
GDP is overrated ni mfumo wa kibeberu kuficha umaskini tu.

Tajiri mmoja anazalisha T 10 halafu vijakazi wake mia mbili wanazalisha 1000 na wote wanawekwa kapu la uchumi unakuwa kwa GDP.
 
Kwa Sasa Tanzania hatuna independent thinkers. Kila mtu anasubiria huruma ya Rais. Na pia kila mmoja anafanya Jambo kumfurahisha Rais.
Huwezi pata Independent thinkers kama nchi imejaa machawa
 
Mkuu ulinganishi wa Nigeria yenye population ya 213 milll na Tanzania 63 mill..automatically GDP yao itakuwa kubwa .mahitaji na uzalishaji wao ni mkubwa kwa hiyo pupolutaion...halafu mambo ya wazungu kutuletea GDP kama kipimo cha uchumi imepitwa na wakati maana haileflect maisha halisi ..
Watu hawalielewi hilo, ndo maana huwa nawashangaa wanaolinganisha US na China
 
Hii imenikumbusha baadhi ya colleagues wangu ambao ni Wahindi kutoka India kabisa na wengine ni wenye asili ya Kihindi lakini waliozaliwa nchi za magharibi.

Nigeria, Egypt, na Afrika Kusini, licha ya kuwa ndo nchi zenye uchumi mkubwa barani Afrika, lakini ikija kwenye GDP per capita, zimeachwa mbali na vinchi vidogo kama Seychelles, Equatorial Guinea, Gabon, na Mauritius!
Swali langu hapa litakuwa simple, kipi kinatangulia kuwa na gdp kubwa au per capita kubwa?

Mimi nadhani shughuli yoyote kubwa katika nchi inayofanya kuwepo kwa gdp kubwa automatically kutapelekea ukuaji wa per capita.

Kwa case ya Nigeria na Tanzania, still per capita ya Nigeria ipo juu ya Tanzania katika ratio ya 1.9:1.3
 
Kila siku 'alaumiwe Nyerere kwa kuharibu uchumi na sera mbovu ya Ujamaa'. Haya nyinyi aliowaachia nchi mmefanya lipi la maana hadi sasa?

Ndo maana hata nchi zilizoendelea ninatunanga tuache kulia lia eti Ukoloni umetusababishia umasikini. Sasa mko huru na bado hamuendelei.
Nyerere ndo sababu ya Tanzania ilivyo.
Yeye ndo kasababisha umasikini, ujinga
 
Kumbe nchi yetu imezidiwa kiasi hiki na nchi yenye boko haram? Yaani kweli wao wanakaribia gdp ya bilioni 400 usd wakati sisi tupo kwenye bilioni 80s usd?
Nenda kwenye source yako kaangalie nigeria ina popolulation ya watu wangap na ukubwa gan ukilinganisha na TZ then urudi hapa
 
Uchumi unabebwa na GDP ndio SI unit yake.

GDP has nothing to do with Population
How are you going to measure economic productivity of your workforce with pure GDP?

Also, GDP is an outdated measure, plagued with many problems, here are some.

Nenda kwenye source yako kaangalie nigeria ina popolulation ya watu wangap na ukubwa gan ukilinganisha na TZ then urudi hapa
Huyu jamaa unaweza kuweka meza A yenye sahani ya ugali wa kilo moja na watu 100 wanaogawana ugali huo, halafu sahani B yenye ugali wa robo kilo na mtu mmoja anakula peke yake, akaangalia ukubwa wa ugali wa meza A, akajiunga huko meza A awe mtu wa 101 kugawana ugali huo, kwa sababu ni ugali mkubwa zaidi tu.

Akamuacha yule mtu mmoja wa meza B ambaye anakula ugalinw arobo kilo peke yake.

Kwa sababu ugali wa robo kilo ni mdogo kuliko ugali wa kilo moja, bila kujali namba ya watu wanaogawana ugali huo.
 
Nigeria wana Mafuta sawa na Kuwaiti
Tanzania pia tuna mafuta na gesi .
Tatizo ni siasa na kujikomba Kwa mataifa ya magharibi na mawakala Wao Wa Falme Za kiarabu.
Mwalimu alikua anaagiza mafuta ghafi . Yalikua yanachujwa pale kigamboni tunapata product nyingine pia.
Waliingia Wahuni wakawa na tamaa ya biashara ya mafuta na kuagiza Ili waiteze wanavyotaka . Hawa ndio wanaodhibiti zoezi Zima la kuchimba mafuta Tanzania.
Hata Uganda kama SIO msimamo Wa Mwafrika Mzalendo halisi Yoweri Kaguta Museveni mafuta yasingechimbwa Uganda.
 
Kumbe nchi yetu imezidiwa kiasi hiki na nchi yenye boko haram? Yaani kweli wao wanakaribia gdp ya bilioni 400 usd wakati sisi tupo kwenye bilioni 80s usd?
Kama takwimu zako ni sahihi basi tupo vizuri sana kuliko Nigeria. Wao wapo watu zaidi ya million 220 sisi tupo million 62.

Na utajiri wa mafuta walionao kwa miaka mingi sasa, tupo vizuri zaidi yao.
 
Mkuu ulinganishi wa Nigeria yenye population ya 213 milll na Tanzania 63 mill..automatically GDP yao itakuwa kubwa .mahitaji na uzalishaji wao ni mkubwa kwa hiyo pupolutaion...halafu mambo ya wazungu kutuletea GDP kama kipimo cha uchumi imepitwa na wakati maana haileflect maisha halisi ..
Vipi kuhusu population ya UK ambayo inakaribiana na TZ lakini wana uchumi mara 30 ya TZ, au uchumi wa South Africa mara nane ya Tanzania lakini wana population ndogo kuliko ya Tanzania, Jamani mnatakiwa kuwe na ufikiri sahihi.
 
Mkuu seriously unalinganisha uchumi wa UK, nchi iliyotawala na kunyonya dunia nzima kwa mamia ya miaka, na Tanzania?
 
Singapore GDP=466bln Usd
GDP per capita=127,564 Usd
Population = 5.9-6 mln

Data by WorldBank 2022
Tanzania GDP= 87 Bln USD
GDP per capita= 1320 USD
Population = 62 Mln.

Watu bado wamejazwa ujinga na CCM. Kila kitu kinapelekwa kisiasa hadi michezo, jana timu yenu ya jumuiya wa wazazi jana ilifungwa nyumbani kwenu na Morocco, acheni kugawanywa na ondoeni uchawa.
 
Mkuu seriously unalinganisha uchumi wa UK, nchi iliyotawala na kunyonya dunia nzima kwa mamia ya miaka, na Tanzania?
Si kuna mtu amesema ukiwa na population kubwa unakuwa na GDP kubwa? Vipi kuhusu Singapore, vipi kuhusu Luxembourg, vipi kuhusu South AFRICA, au Algeria, haya kuhusu Egypt au hawa nao waliwaibia. Talk about substance, siyo mnaongea pumba.
 
Back
Top Bottom