Nimesikitika baada ya kuona Nigeria ina GDP karibu mara tano ya Tanzania

Nimesikitika baada ya kuona Nigeria ina GDP karibu mara tano ya Tanzania

Nigeria imetuzidi vyote
Kwenye GDP unalinganisha visivyolinganishika.

Timu ina wachezaji zaidi ya 215 milioni unaishindanisha na timu ina wachezaji hawajafika hata 65 milioni.

Yani Tanzania tukiifanya idadi yetu iwe mara tatu ya sasa, bado hatujaifikia idadi ya watu ya Nigeria kwa sasa.

Sasa hapo unalinganishaje GDP?

Toa hii hoja ya GDP kwanza tuangalie mengine kama unataka a fair comparison.
 
Acha upuuzi wako,hivyo vimapambo utalinganisha na mafuta? Umewahi sikia uchumi wa Dunia ukayumba Kwa sababu ya kukosa Tanzanite?

Kwenye top 15 ya gas Tanzania haipo

Kama Tanzania Kuna Almasi Botswana,Angola na South Africa watasemaje?

Kwa taarifa Yako tuu kati ya vyote ulivyotaja hapo Nigeria hawana Makaa ya Mawe tuu ambayo ni useless Duniani.

Tanzania inajitahidi kwenye dhababu tuu lakini Dhahabu sio hitaji la lazima kwenye uchumi wa Dunia kulinganisha na mafuta na hiyo Dhahabu ipo karibu Kila Nchi.
Rwanda wana mafuta?
 
Kwenye GDP unalinganisha visivyolinganishika.

Timu ina wachezaji zaidi ya 215 milioni unaishindanisha na timu ina wachezaji hawajafika hata 65 milioni.

Yani Tanzania tukiifanya idadi yetu iwe mara tatu ya sasa, bado hatujaifikia idadi ya watu ya Nigeria kwa sasa.

Sasa hapo unalinganishaje GDP?

Toa hii hoja ya GDP kwanza tuangalie mengine kama unataka a fair comparison.
Hivi unajua sisi tunaizidi Kenya kwa uwingi wa watu?
Shida nchi yetu ni uongozi,ifike mahali tufanye free and fair election,yawezekyawezekana tumapata viongozi bora,kuliko sasa hivi tunapopata viongozi mchanganyiko,yaani wazuri na wabaya,kwa maelekezo.
 
Kwenye GDP unalinganisha visivyolinganishika.

Timu ina wachezaji zaidi ya 215 milioni unaishindanisha na timu ina wachezaji hawajafika hata 65 milioni.

Yani Tanzania tukiifanya idadi yetu iwe mara tatu ya sasa, bado hatujaifikia idadi ya watu ya Nigeria kwa sasa.

Sasa hapo unalinganishaje GDP?

Toa hii hoja ya GDP kwanza tuangalie mengine kama unataka a fair comparison.
Uchumi unabebwa na GDP ndio SI unit yake.

GDP has nothing to do with Population
 
Kumbe nchi yetu imezidiwa kiasi hiki na nchi yenye boko haram? Yaani kweli wao wanakaribia gdp ya bilioni 400 usd wakati sisi tupo kwenye bilioni 80s usd?
Tanzania ni kubwa kuliko Nigeria kwa tofauti ya kama kilometer za mraba 23,000 ila population yake ni karibu 224 milion. Watu na raslimali zinazosimamiwa vizuri ndo factors kubwa na za msingi katika kukuza uchumi.
Hii nchi ya chief Hangaya ina safari ndefu sana.
 
Hivi unajua sisi tunaizidi Kenya kwa uwingi wa watu?
Shida nchi yetu ni uongozi,ifike mahali tufanye free and fair election,yawezekyawezekana tumapata viongozi bora,kuliko sasa hivi tunapopata viongozi mchanganyiko,yaani wazuri na wabaya,kwa maelekezo.
Shida yetu ni zaidi ya uongozi, tuache kulaumu uongozi tu.

Nakubaliana nawe. Naelewa "Noblesse Oblige". Waliopewa talanta nyingi zaidi watadaiwa marejesho mengi zaidi, hata mwanafalsafa Yesu alituambia hili katika mfano wake.

Uongozi una lawama kubwa kabisa na za awali kabisa. Hilo halina ubishi. Lakini, uongozi haujiweki wenyewe. Watu wanaoongozwa pia wana sehemu ya lawama kwa kujiruhusu kuwa na uongozi huu. People get the leadership they deserve. Else they remove that leadership and put one that they deserve.

Kwa kila rais mmoja anayeiba kura, kuna maelfu na maelfu ya wasimamizi wa uchaguzi mpaka majaji walio katika tume ya uchaguzi wanaoshiriki wizi huu.

Kuna wananchi mamilioni wanaoona wanaibiwa kura lakini wanakubali kikondoo na kusema hewala hewala tu.

Kuhusu wingi wa watu;

Wingi wa watu kama hujajipanga kuwatumia hao watu kuzalisha ni tatizo.

Kwa maana utakuwa na watu wengi wa kuwalisha na kuwahudumia wakati hawazalishi.

Bongo watu wanamaliza chuo na kukaa miaka mitano mpaka kumi wanatafuta kazi. Yani hapo hata mtu akipata kazi, usomi ushapotea anabaki kuwa Mmachinga tu.

Sasa hapo wingi wa watu utasaidia nini?

Pia, kusema Tanzania tunawazidi Kenya kwa wingi wa watu , obviously Tanzania ni nchi kubwa, so kuongelea wingi wa watu tu unarudi kule kule kwenye kuongelea GDP.

What is the population density? What about arable land? How many people are employed? How many are in disguised unemployment? How many are productive (population minus children, the eledery, the infirm)

Unaweza kuwa na nchi ina watu wachache, lakini ina wazalishaji wengi na watoto/wazee/wagonjwa wachache, na unaweza kuwa na nchi ina watu wengi, lakini wqzalishaji wachache, wengi ni watoto/wazee/ wagonjwa.

So, wingi wa watu tu hautuoneshi kitu specifically hata kama unaweza kuwa indicator in similar countries under ceteris paribus.
 
Sasa kama ni hivyo aliyelinganisha Tanzania na Nigeria alitumia vigezo gani?
GDP ni pato la taifa. Pato zima la taifa ni matokeo ya kodi, mikopo, grants utalii na kila kitu. Hii haitegemei sana population bali uwekezaji katika nchi husika. Ndio maana Israel inatuzidi GDP licha ya kuwazidi population.
Mikopo na grants zipo kwenye gdp!?
 
Uchumi unabebwa na GDP ndio SI unit yake.

GDP has nothing to do with Population
Kuupima uchumi kwa GDP tu kunaweza kukufanya uione nchi masikini yenye watu wengi wanaoishi kwa uchumi wa dola 2 za Kimarekani kwa siku (Nigeria, GDP 440.8 billion USD, 2021) kuwa ni tajiri kuliko nchi kama Mauritius yenye GDP ya 11.53 billion USD.

By GDP, Nigeria's economy is 38.2 times larger than that of Mauritius.

GDP per capita ya Nigeria ni takriban $ 2066

GDP per capita ya Mauritius ni $9,106.

Kipato cha wastani cha mtu wa Mauritius ni mara 4.4 zaidi ya kipato cha wastani cha mwananchi wa Nigeria.

Seychelles ina GDP ndogo sana. Only 1.454 billion USD.

By GDP Nigeria ina uchumi mkubwa mara 303 ya uchumi wa Seychelles.

Ila, Seychelles ina watu wachache pia, hivyo ina GDP per capita ya $14,653.

Nigeria ina watu wasiopungua milioni 215.

Seychelles ina watu 99,258. Idadi ya watu wote wa Seychelles ni kama mtaa mmoja tu hapo Lagos.

Kwa kila mtu mmoja wa Seychelles, kuna Wa Nigeria 2166.

Sasa hapo unawezaje kupima uchumi wa nchi kwa kuangalia GDP tu bila hata kuangalia per capita income?

Mwananchi mmoja wa Seychelles kwa watani ana kipato mara 7 ya kipato cha mwananchi wa Nigeria.

Tunarudi kule kule.

Unaangalia ukubwa wa ugali bila kuangalia wingi wa watu wanaokula huo ugali na kujua kila mtu atapata matonge mangapi.

Ukiona ugali mkubwa, unafurahi tu, ugali mkubwa.

Kumbe, walio na ugali mdogo wanaweza kushiba zaidi, kwa sababu wako wachache sana na ukigawanya matonge, kwa wastani, kila mmoja atapata matonge mengi kuliko wale wenye ugali mkubwa.
 
Kanuni muhimu ya kulinganisha ni kulinganisha vinavyolinganishika.

Yani, linganisha machungwa na machungwa, matufaa na matufaa.

Usilinganishe machungwa na matufaa.

GDP ni hesabu inayoweza kukupotosha.

Kwa sababu, haiangalii mgawanyo wa watu.

Ni hivi, ukiwa na nyumba A yenye watu 10, na kipato cha shilingi milioni 10, halafu ukawa na nyumba B ya mtu mmoja, mwenye kipato cha shilingi milioni tano, utasema hiyo nyumba A yenye watu kumi na kipato cha shilingi milioni 10 imeizidi uchumi nyumba yenye mtu mmoja na kipato cha shilingi milioni tano?

Huoni kwamba ukifanya hesabu hapo ukagawanya utapata nyumba A kwa wastani kila mtu ana kipato cha shilingi milioni moja, wakati nyumba B mtu mmoja ana kipato cha wastani cha shilingi milioni tano?

Ni bora uongelee GDP per capita, ambayo inachukua GDP na kuigawanya kwa idadi ya watu, ukapata kila mtu ana GDP per capita gani.

Nigeria ina watu zaidi ya milioni 215, Tanzania haijafikisha hata watu milioni 65. Maana yake unaweza kuzijumlisha Tanzania tatu kwa idadi ya watu, na bado usiifikie idadi ya watu wa Nigeria.

Unaweza kujumlisha idadi za watu wa Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia na Sudani ya Kusini, na bado usiifikie idadi ya watu ya Nigeria.

Sasa hapo unaona kuzilinganisha nchi mbili hizi kwa GDP tu ni sawa?
Hata ukitumia per capita bado wametuzidi kwa ratio ya 1.9:1.3 kwahiyo kwa hapa bado tumezidiwa.
 
Wewe na mtoa mada mna matatizo makubwa sana.

Uache kushangaa Kenya,Angola na Ethiopia kutuzidi uje kushangaa Nchi yenye Uchumi mkubwa Afrika kutuzidi?

On top of that Nigeria ndio inaongoza Afrika Kwa mafuta Sasa hapo kipi Cha kushangaza maana wanatuzidi Kwa Kila kitu kuanzia Utajiri wa rasilimali Hadi idadi ya watu na Ukubwa wa Nchi.
Utajiri wa kweli sio rasilimali bali ni akili. Uingereza haina rasilimali yoyote lakini ilitawala dunia. Leo hii pale Israel kuna rasilimali gani?

Kule Bahamas wanategemea fukwe ambazo ni kilomita chache sana ukifananisha na tulizo nazo na wanaingiza mapato mara tano zaidi yetu.
 
Kumbe nchi yetu imezidiwa kiasi hiki na ie GDP itu vinavo fanya uchumesmnchi yenye boko haram? Yaani kweli wao wanakaribia gdp ya bilioni 400 usd wakati sisi tupo kwenye bilioni 80s usd?
Umesoma uchumi buda GDP ya nchi ukijua iloubwa sana kaaa t kfautou na nigeria yettokana na mamb meng kwaiyo atuwez kufanana kwanza population fulani inakua ku
Thamani ya pesa isitoe taswira ya hali ya uchumi.

Hao nigeria wenyewe hela yao inazidiwa thamani na hiyo kwacha,haya pima uchumi sasa
 
Kumbe nchi yetu imezidiwa kiasi hiki na nchi yenye boko haram? Yaani kweli wao wanakaribia gdp ya bilioni 400 usd wakati sisi tupo kwenye bilioni 80s usd?
GDP haipimwi hivyo, obvious ukiwa na wananchi 200m plus huwezi kuwa na GDP kuliko nchi yanye watu million 60 kama Tanzania!!. Huwa tunachukua GDP tunagawa na population ya wananchi ukifanya hivyo Nigeria inakua almost USD 2000 na Tanzania ni USD 1000. So wametuacha nusu tu.

Ni vizuri takwimu ziwekwe sawa tuache exaggerations.
 
Hata ukitumia per capita bado wametuzidi kwa ratio ya 1.9:1.3 kwahiyo kwa hapa bado tumezidiwa.
Hii ya per capita ndiyo point ya kuongea, si pure GDP.

Ila per capita nayo ina matatizo yake nimeyataja hapo juu, mabilionea wachache wanaweza kupandisha per capita GDP ya watu wengi.

Aliko Dangote peke yake anapandisha per capita GDP ya wa Nigeria karibu 4.9 million kutoka $0 mpaka %2066. Na kuna mabilionea watatu last time I checked, ma millionaire ndiyo kibao.

So, tunacheza pale pale.

Nchi yenye watu wengi ina uchumi mkubwa unaoleta mabilionea wachache wanaoinua per capita ya masikini wengi waoneoane wana afadhali on paper, wakati kiuhalisia uchumi wa kila siku wa hao watu ni mbaya sana.

So.

1. Pure GDP ni indicator mbaya kwa sababu haioneshi mgawanyo per capita.

2. GDP per capita ni indicator yenye afadhali kuliko pure GDP, kwa sababu inaonesha mgawanyo wa GDP kwa kila mtu (hence per capita) lakini bado ni distorted figure, mabilionea na mamilionea wachache wa USD wanawanyanyua mamilioni ya watu masikini kabisa na kuwafanya waonekane wanaishi maisha ya afadhali.

Unaweza kuwa na nchi yenye GDP per capita nzuri, halafu ikawa na high inequality, hii haioneshi uchumi mzuri.

Matatizo mengine mengi ya GDP yameelezwa hapa.

 
Back
Top Bottom