Hii imenikumbusha baadhi ya colleagues wangu ambao ni Wahindi kutoka India kabisa na wengine ni wenye asili ya Kihindi lakini waliozaliwa nchi za magharibi.
Miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakitamba sana kuwa India sasa ipo tano bora ya nchi zenye uchumi mkubwa duniani [trillion dollar economies].
Wanajivunia sana kuwa sasa wana uchumi mkubwa kuliko hata Uingereza, taifa lililowatawala.
Lakini kama ulivyosema, hesabu ya GDP ukiiangalia kwa juu juu, inaweza kukupotosha sana.
Ndiyo, India ina GDP kubwa kushinda nchi nyingi tu za Ulaya magharibi.
India ina GDP kubwa kuzishinda Canada, Australia, na New Zealand.
Lakini licha ya kwamba India ina GDP kubwa kuzishinda hizo nchi, ikija kwenye GDP per capita, hiyo nchi haipishani sana na nchi za Kiafrika.
Viwango na ubora wa maisha kwenye nchi za Scandinavia ni vya juu sana kushinda India. Wastani wa kipato cha mtu mmoja mmoja nao ni mkubwa mno kiasi kwamba huwezi kabisa hata kujaribu kulinganisha.
Ukubwa wa GDP si wa kuuangalia tu na kuishia juu juu na kutoa hitimisho.
GDP ya nchi inaweza ikawa kubwa lakini watu wake wengi sana wakawa bado ni mafukara.
Nigeria, Egypt, na Afrika Kusini, licha ya kuwa ndo nchi zenye uchumi mkubwa barani Afrika, lakini ikija kwenye GDP per capita, zimeachwa mbali na vinchi vidogo kama Seychelles, Equatorial Guinea, Gabon, na Mauritius!