Kumbe nchi yetu imezidiwa kiasi hiki na nchi yenye boko haram? Yaani kweli wao wanakaribia gdp ya bilioni 400 usd wakati sisi tupo kwenye bilioni 80s usd?
Kanuni muhimu ya kulinganisha ni kulinganisha vinavyolinganishika.
Yani, linganisha machungwa na machungwa, matufaa na matufaa.
Usilinganishe machungwa na matufaa.
GDP ni hesabu inayoweza kukupotosha.
Kwa sababu, haiangalii mgawanyo wa watu.
Ni hivi, ukiwa na nyumba A yenye watu 10, na kipato cha shilingi milioni 10, halafu ukawa na nyumba B ya mtu mmoja, mwenye kipato cha shilingi milioni tano, utasema hiyo nyumba A yenye watu kumi na kipato cha shilingi milioni 10 imeizidi uchumi nyumba yenye mtu mmoja na kipato cha shilingi milioni tano?
Huoni kwamba ukifanya hesabu hapo ukagawanya utapata nyumba A kwa wastani kila mtu ana kipato cha shilingi milioni moja, wakati nyumba B mtu mmoja ana kipato cha wastani cha shilingi milioni tano?
Ni bora uongelee GDP per capita, ambayo inachukua GDP na kuigawanya kwa idadi ya watu, ukapata kila mtu ana GDP per capita gani.
Nigeria ina watu zaidi ya milioni 215, Tanzania haijafikisha hata watu milioni 65. Maana yake unaweza kuzijumlisha Tanzania tatu kwa idadi ya watu, na bado usiifikie idadi ya watu wa Nigeria.
Unaweza kujumlisha idadi za watu wa Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia na Sudani ya Kusini, na bado usiifikie idadi ya watu ya Nigeria.
Sasa hapo unaona kuzilinganisha nchi mbili hizi kwa GDP tu ni sawa?