Nimetafuta kwenye Quran hakuna sehemu Mungu amesema waislamu muoane

Uwesutanzania

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2019
Posts
1,380
Reaction score
1,686
Ni mimi wako UWESUTANZANIA ✍️

Sipo hapa kwa kubeza wala kukejeli nataka kupewa elimu kutoka kwa muislamu aliyesoma Quran tukufu ambayo ndio muongozo wa muislamu na usinilete hadithi kutoka muslim na tilmizu eti alimsikia mtume akisema hapana.

Nataka kwa mwenye andiko kutoka kwenye kitabu (Qur-an
  • wapi Mungu kasema tuoane
  • wapi Mungu kasema uoe wanawake wanne
  • wapi Mungu kasema ukioa mkigombana umpe taraka na watoto.
  • wapi Mungu kasema ukimkumbuka uende kwao ukamlejee.

Asanteni.
 
Sawa ni kweli yote hayo waislamu wanaruhusu kuoa hata wasio waislamu wakuristo, na wanaruhisiwa kuoa mke moja mpaka kuepo na sababu tena, ........ kwahilo sioni ligi unao tafuta ya nini tena kuoa mke wa pili watatu sio lazima na kuoa muislamu sio lazima, sasa unacho tafuta ni nini mkuu?
 
Wanaruhusiwa na nani?
 
24:32
Na waozeni wajane miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri Mwenyezi Mungu atawatajirisha kwa fadhila yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa Mwenye kujua. surah an nur aya 32
 
Mi na sikia kilishushwa kama kimondo
 
وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي الْيَتَامَىٰ فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَلَّا تَعُولُوا ﴿٣﴾

3. Na mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu kwa mayatima, basi oeni waliokupendezeni katika wanawake (wengine); wawili au watatu au wanne. Lakini mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi mmoja tu au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki.[2] Hivyo ni karibu zaidi kwamba hamtoelemea kudhulumu.[3]
 
😂
 
Hizo Hoja zako zinajibiwa na mtoto wa miaka 7 wa madrasa,yani kuanzia Leo kaa ukijua kuwa ukimuuliza Muislam swali lolote basi kuna Ayah zinakuja kichwani si Chini ya 10 kwa haraka,haihitaji kusoma Quran kuzitafuta zipo kichwani miaka mingi zimehifadhiwa.
 
Al baqarah 2: 226, 227,228,229,230

Kwa wanao apa kuwa watajitenga na wake zao, wangojee miezi mine. Wakirejea basi Mwenyezi Mungu hakika ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu. aya ya 226

Na wakiazimia kuwapa talaka basi, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mjuzi. aya 227

Na wanawake walio achwa wangoje peke yao mpaka t'ahara (au hedhi) tatu zipite. Wala haiwajuzii kuficha alicho umba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao, ikiwa wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na waume wao wana haki ya kuwarejesha katika muda huo, kama wakitaka kufanya sulhu. Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu yao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima. aya 228

T'alaka ni mara mbili. Kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa vizuri. Wala si halali kwenu kuchukua chochote mlicho wapa wake zenu, ila ikiwa wote wawili wakiogopa ya kwamba hawataweza kushikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu. Basi mkiogopa kuwa hawataweza kushikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu hapo itakuwa hapana lawama ikiwa mwanamke atajikomboa. Hii ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu; basi msiikiuke. Na watakao ikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, hao ndio madhaalimu. 229

Na kama amempa t'alaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hayo mpaka aolewe na mume mwengine. Na akiachwa basi hapana ubaya kwao kurejeana wakiona kuwa watashikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na hii ni mipaka ya Mwenyezi Mungu anayo ibainisha kwa watu wanao jua. 230
 
wapi Mungu kasema ukioa mkigombana umpe taraka na watoto.


يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحْصُوا الْعِدَّةَ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ رَبَّكُمْ ۖ لَا تُخْرِجُوهُنَّ مِن بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخْرُجْنَ إِلَّا أَن يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ ۚ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّـهِ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ ۚ لَا تَدْرِي لَعَلَّ اللَّـهَ يُحْدِثُ بَعْدَ ذَٰلِكَ أَمْرًا﴿١﴾

1. Ee Nabiy! Mtakapowataliki wanawake, basi watalikini katika wakati wa eda (twahaarah) zao, na hesabuni barabara eda, na mcheni Allaah Rabb wenu. Msiwatowe katika nyumba zao, na wala wao wasitoke isipokuwa wakileta uchafu ulio bayana. Na hiyo ndio Mipaka ya Allaah. Na yeyote atakayevuka Mipaka ya Allaah, basi kwa yakini amedhulumu nafsi yake. Hujui; huenda Allaah Atatokezesha jambo jingine baada ya haya.[1]

وَالْوَالِدَاتُ يُرْضِعْنَ أَوْلَادَهُنَّ حَوْلَيْنِ كَامِلَيْنِ ۖ لِمَنْ أَرَادَ أَن يُتِمَّ الرَّضَاعَةَ ۚ وَعَلَى الْمَوْلُودِ لَهُ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ لَا تُكَلَّفُ نَفْسٌ إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَا تُضَارَّ وَالِدَةٌ بِوَلَدِهَا وَلَا مَوْلُودٌ لَّهُ بِوَلَدِهِ ۚ وَعَلَى الْوَارِثِ مِثْلُ ذَٰلِكَ ۗ فَإِنْ أَرَادَا فِصَالًا عَن تَرَاضٍ مِّنْهُمَا وَتَشَاوُرٍ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا ۗ وَإِنْ أَرَدتُّمْ أَن تَسْتَرْضِعُوا أَوْلَادَكُمْ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِذَا سَلَّمْتُم مَّا آتَيْتُم بِالْمَعْرُوفِ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٣٣﴾

233. Na wazazi wa kike wanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili, kwa mwenye kutaka kutimiza kunyonyesha. Na ni juu ya mzazi wa kiume kuwapatia chakula chao na nguo kwa mujibu wa ada. Hailazimishwi nafsi ila kwa iliwezalo. Asidhuriwe mzazi wa kike kwa ajili ya mwanawe, na wala mzazi wa kiume kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi (wa baba) mfano wa hivyo. Watakapotaka kumwachisha kunyonya kwa maridhiano baina yao wawili na mashauriano, basi hapana dhambi juu ya wawili hao. Na mtakapotaka kutafuta wa kuwayonyesha watoto wenu, basi si dhambi kwenu ikiwa mtalipa mlichoahidi kwa mujibu wa sharia. Na mcheni Allaah na jueni kwamba hakika Allaah Ni Mwenye Kuona yale myatendayo.
 

A. KUOANA /NDOA

1. Surah Ar-Rum (30:21)
2. Surah An-Nisa (4:1)
3. Surah Al-Baqarah (2:221)
4. Surah An-Nur (24:32)
5. Surah Al-Ma'idah (5:5)
6. Surah An-Nisa (4:19)
7. Surah Al-Baqarah (2:228)
8. Surah An-Nisa (4:34)
9. Surah Al-Baqarah (2:187)
10. Surah Al-Baqarah (2:231)
11. Surah At-Talaq (65:2-3)

B. KUOA WANAWAKE WANNE

1. Surah An-Nisa (4:3)

C. TALAKA

1. Surah Al-Baqarah (2:226-232)
2. Surah Al-Baqarah (2:236-237)
3. Surah Al-Baqarah (2:241-242)
4. Surah An-Nisa (4:19-21)
5. Surah An-Nisa (4:127-130)
6. Surah At-Talaq (65:1-7)

D. KUMREJEA MTALAKA

1. Surah Al-Baqarah (2:228)
2. Surah Al-Baqarah (2:229)


Unaweza kupitia hizo verses zipo very direct haihitaji maelezo meeengi
 
Mumeleta maandiko marefu sana bila kuweka andiko wapi Mungu anampa muislam amri ya kuoa!.

Nilipenda kuona hiyo amri, vigezo na masharti ya kuoa. Lakini maandiko yenu yote yame skip hitaji langu mama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…