Nimetazama interview ya hawa wanafunzi wa Kitanzania nchini Iran nikaelewa jambo

Nimetazama interview ya hawa wanafunzi wa Kitanzania nchini Iran nikaelewa jambo

Tanganian naingia mkono hoja yako ya demokrasia ni utapeli mkubwa , tazama waliokuletea demokrasia mfano marekani , uingereza , ujermani ,ufaransa Wana vyama vinganpi vya siasa , muundo wa serikali zao, halafu hesabu vyama vya siasa vya Tnchi yako , au idadi ya vyama pale DRC utagundua kua demokrasi iliyokuja afrika ilitengenezwa ili serikali za magharibi ziweze kupata vibaraka kupitia vyama vya siasa na kucontrol rasilimali zote na kufanya wizi wa mchana kweupe
Watanzania hwataki maisha mazuri wanataka demokrasia 🤣🤣..Hii inatokana na elimu wanayopewa tangu shule ya awali ,hivi mtu akilelea nchi kama kiongozi mpaka mkapata maendeleo kuna ulazimisha gani kuitishi uchaguzi na kutumia karibu bil 900 ambazo ni trilion kasoro ..Baadaye mnaanza kuhudumia vyama vya siasa kwa kuwapa ruzuku ili waendele kupiga kelele kurubuni watu ili wawachague ..

Mfano Lissu anakuwaje popular wakati ni mwanasiasa na msomi butu ambaye hajagundua chochote cha kurahisisha maisha ya mtanzania zaidi ya kukariri vifungu vya sheria ..Wasomi walete tija sio kukimbilia mambo ambayo haywezi kurahisisha maisha ya mtu mmoja mmoja.
 
Wanadai maisha ya Iran ni cheap sana, ukiondoka na 1 milion TZS unaishi mwaka mzima bila shida kabisa.
Wanasema 2500 ni sawa na pesa za Iran rial 100 ambapo lita moja ya mafuta ya gari ni rial 3. hivyo yani kwa 2500 za kibongo karibu unapata rita 33 za mafuta.
Wanasema iran wana mitandao yao wenyewe hivyo kutumia mitandao ya nje ni mara chache.
Wanasema hata usafiri wa umma ni bei nafuu sana kwenda na kurudi kutoka kazini ni chini ya buku.
Pia wanasema hata na vikwazo vyote walivyowekewa, wairan wamejiandaa kukabiliana navyo na maisha yao yako sawa tu.
Hizi ni propaganda za wasioishi Iran ila waliofika ni vinginevyo.
Nimeona na black amerca fulan ni traveller ana YT channel yake, alikuwa Iran anaonyesha maiisha yao yalikuwa poa tu. Wana hadi subways, ila mtanzania asiye na vikwazo baada ya miaka 60 ya uhuru anaicheka iran akisema ina hali mbaya.

View: https://www.youtube.com/watch?v=EcBr430km-I

WAHAMIE HUKOOO SASA KWA MAKOBASI
 
Utajiri wa Ayatollah Khomeini kupitia Execution of Imam Khomeini's Order (EIKO)/Setad unakadiriwa kuwa ni $billion 95.
Acha uongo wewe , Ayatollah mpaka nyumba yake inajilikana iliyopo .Yule Rais aliyekufa tu alikuwa anaishi maisha ya kawaida .

Acha propaganda jamaa anaishi maisha ya kawaida ...
 
Acha uongo wewe , Ayatollah mpaka nyumba yake inajilikana iliyopo .Yule Rais aliyekufa tu alikuwa anaishi maisha ya kawaida .

Acha propaganda jamaa anaishi maisha ya kawaida ...
Soma kuhusu Execution of Imam Khomeini's Order (EIKO)/Setad.
 
Hapa bongo ungependa familia ya nani iwe Sultan?
Usultani hauwi kwa kusema tu mkuu.
Familiaa yoyote itakayokidhi vigezo vya Usultani hata kama yako chief.
 
SHEIKH AELEZEA ALIVYOKIMBIA KIMBIA KATIKA NCHI KADHAA ZA MASHARIKI YA KATI HADI KUTUA NCHI YA IRAN 1978

Sheikh Abdallah Seif anaelezea ugumu wa kukubalika hata kama umesoma sana mabuku ya imani kwa sisi waMatumbi

TOKA MAKTABA : Safari ya kutafuta elimu ya imani na uongozi


(NZIMA)-SIMULIZI YA MAREHEMU SHEIKH ABDALLAH SEIF (1939 -2020) - HISTORIA YETU part 1



KIU YA ILMU, SHEIKH ABDALLAH SEIF ILIMPELEKEA KUSOMA KWA MIAKA 11 MFULILIZO KATIKA NCHI ZA IRAQ, LEBANON NA IRAN (1968-1979)

Sheikh Abdallah Seif Linganaweka anatujuza kuwa Wenyeji wa Lindi jina Lao la asili ni Wakudewe kwa sasa almaaruf wanafahamika kama waMachinga wa pwani ya Lindi.

Babu yake Babu Abdallah Seif alikuwa mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga mwenye watumwa baada ya kuwazidi wanyonge majirani kuja kuwatumikisha kujaza vyakula. Mfalme Alei(Ali)waLunga.. wa Lindi.

Baada ya kuja mkoloni Muingereza nchini Tanganyika, aliua ufalme na kubakiza uchifu. Sehemu za pwani ziliathirika kwanza kwa kupoteza ufalme mapema kabla ya watu wa bara.. Pwani wakabakia na usheikh na uchifu... usiokuwa na nguvu kama falme za asili za maeneo yao Lindi / Kilwa kabla ya kuja ukoloni...

Sheikh MbogaBure mjuzi wa lugha ya Kiarabu, dini pia mmoja wa waanzilishi wa madhehebu ya Shia Tanzania amuunganisha Mzee Abdallah Seif kupata scholarship kwenda Baghdad, Iraq mwaka 1968 kusoma zaidi dini...

Kijana Abdallah Seif mwaka 1968 alipokwenda Kijijini ashutumiwa kupotea kwa kuukumbatia u-Shia mojawapo ya madhehebu ya dini ya KiIslamu, wakati wengine wote ni Sunni. Lakini babu yake msomi wa dini madhehebu wa Sunni anayetambulika Lindi na Kilwa hakuwa anatoa shutma zozote alikuwa msikivu na kumtia moyo Abdallah Seif asome zaidi na ili kuifahamu dini vizuri zaidi.

Kilichomsukuma Sheikh Abdallah Seif kuvutiwa na u-Shia ni namna masheikh wa ki-Shia walivyokuwa wazi (tabligh) kukaribisha maswali tofauti na madhehebu mengine ya KiIslam ambapo kijana hakuruhusiwa kuhoji na pia kuuliza maswali ilikuwa inachukuliwa ni utovu wa nidhamu kwa waalimu au masheikh wake.

Safari ya Sheikh Abdallah Seif wenzie vijana wakiwemo kina Sheikh Isihaka Pingili kwenda Iraq kwa meli iliwachukua mwezi mzima kupitia bandari mbalimbali za Zanzibar, Tanga, Mogadishu, Bahrain na kuishia Basra nchini Iraq na kutua katika chuo cha Hawza mji wa Najaf Iraq

Ujio wao Basra, Iraq ulileta tafrani kwa mwenyeji wao Mpakistani mfanyabiashara mkubwa nchini Iraq enzi hizo na kupelekea Saadam Hussein kumshutumu mfanyabiashara huyo tajwa kuleta majasusi wa kiAfrika ikumbukwe ndiyo kwanza Saddam Hussein na chama chake cha Baath walikuwa wanajaribu kushika hatamu za kuongoza nchi baada ya mapinduzi nchini Iraq. Mpakistani huyo alinyongwa mwaka 1969 pamoja na wafadhili wengine kama kuna Bakri Sadr waliowezesha ujio wa vijana wa kiAfrika kuingia Iraq kwa dhumuni la kusoma dini.

Kutokana na hilo ikabidi Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine wa kiAfrika waondoke Iraq mwaka 1970 kwenda Lebanon kwenda kuendelea na azma yao ya kusoma dini.

Sheikh Abdallah Seif wakakaa Lebanon kuanzia mwaka 1970 mpaka 1978 ambapo mara nyingine masomo ya dini yakaingia changamoto baada ya vita baina ya Wapaletina waliokuwa kambi za ukimbizi Lebanon na waLebanon wenye nchi na kuzua vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mwaka 1978 Ikabidi Sheikh Abdallah Seif na wenzie wahamie nchi ya jirani ya Iran kwenda katika mji wa Qom city kuendelea na masomo yao ya dini. Iran ilikuwa imetulia nchi ya amani chini ya utawala wa mfalme (Shah) Mohammed Reza Pahlavi Historic Personalities of Iran: Mohammad Reza Shah Pahlavi miaka 7 waliakaa Iran wakiendelea kusomeshwa.

Wakati wa likizo Iran wengine wenda Ufaransa kuchuma zabibu mashambani au kufanya kazi sehemu za utalii wa ndani wa Iran au kuchukua mabusati ya kushona ya Iran yanayosifika Uarabuni kote kwenda kuyauza ktk nchi mbalimbali za Arabuni ndivyo mwanafunzi kama Sheikh Abdallah Seif na wenzie vijana walivyojiongezea fedha za kujikimu na kupeleka kiasi cha pesa nyumbani Tanzania.

Hatimaye mwaka 1980 baada ya kusoma kwa miaka 11 nje ya Tanzania ,walitunikiwa shahada ya baccalauréat ya masomo ya dini na kurejea Tanzania. Kwa miaka hiyo 11 ughaibuni pia waliweza kusoma elimu ya secular kiwango cha sekondari kwa njia ya posta masomo ya nchi ya Uingereza kwa msaada mkubwa wa swahiba wa kiongozi wa kijeshi wa Nigeria Jenerali Yakubu Gowon. Swahiba huyo alikuwa mfanyabishara wa vituo vya mafuta na makazi yake Uingereza.

Mahojiano haya yanakuja kwa hisani kubwa ya Ammar Dachi aliyemshawishi Mzee Abdallah Seif kufunguka historia ya mapito yake, ukoo , ilmu na utafiti wa mafuta 1955 na pia ujio wa madhehebu ya Shia nchini Tanzania


HISTORIA YA ABDALLAH SEIF (1939 -2020) Part - 2



Sheikh Alhaj Sheikh Abdallah Seif Linganaweka mzaliwa na mwenyeji wa kijiji cha Mnan’gole sehemu za Dimba mkoa Lindi Tanzania anaendelea kusimulia kazi kubwa aliyofanya ya kujitolea ya kueneza dini.

Sheikh Abdallah Seif anasisitiza umuhimu wa ilmu na elimu kwa wanazuoni wote wa KiIslamu.

Anasema ili sheikh awe mwanazuoni aliyekamilika kufundisha chuoni lazima kusoma ilmu ya dini kwa angalau miaka 15.

Anakumbuka alivyokuwa mjini Qom Iran akisoma chuoni alionana na wazee wenye umri wa miaka 70 wakijiendeleza na kuwaambia wao vijana kuwa inahitajika jumla ya miaka 35 ili kuielewa dini nje ndani kwa ufasaha. Wazee hao walicheka waliposikia vijana Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine toka Afrika wakisema wanataka kusoma dini kwa miaka 5 mpaka 10 tu ilihali wametoka Afrika na kuwaambia bila kupepesa macho kuwa ili wawe wabobevu wafikirie miaka angalau 15 ya ilmu ya dini ngazi ya chuo.

Hivyo akiwa amepikika kwa elimu tosha ya kidini baada ya kufanya kazi kwa takriban miaka 11 nchini Tanzania, mwaka 1990 sheikh Abdallah Seifu alikwenda Nampula jimbo la Cabo Delgado nchini Mozambique kufanya kazi ya dini.

Kisha sheikh Abdallah Seif alishuka mpaka mji mkuu wa Maputo Mozambique na alisaidia kufungua taasisi rasmi inayotambulika na serikali na kupewa leseni iliyosajiliwa Maputo Mozambique kwa ajili ya taasisi ya Shia Ithna-Asheri Muzdalifah . Sheikh Abdallah Seif anazungumza lugha za Kiswahili, Kiarabu, Kiingereza na Kireno.

Source : Asadiqmedia

RAMBIRAMBI NA WASIFU - Marhum Sheikh Abdallah Seif



Source : Asadiqmedia
 
Kuna Wairan milioni moja Ulaya.
Ni swala la accessibility .

Hata watanzania wangekuwa na hiyo fursa ya kwenda ulaya wangekuwa wapo zaidi ya hiyo one million ya wairan.

Tunachoangalia ni .
 
Huenda ni Kweli.
Mimi nikisikia Iran najua kabisa ni Taifa la Kishetani kumbe sivyo! Hasa ukizingatia ni Taifa la Kiislam.
Labda ambalo hatujui ni Ubaguzi wa Dini.
Niseme tu ni propaganda za nchi za Magharibi zinazoichafua Iran na kutaka kuchafua ustaarabu wake!
Nchi za Magharibi hazipendi kusikia Taifa lo lote duniani linainuka zaidi yao Kijeshi,Kiuchumi,Kiutamaduni,nk
Lazima Taifa hilo wataliangusha tu!
 
Back
Top Bottom