Nimetembelea shule inayoitwa 'Indian School Dar es Salaam'. Nimegundua wahindi wametuzidi akili sana

Wahindi wapo Dunia mzima na hizi shule zipo dunia nzima
 
Wahindi siyo saizi yetu kwenye ulimwengu wa Elimu.
 
Shule nyingi za serikali hazina hadhi ya kuitwa shule nyingi ni SAwa na maboma ya mifugo. Kuanzia mazingira, viwanja vya michezo, bustani. Angalau zile za seminary unaweza ziita shule
 
Wao wamefanya hivyo kwa sababu wanaamini mtaala wao ni bora kuliko wa kwetu. Vipi kuhusu ninyi, mnafikiria hivyohivyo kwa mtaala wenu?
 
Kwenye top position kwa US ukilinganisha indians na africans indians ni wengi
Moja ya strategies za wahindi (India) ni kuexport utaalamu hasa katika maeneo ya IT. Hivyo huwa wanawapa kiwango cha juu cha elimu watoto wao ili waweze kushindana kimataifa na kushinda kwenye positions mbali mbali.

Hata ukiangalia zile nat geo competitions za wanafunzi wao wa levels tafauti utaona jinsi walivyo juu sana kielimu kuliko sisi.

Strategies za aina hii sisi waafrika hatuna.
 

Uko sawa mkuu. Baadhi yetu tumejibu kwa harakaharaka tu kua kwani kuna nini cha ajabu, ila content wanayosoma na mazingira ya utoaji wa elimu yenyewe ni friendly kwa mtoto. Hili sisi kama Taifa bado mbaya ni kuwa hatuwezi ku maintain consistency ya ubora shule zetu nyingi ni panda shuka kwenye ubora.
 

Tanzania iweke shule nje ya nchi[emoji23][emoji23][emoji23]
Which is which?
Why?
Viwooonder
 

Uko sahihi[emoji817]
 
Indian community.
Arabs commnunity.
Chinise community.

Wamegundua jambo ili kulinda tamaduni zao na kumaintain status zao za maisha.
Ukishindwa kulinda utamaduni wako maana yake umechagua kuwa mtumwa na ni rahisi kuwa manipulated and compromise.

Mwafrica ameshindwa kulinda tamaduni zake na uwepo wake baadala yake amechagua kuishi kiholela na tamaduni zake kampa Mzungu matokeo yake yuko compromised na manipulated na Mzungu kadili Mzingu aonavyo inafaa.
 
Tanzania hatufanyi hivo ndio kwa sababu hatuna sababu ya kufanya hivo kwa sababu hatuna expatriate wengi wa kitanzania wanaofanya kazi nje ukilinganisha na wahindi....

Kwahiyo wahindi kuwa na shule yao hapa sioni kama ni kipimo haswa cha akili..
Kwanini Wahindi wawe wengi kwenye kufanya kazi nchi zingine ikiwemo hapa Tanzania? Na kwa nini Watanzania ni wachche wanaofanya kazi huko nje?

Nasimama na mleta mada, Akili ndio imewafanya wenzetu ikiwemo hawa Wahindi waweze kufanya kazi kwa wingi nchi zingine kwa akutengeneza ajira wao wenyewe. Ukitafuta Watanzania waliotengeneza ajira huko nje nchi zingine unaweza ukapata wachache au usipate kabisa. Sisi tumezoea kusema kubeba box yaani kutumikishwa huko kwa wenzetu.

Wahindi wakija huku kwetu wanawekeza na wala hawatafuti kubeba boksi kama sisi wabongo tukienda kwenye nchi zao.
 
Mimi hata hiyo English hawajanizidi. Wabovu sana hata kingereza hawajui
 
SASA WAO KUWA NA SHULE HUKU NDIO KUTUZIDI AKILI?
 
Mi nimesoma nao huko Punjab, nilikuwa nawaburuza mno.....
Ila wanakariri sana
 
Kuna waafrika kibao kwenye hayo makampuni na taasisi kubwa tatizo ni kwamba hatupendi ku-appreciate vya kwetu.
Wataje basi mkuu maana mwenzio kaweka majina na taasisi kabisa ili nasi tujifunze
 
Haina tofauti na IST au ISM. Labda kilicho kushangaza ni kuwa ya India badala ua UK au USA!
 
Kiongozi kuna vitu vingine ni kuviacha tu ..

Wahindi ni miongoni mwa watu wenye strong culture and religion believes so lazima vitu km hivyo wafanye kujilinda..

Ila pia wapo wengi sana na wamesambaa duniani potee kwa hiyo kuwa na shule ilikuwa muhimu kukidhi haja zao..

tofaut na sisi unaweza kwenda London kuna watanzania labda elfu 1500 tu.. na wapo scattered hapo unadhani kutakuwa na jipya sisi ni watu wakujifungia sana ndani (nchini )maana bado nchi yetu inaweza kutumudu vizuri tu...
 
Ni akili gani unazungumzia ndugu yangu Mushi? Kwa sababu Tanzania kwetu kitu tunachoita ''akili'' pengine ni tofauti katika na akili za mataifa mengine kwani ''akili'' zetu hazionyeshi matunda yoyote. Unaona kama hilo la kuanzisha shule yao yenye elimu ya kiwango cha juu wewe sisi tunaweza tukaona siyo akili lakini mimi nikumbie kitu: hakuna kitu kigumu kama kuji-organize na kufanya kitu chenye manufaa kama hicho. Sisi tumeweza nini kama tuna akili? Mbona hata kuendesha nchi tu imetushinda?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…