Nimeuza kiwanja changu milioni 10, nataka ninunue bodaboda 3. Hii biashara mnaionaje?

Kwenye biashara ya Bodaboda mnufaika ni Mwendeshaji( unaempa kimkataba)

Gharama za bodaboda mpya ni 3,200,000 ambayo mkataba wake wa 10,000 kwa siku huwa ni miezi 15 wengi hufanya, ambayo ni kama 4,500,000 kwa kipindi chote.

Ukitoa na hela ya kununulia itabaki 1,300,000(faida) ukigawa kwa miezi 15 utapata faidA ya kama 80,000 kwa kila mwezi. Ukiongeza miezi ya mkataba inaweza fika 1,500,000 kwa mkataba wote kumalizika kama faida.

Hi faida ni sawa na wastani wa 2,500 hadi 3,500 kwa siku ambayo hata muuza mahindi tena anae choma kwa jioni tuu anakuzidi.

Ikiwa hela hiyo huna uwezo wakufanyia biashara nyingine kuungiza faida zaidi na unataka kuitumia kama hela ya matumizi( yaani kidogo kidogo uwe umaipat) basi kutumia boda boda ni sahihi ila sio biashara ya mtu mwenye malengo anasema anaifanya.
 
Ukishanunua hizo bodaboda mkuu nikupe kijana mmoja wa mkataba....
 
 
Hii naielewa vizuri sana mkuu,nimetoa mkataba toka mwezi wa Kwanza lakini mpaka sasa sina akiba yoyote zaidi ya elfu 20 tu na mkataba unaisha mwezi wa 11 mwaka huu. Ni kama pesa yangu naila kidogo kidogo hakuna cha kusema naweza kununua nyingine mkataba ukiisha labda ninunue kwa chanzo kingine. Sema tu ni kuwa hukosi pesa ya mboga basi lakini mengine hayawezekani. Na jaama wana sound sana,mara mvua mara garage acha tu
 
Aisee kumbe ndio kupo hivyo
 
Biashara ya bodaboda ni biashara kichaa.
Yaani utupe mamilioni kwa mnyoa kiduku.
Biashara hiyo boda akiibiwa mchezo umekwisha.
Biashara hiyo boda akikabwa au kupata ajali kubwa mchezo umekwisha.
Pia hesabu inazingua.
Hiyo biashara tuwaachie WATU CREDITS wao hununua china pikipiki kwa laki 8 Kodi plus tra million 1. Hivyo lazima wapate faida .
 
Nimeuza kiwanja changu jana kilichokuwepo kibaha nimepata milioni 10 nikaona nifanye biashara ya bodaboda nizinunue 3 halafu niwape vijana waniletee hesabu je itanilipa wakuu Kwa mliowahi kufanya hii biashara au nitaingia loss
nunua moja tu alafu test mitambo wewe mwenywewe usimpe mtu, ndyo utajua kama inalipa au hailipi, kama inalipa utafanya maamuzi mwenyewe
 
Nimeuza kiwanja changu jana kilichokuwepo kibaha nimepata milioni 10 nikaona nifanye biashara ya bodaboda nizinunue 3 halafu niwape vijana waniletee hesabu je itanilipa wakuu Kwa mliowahi kufanya hii biashara au nitaingia loss
Bora ununue bajaji uendeshe mwenyewe, bodaboda ni biashara kichaa,hasa kuingia mkataba na mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…