Nimevamiwa nyumbani kwangu na mwanamke niliyempa mimba. Nifanyeje?

Nimevamiwa nyumbani kwangu na mwanamke niliyempa mimba. Nifanyeje?

Acha kuharibia watt wa watu maisha halafu mnakuja humu Tena mnasema. Usioe single Maza ishi na mtt wa watu usimuharibie maisha yake na kwa nn usitumie ndomu wakati unajua huna malengo nae
 
1. Pole Sana mkuu.
2. Si vema KUFANYANA na usiyempenda.
3. Ikilazimika KUFANYANA na usiyempenda fikiria na chukua tahadhari ya mimba na magonjwa ya zinaa.
Hadi hapo tambua kosa ni lako.

Kwa upande mwingine mwenzio alijipanga vizuri zaidi YAKO.
1. Most likely aliitaka mimba YAKO. Kwako ni ajali kwake ni mission accomplished.
2. Sidhani Kama una uhakika kuwa Mimba ni YAKO au umebambikwa.

UNAFANYAJE?
1. Kuwa mpole.
2. Mdodose vizuri ujue tatizo la msingi. INAWEZEKANA hakupendi pia ila hana pa kula Wala kulala.
3. Kama unaweza mpangie chumba au muachie chumba.
4. TAFUTA WATU MHIMU ANAOWESHIMU HIYO MCHUMBA WAKO WAWASHAURI NAMNA YA KUTOKA HAPO
5. Usimfokee, usimtukane, sababu hana pa kushika isipokuwa kwato tu.

Msaidie KWA upendo kuvuka.
Mtavuka wote salama.

USISAHAU KUPIMA DNA. Kuna uwezekano by 50% mimba si YAKO.
Nimekuelewa kiukweli. Nimependa maono yako mkuu. Nitayafanyia kazi
 
Hali uliyo nayo inahitaji utulivu na mawasiliano wazi;

●Mweleze kwa upole na kwa uwazi kuwa unathamini ujauzito na uko tayari kuwajibika, lakini hujajiandaa kuishi naye.

●Jadili namna ya kumsaidia kifedha na kihisia akiwa kwao.

●Weka mipaka ya wazi kuhusu nafasi yako ya binafsi na msimamo wako wa kutotaka kuishi pamoja. Ikiwezekana, tafuta msaada wa mshauri wa mahusiano au mtu mwenye busara kusaidia kufikia mwafaka.

●Licha ya tofauti zenu, zingatia ustawi wa mtoto kwa kushirikiana kwa uwazi na uwajibikaji.
Amin bro
 
Screenshot_20250304-230326_1741118668970.jpg
 
Aliniletea pigo hizo niliita difenda akawekwa ndani,alipoachiwa hakurudi
 
Sisi hatukushika Miguu wakati unaichapa..Uliichakata mwenyewe Starehe ya dakika 5 Matokeo ya Maisha..Hapo ndio wahenga wakasema "UTAVUNA ULICHOKIPANDA" Umepanda mbegu za uzinzi kula Chuma iko
 
Sisi hatukushika Miguu wakati unaichapa..Uliichakata mwenyewe Starehe ya dakika 5 Matokeo ya Maisha..Hapo ndio wahenga wakasema "UTAVUNA ULICHOKIPANDA" Umepanda mbegu za uzinzi kula Chuma iko
Sawa kenge
 
NO sio sahihi kuacha kila kitu kwa malaya angekuwa mke saw. Anachopaswa kufanya aongee na washikaji zake awaambie waje watoe kila kitu cha muhimu cha jamaa kisha wapeleke geto jingine ndo jamaa ahamie huko yani aondoe kila nguo na vitu vya muhimu.

Muhimu siku wanahama jamaa atokee nae out kisha awe anawasiliana na jamaa zake kwa sms wakati wa kurudi yeye na malaya wake amwambie tangulia home napita kwa J mara moja kisha baada ya muda amwambie mimi hapo ni mehama nimekuachia wewe maana umekuja kishari sijajua umekuja kwa nia gani kwangu nahofia usalama wangu. Ishi hapo mimba nitahudumia kama kawaida kisha piga kimyaa
Kumbe waharibifu wa watoto wetu wengi mko JF ?!
 
Niliachana na mke wangu mwaka jana baada ya kutofautiana mienendo. Japo hatukufunga ndoa ila nilimposa na kila kitu tulikamilisha tukaanza maisha.

Baadae niliamua kutafta mwanamke mwingine tukawa na mahusiano ya kawaida tu, na hatukuwa tukiishi wote. Mwezi uliopita tulizinguana na kila mmoja akapita na mambo yake japo siku kadhaa kabla ya kuachana aliwahi kunidokezea kuwa anahisi ana mimba yangu. Sikufikiria kitu kwa vile hakuwa na uhakika na hali ile.

Bas bwana, zikapita siku nne baada ya kuachana akaomba tuonane. Sikukataa na nilifanya hivyo. Alinipa taarifa rasmi kuwa amefanya UPT na majibu yanaonesha ni kweli amebahatika kuwa na mimba japo haukuwa mpango wetu.
Nilipokea taarifa kisha kila mtu akaendelea na mambo yake.

Baada ya muda aliomba tuende clinic ya kwanza kama yalivyo maelekezo ya wadau wa afya kuwa mahudhurio ya kwanza ni lazima waende wahusika wa ujauzito kwa ajili ya vipimo. Hapo nilichenga kulingana na nature ya kazi yangu..... niko busy sana mda mwingi. Siku zilisonga na alipewa barua ya kumruhusu kusajiliwa na kuanza clinic bila ya uwepo wangu.

Juzi nipo zangu kwangu (japo nimepanga) nikiwa napumzika mara paap!! Mabegi na mazagazaga yote ya yule mwanamke. Alipita hadi ndani kisha akawa mkali na maneno makali sana. Alinipa uhakika kuwa ameamua ahamie kwangu rasmi kwa sababu ya mimba japo sikuwahi kukataa kumtunza na kuilea mimba. Ila kiufupi ni kuwa nimevamiwa na mke.

Binafsi sijakubaliana na hii hali na sikumwonesha mwitikio hasi juu ya maamuz yake yaliouchukiza moyo wangu.

Sasa wadau hizi scenario huwa mnazitatuaje asee. Me sielewi yani ila nataka nimtoe niendelee na maisha ya kivyangu na nimtunze akiwa kwao hukohuko.

Karibuni kwa maoni
Kwanza umeshasema umevamiwa na mke sidhani kama mke anavamia. Anakuja kama alivyokuja.

Vipi wewe kwa upande wako, unaweza ruhusu binti yako aliyejazwa mimba alelewe kwako? Siku hizi ndoa zinatafutwa kwa kila mbinu ameshakuwa mke huna namna
 
Utakuja kujuta kuweka huyo mwanamke ndani ya Nyumba yako,

Ila ulikosea sana hapa:

“Baada ya muda aliomba tuende clinic ya kwanza kama yalivyo maelekezo ya wadau wa afya kuwa mahudhurio ya kwanza ni lazima waende wahusika wa ujauzito kwa ajili ya vipimo. Hapo nilichenga kulingana na nature ya kazi yangu..... niko busy sana mda mwingi. Siku zilisonga na alipewa barua ya kumruhusu kusajiliwa na kuanza clinic bila ya uwepo wangu.“

Mwanamke ukimpa mimba na huna mpanfo wa kukaa naye au kufanya maamuzi ya kuishi naye kwa haraka, ni muhimu sana kucheza na saikolojia yake na kuwajibika!
 
Niliachana na mke wangu mwaka jana baada ya kutofautiana mienendo. Japo hatukufunga ndoa ila nilimposa na kila kitu tulikamilisha tukaanza maisha.

Baadae niliamua kutafta mwanamke mwingine tukawa na mahusiano ya kawaida tu, na hatukuwa tukiishi wote. Mwezi uliopita tulizinguana na kila mmoja akapita na mambo yake japo siku kadhaa kabla ya kuachana aliwahi kunidokezea kuwa anahisi ana mimba yangu. Sikufikiria kitu kwa vile hakuwa na uhakika na hali ile.

Bas bwana, zikapita siku nne baada ya kuachana akaomba tuonane. Sikukataa na nilifanya hivyo. Alinipa taarifa rasmi kuwa amefanya UPT na majibu yanaonesha ni kweli amebahatika kuwa na mimba japo haukuwa mpango wetu.
Nilipokea taarifa kisha kila mtu akaendelea na mambo yake.

Baada ya muda aliomba tuende clinic ya kwanza kama yalivyo maelekezo ya wadau wa afya kuwa mahudhurio ya kwanza ni lazima waende wahusika wa ujauzito kwa ajili ya vipimo. Hapo nilichenga kulingana na nature ya kazi yangu..... niko busy sana mda mwingi. Siku zilisonga na alipewa barua ya kumruhusu kusajiliwa na kuanza clinic bila ya uwepo wangu.

Juzi nipo zangu kwangu (japo nimepanga) nikiwa napumzika mara paap!! Mabegi na mazagazaga yote ya yule mwanamke. Alipita hadi ndani kisha akawa mkali na maneno makali sana. Alinipa uhakika kuwa ameamua ahamie kwangu rasmi kwa sababu ya mimba japo sikuwahi kukataa kumtunza na kuilea mimba. Ila kiufupi ni kuwa nimevamiwa na mke.

Binafsi sijakubaliana na hii hali na sikumwonesha mwitikio hasi juu ya maamuz yake yaliouchukiza moyo wangu.

Sasa wadau hizi scenario huwa mnazitatuaje asee. Me sielewi yani ila nataka nimtoe niendelee na maisha ya kivyangu na nimtunze akiwa kwao hukohuko.

Karibuni kwa maoni
Halafu kesho na kesho kutwa mnaanza kuwananga Single mothers!!!!
 
Hiv inakuwaje mnakaa kabisa na mtu ambae hauna mpango nae. Hebu fikiria angekuwa mwanao ungefurahia aaribikiwe maisha kabisa. Unaenda kumfanya mtoto wa mtu mzinzi mazima kwa tamaa zako.
Bota mtu tu anakua ni mtu mzima, hii ya kutia mimba halafu "nitalea" ni mbaya sana.

Mtoto hapati malezi ya baba wala babu, hawa singo maza sio wazuri sana kwenye malezi, mijini watoto wanaharibikiwa sana.
 
Back
Top Bottom