Nimezaa na mke wa mtu watoto wawili na ana mimba ya tatu

Status
Not open for further replies.
Wakuu asalaam Aleikum, Tumsifu Yesu Kristo, Bwana Yesu Asifiwe, nawasalamu kwa jina la Jamhuri ya Muungano.

Nije kwenye mada mimi ni mwanaume ambaye kidogo nimeshavuta vuta umri kiasi (niko around 40+) nina mke na watoto watatu. Lengo la kuja hapa naomba tupeane ushauri. Binafsi nimezunguka mikoa mbalimbali katika kutafuta riziki, mwaka 2012 nikiwa Dar na familia ikiwa mkoani nilikutana na dada mmoja bank flani hapohapo Dar.

Nikiwa kwenye foleni ya kuchukua visenti vyangu nyuma yangu kulikuwa na mwanadada ambaye ni kama age mate wangu tofauti yetu ni kama miaka miwili, yaani namzidi miaka 2.

Huyu dada alikuwa hana kalamu kwa ajili ya kujazia ile slip ya benki, hivyo akaniomba kalamu, nami bila hiana nikampatia huku nikiendelea kusogea counter ili nichukuwe visenti vyangu. Wakati namaliza kuchukuwa hela naye alikuwa amemaliza kujaza ile karatasi hivo akawa anasogea counter, yeye alikuwa ana depost hela.

Akanipatia kalamu yangu nikajivuta nje ya benki na hatimaye barabarani kusubiria daladala, nikiwa bado nasubiri daladala huyu dada akawa amekuja huku akiwa na ki IST chake akaniuliza unaelekea wapi nikamwambia Mwenge alafu Mbezi, akanIambia twende nikusogeze na hapo ndo mazungumzo yalianza.

Alinieleza mambo mengi kuhusu familia yake kuwa yeye ni yatima hamjui mama wala baba na alikuwa ameolewa mkoa fulani hivi lakini kutokana na tabia za mmewe waliamua kuachana, yeye kachukuwa watoto wake kuja Dar. Tangu siku hiyo tukaanza mazoea na hatimaye mahusiano. Kwa bahati mbaya yeye akataka sana ni muoe kitu ambacho mimi sikuweza kwa sababu tayari nilikuwa na mke.

Baada ya mahusiano ya takribani miaka mitatu huyu dada akapata mtu wa kumuoa na akanijulisha kuwa anaolewa kwa hiyo uhusiano wetu umefika mwisho , nikamwambia sawa na namba akabadilisha. Baada ya miezi sita akanipigia simu na namba mpya akaniomba samahani na kunIambia kama bado uko Dar naomba tuonane na kipindi hiki mimi pia nilikuwa nimeshaleta familia yangu Dar, nikamwambia sawa.

Tukakutana kwenye ile hoteli aliyofia yule mzee wa miaka 80 akiwa na binti. Akaniomba tena samahani na usema kuwa tangu ameolewa hajawahi kuinjoi penzi, kwani mume wake hata dakika hamalizi anakuwa ameshakojoa na hawezi kurudia tena, kinachofuata ni kuomba samahani tu. Nikamuuliza kwa hiyo nikusaidiaje? akasema 'kama kuna dawa unaijua naomba nimpelekee m'ume wangu', nikamwambia sina dawa na akanipa tena mzigo nikagonga na akawa amepata ujauzito siku hiyohiyo.

Tumeendelea na uhusiano mpaka sasa na nimeshamzalisha watoto wawili na ana mimba ya tatu anatarajia kujifungua mwezi wa nane.

Kwa sasa yeye na mume wake hawaishi Dar ila kwa kuwa ni mfanyabiashara mara nyingi anakuja Dar kuchukuwa mzigo na mbinu anayotumia akitaka kuja na akiwa na lengo la kubeba ujauzito anakuja akiwa anakaribia zile siku za hatari, hivyo tunafanya yetu alafu anarudi kwa mumewe.

Akifika kwa mume kwa kuwa mume anaifahamu kalenda yake mwanamke atajifanya ameingia period na kuvaa pedi kama kawaida na baadaye anamtegeshea jamaa anagonga alafu mwanamke anamwambia ameshika ujauzito.

Hii mbinu kwa upande wa mwanamke imefanya kazi vizuri lakini kwangu sasa naumia na natamani damu yangu, kwa lugha nyingine nahitaji hawa watoto wangu. Mke wangu hajui lakini yule mume mwenzangu pia hajui. Lakini ananijua tu kwa jina kwani mara nyingi amewahi kufuma sms zangu kwenye simu ya mkewe na kunipigia simu akiomba niachane na mke wake kwa kuwa anampenda sana mkewe.

Mwaka jana baada ya kuwa amekaa muda tangu kujifungua mtoto wa pili nikamtania hutaki tena kuzaa akasema nataka lakini naona kama wameisha make jamaa miaka yote nimemwachia jamaa lakini sishiki mimba, nikamwambia njoo tujaribu hii ilikuwa ni mwezi akaja na matokeo kashika mimba ya tatu tena. Kiuchumi yuko vizuri tu ana biashara zake, na mume ni mfanyakazi Serikalini.

Hebu tushauriane nini nifanye make natamani hawa watoto wangu ukizingatia mke wangu hazai tena na watoto wetu ni wakubwa wa mwisho amemaliza six anaenda JKT, wawili wako chuo. Na huyu jamaa akijua kinachofuata ni yale ya SAIDI. Mwanamke ananisihi sana nisaidae hawa watoto ila ikitokea mume wake amekufa kabla yangu atawaambia watoto ukweli tofauti na hapo hawezi na ananiomba sana nisithubutu.
Dah, pole sana Mzee.. hii imenifanya nikumbuke ile speech ya Prof Kabudi with a say kuwa 'Fathers are always happy kwenye Familia hata kama wanajua those children are biologically NOT theirs. Hii ni kwa upande wa pili

Sema I would advise u- focus na maisha yako maana ulifanya mistake kwenda kulima shamba la jirani japo umepata matakeo lakini forget about it and move the hell on vinginevyo ukifunguka utazua mambo mengine

The good thing upo mbali na huyo mwanamke with her Family achana nae na focus na maisha yako that's all
 
Hamna tatizo umewasaidia kufanya sperm donation.

Kuliko wangekosa watoto kabisa.

Kukubwa mie azidi kumheshimu mumewe na kumsitiri.

Jamaa atakuwa Baba mlezi na heshima yake ibaki palepale kama ya Baba mzazi.
 
Sema sasa unapofanya sperm donation hutakiwi kuwa na husuda tena hao watoto .

Nazi ikidondokea ndani wa ukuta wa jirani ni ya huyo jirani usiende kuiulizia maana kwanza unaweza uziwa kesi kuwa huenda ilimdokea mtu kichwani na yuko mahututi utafanyaje si bora upotezee ?!
 
Katika mazingira hayo werevu watakuelewa lakini sasa usijiweke karibu sana na kutaka ijulikane wewe ndie baba mzazi .

Dunia iko na mambo mengi sana.

Na yalikuwepo tangu enzi za mababu.
 
Sasa chakushangaza Mwanaume wa ndoa wa huyo jamaa utasikia amezaa nje na mchepuko,

Hapo mke ndio atakuwa confused kwa vipi ? Wakati jamaa hajiwezi kushughulika ipasavyo?!

Ndio unakuta kama ni mtu wa neema ya vijisenti mchepuko anamchomekea kuwa nina mimba yako kumbe anataka kuzidi kumwibia vihela vyake [emoji108]

Wajinga ndio waliwao!
 
Umefanya vema umemsitiri kwa kum-support muhimu usijiweke Karibu nao baki kuwa rafiki tu wa huyo mwanamke pasipo hila yoyote.
 
Kwanza ongea na mkeo. Ongea kwa mafumbo. Atakubali kupokea na kulea watoto hao? Akikataa, utawapeleka wapi? Pata majibu ya maswali haya kwanza. Mimi nathamini damu yangu kwa kweli.
 
Hata kwenye surrogate procedure makubaliano mtoto akishazaliwa haonwi na mama alibeba mimba,

Mtoto anakabidhiwa Kwa baba alotoa mbegu na mama alitoa yai.

Na baada ya hapo ndio ntoleee imeisha hiyo !
 
Kuonesha kwanza ulifanya hisani ya sperm donation usijiingize kwenye gharama ya kutunza hao watoto,

Wacha wawajibike wenyewe.

Ukikosea ukajichanganya utafuta ile dhamiri yako njema ya awali kisha utakuwa kama mhuni tu na mharibifu wa nyumba za watu.

Usimpe hela huyo mwanamke.
 
Mkuu ukiwa na kifua bas nyamaza...hate sisi wenzako tuna hali Kama yako lkn tumenyamaza..nakusihi wewe nyamaza..tulia...kula maisha..
Hamuwatendei haki watoto. Ipo siku dada na kaka wataoana. Watoto wana haki ya kujua biological parents wao.
 
Kwanza wanaume wengine wanawaruhusu kabisa wake zao wakabebe mimba nje ilimradi wawatunzie Siri wasimwambie mtu!

Dunia ina mengi sana bado hatujayasikia wala kuyaona!
 
Kwani kwenye kadi za clinic majina wa watoto ubini uko wa Baba yupi mzazi au mlezi ?

Kama mlezi hainashida awalee kiroho Safi Kama damu yake.

Mtoto anazingatia anachoona na kukua Nacho , huyo ndio watamtambua kama baba mzazi na mlezi wao.
 
Wakuu asalaam Aleikum, Tumsifu Yesu Kristo, Bwana Yesu Asifiwe, nawasalamu kwa jina la Jamhuri ya Muungano.

Nije kwenye mada mimi ni mwanaume ambaye kidogo nimeshavuta vuta umri kiasi (niko around 40+) nina mke na watoto watatu. Lengo la kuja hapa naomba tupeane ushauri. Binafsi nimezunguka mikoa mbalimbali katika kutafuta riziki, mwaka 2012 nikiwa Dar na familia ikiwa mkoani nilikutana na dada mmoja bank flani hapohapo Dar.

Nikiwa kwenye foleni ya kuchukua visenti vyangu nyuma yangu kulikuwa na mwanadada ambaye ni kama age mate wangu tofauti yetu ni kama miaka miwili, yaani namzidi miaka 2.

Huyu dada alikuwa hana kalamu kwa ajili ya kujazia ile slip ya benki, hivyo akaniomba kalamu, nami bila hiana nikampatia huku nikiendelea kusogea counter ili nichukuwe visenti vyangu. Wakati namaliza kuchukuwa hela naye alikuwa amemaliza kujaza ile karatasi hivo akawa anasogea counter, yeye alikuwa ana depost hela.

Akanipatia kalamu yangu nikajivuta nje ya benki na hatimaye barabarani kusubiria daladala, nikiwa bado nasubiri daladala huyu dada akawa amekuja huku akiwa na ki IST chake akaniuliza unaelekea wapi nikamwambia Mwenge alafu Mbezi, akanIambia twende nikusogeze na hapo ndo mazungumzo yalianza.

Alinieleza mambo mengi kuhusu familia yake kuwa yeye ni yatima hamjui mama wala baba na alikuwa ameolewa mkoa fulani hivi lakini kutokana na tabia za mmewe waliamua kuachana, yeye kachukuwa watoto wake kuja Dar. Tangu siku hiyo tukaanza mazoea na hatimaye mahusiano. Kwa bahati mbaya yeye akataka sana ni muoe kitu ambacho mimi sikuweza kwa sababu tayari nilikuwa na mke.

Baada ya mahusiano ya takribani miaka mitatu huyu dada akapata mtu wa kumuoa na akanijulisha kuwa anaolewa kwa hiyo uhusiano wetu umefika mwisho , nikamwambia sawa na namba akabadilisha. Baada ya miezi sita akanipigia simu na namba mpya akaniomba samahani na kunIambia kama bado uko Dar naomba tuonane na kipindi hiki mimi pia nilikuwa nimeshaleta familia yangu Dar, nikamwambia sawa.

Tukakutana kwenye ile hoteli aliyofia yule mzee wa miaka 80 akiwa na binti. Akaniomba tena samahani na usema kuwa tangu ameolewa hajawahi kuinjoi penzi, kwani mume wake hata dakika hamalizi anakuwa ameshakojoa na hawezi kurudia tena, kinachofuata ni kuomba samahani tu. Nikamuuliza kwa hiyo nikusaidiaje? akasema 'kama kuna dawa unaijua naomba nimpelekee m'ume wangu', nikamwambia sina dawa na akanipa tena mzigo nikagonga na akawa amepata ujauzito siku hiyohiyo.

Tumeendelea na uhusiano mpaka sasa na nimeshamzalisha watoto wawili na ana mimba ya tatu anatarajia kujifungua mwezi wa nane.

Kwa sasa yeye na mume wake hawaishi Dar ila kwa kuwa ni mfanyabiashara mara nyingi anakuja Dar kuchukuwa mzigo na mbinu anayotumia akitaka kuja na akiwa na lengo la kubeba ujauzito anakuja akiwa anakaribia zile siku za hatari, hivyo tunafanya yetu alafu anarudi kwa mumewe.

Akifika kwa mume kwa kuwa mume anaifahamu kalenda yake mwanamke atajifanya ameingia period na kuvaa pedi kama kawaida na baadaye anamtegeshea jamaa anagonga alafu mwanamke anamwambia ameshika ujauzito.

Hii mbinu kwa upande wa mwanamke imefanya kazi vizuri lakini kwangu sasa naumia na natamani damu yangu, kwa lugha nyingine nahitaji hawa watoto wangu. Mke wangu hajui lakini yule mume mwenzangu pia hajui. Lakini ananijua tu kwa jina kwani mara nyingi amewahi kufuma sms zangu kwenye simu ya mkewe na kunipigia simu akiomba niachane na mke wake kwa kuwa anampenda sana mkewe.

Mwaka jana baada ya kuwa amekaa muda tangu kujifungua mtoto wa pili nikamtania hutaki tena kuzaa akasema nataka lakini naona kama wameisha make jamaa miaka yote nimemwachia jamaa lakini sishiki mimba, nikamwambia njoo tujaribu hii ilikuwa ni mwezi akaja na matokeo kashika mimba ya tatu tena. Kiuchumi yuko vizuri tu ana biashara zake, na mume ni mfanyakazi Serikalini.

Hebu tushauriane nini nifanye make natamani hawa watoto wangu ukizingatia mke wangu hazai tena na watoto wetu ni wakubwa wa mwisho amemaliza six anaenda JKT, wawili wako chuo. Na huyu jamaa akijua kinachofuata ni yale ya SAIDI. Mwanamke ananisihi sana nisaidae hawa watoto ila ikitokea mume wake amekufa kabla yangu atawaambia watoto ukweli tofauti na hapo hawezi na ananiomba sana nisithubutu.
Muoe mbona brother unasubiria Nini kikao Cha juzi tulikubaliana mke was pili ni lazima
 
Juzi tu wanawake ndo tulikuwa mashetani kwa usaliti leo nae mwanaume mkubwa wa mashetani, anajua anachofanya sio fair ila bado anafanya.

Siku hizi wanaume wanadanga kuliko hata wanawake. Ona anavyo jimwambafai ati mwanamke ana hela dah .

Mungu hawa viumbe wote wapige matukio wakome umalaya.
 
Kuni zako zitakazotumika kukuchoma kule mbinguni zitakuwa za gas[emoji16]
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom