Nimwombe Rais Samia awaondoe haraka wanajeshi wetu kule DRC Congo. Mnapigana na nchi ya EAC

Nimwombe Rais Samia awaondoe haraka wanajeshi wetu kule DRC Congo. Mnapigana na nchi ya EAC

Hii inaenda kuwa kashfa kama ile ya Biafra tulisapoti wrong side katika History badala kujikita kwenye kupatanisha.

Col. Ojukwu hivi aliwahi hata kuja Nchini kutembelea makaburi ya Askari wetu kweli?

Au alikuwa anakaa kwenye Mahoteli ya hali ya juu na kubadilisha Wasichana Warembo huko Abidjan?
Sijui nani amewashauri kushiriku kuingilia huo mgogoro mgumu hivyo!
 
Bahima Empire,Plundering and piracy ya resources ndio msingi mkubwa wa mauaji ya raia wasio na hatia..

Hatuwezi kuwa salama kama nchi ikiwa tutabariki uharamia wa rasilimali kwa wenzetu (DRC) wenye impact kubwa kwenye uchumi wetu..Logistics infrustructure and trade.

Tukizembea na kujizima data ipo siku M24 wataingia Ngara,Geita,Kahama,Biharamulo..
Tatizo la DRC halitaisha kama DRC yenyewe haitakuwa serious kulimaliza, hata wapelekwe mamilioni ya wanajeshi.
 
..SADC wanatakiwa kwenda KIVITA na kufukuza waasi wote.

..baada ya hapo eneo hilo lilindwe na askari wa SADC na kuwe na demilitarized zone ktk mpaka wa DRC na Rwanda.

..Na vita hiyo wasiachiwe Tanzania, Malawi, na South Africa, peke yao. Nchi zote za SADC ziamue kwa kauli moja kumtetea mwanachama mwenzao.
Unamteteaje mtu ambaye hayuko tayari hata kutetewa na haoenekani kuwa na nia thabiti ya kumaliza matatizo yake?
 
Watusi bwana mijinga sana.Wanajeshi wa Tanzania wako Msumbiji, Lebanon, Central Africa Republic n.k hizo ni kazi zao kufa hata wakibaki makambini wanauza maduka watakufa.Mbona wanajeshi wa Rwanda wanakufa Hapo Msumbiji? Wanajeshi wa Tanzania wakiwa chini ya Munusco mwaka juzi waliokufa wengi zaidi ya hao watatu.Huyu Mama sio poyoyo kama huyo slim wenu huko Kigali.
 
Mkuu 'imhotep' usichanganye mambo na kuweka uongo usiokuwa na miguu ili kunogesha unakokupigania wewe. Biafra na DRC havina uhusiano wowote. Ni wakati sasa mwambieni kiongozi wenu Kagame kuwa hamuwezi kuwa nyinyi watu tofauti na wengine. 'Model' mnayoifuata ya wayahudi ni tofauti kabisa na haya mnayoyasukuma nyinyi.
Kubalini, kuishi na watu wengine mnaoishi nao, msijione nyinyi mnayo haki au utofauti wowote na raia wengine mnaoishi nao mitaani.
Kagame ana matatizo yake ila DRC ndiyo yenye matatizo makubwa zaidi katika kushindwa kumalizika kwa huo mgogoro.
 
Heshima mkuu, lakini kuhusu hili sina sababu kabisa ya kuingia youtube kama unavyo nishauri. Kenya walifanya utapeli wa hali ya juu sana na kumdanyanya Tishekedi kuwa watakwenda kupambana na M23. Walipofika Goma wimbo ukabadilika na kusema wao hawakuja kupigana vita bali kulinda amani. Hakuna mahali popote Kenya alipowasambaratisha M23, bali walianza kushirikiana na M23 na kukubaliana M23 aondoke baadhi ya maeneo kimkakati, ili kuhadaa serikali ya Congo.

Unanishangaza sana unapo sifia mafanikio waliyopata Kenya kwa kazi waliyofanya Congo, wakati imelazimika waondoke kwa aibu kubwa baada ya kustukiwa udanganyifu waliokuwa wakiufanya.
Huyo Nyaga unayemwonyesha hapo, hivi hujui alivyoondoka Congo kwa aibu?
Hata kikosi cha SADC ambacho Tanzania amechangia jeshi hawajaenda DRC kupambana na M23, kama wanafanya hivyo ni kinyume na mission iliyowapeleka ya peacekeeping.
 
1. Rwanda na Uganda wanatoa wapi budget ya kufadhili maasi dhidi ya DRC? Kama budget ya kufadhili maasi ipo, basi budget ya kuzima uasi lazima chanzo chake kip.

2. DRC wataweza kusimika mifumo ya ulinzi, usalama, na utawala, ikiwa kutakuwa na mazingira ambako hakuna uasi. Hata jeshi letu Jwtz lilianzishwa baada ya uasi wa Tanganyika Rifles kuzimwa na Muingereza, na Nyerere kuwa na " space " ya kufanya what was needed to be done.
Uasi wa Tanganyika Rifles ni tofauti sana na uasi unaoendelea DRC kwa miongo mingi, uasi wa DRC unahusisha ukabila, rasilimali na mipaka ya nchi na hivyo hautazimwa kijeshi, unaweza kutulizwa kwa muda tu ila utaibuka tena na tena.
 
1. Rwanda na Uganda wanatoa wapi budget ya kufadhili maasi dhidi ya DRC? Kama budget ya kufadhili maasi ipo, basi budget ya kuzima uasi lazima chanzo chake kip.

2. DRC wataweza kusimika mifumo ya ulinzi, usalama, na utawala, ikiwa kutakuwa na mazingira ambako hakuna uasi. Hata jeshi letu Jwtz lilianzishwa baada ya uasi wa Tanganyika Rifles kuzimwa na Muingereza, na Nyerere kuwa na " space " ya kufanya what was needed to be done.
Uasi wa Tanganyika Rifles ni tofauti sana na uasi unaoendelea DRC kwa miongo mingi, uasi wa DRC unahusisha ukabila, rasilimali mipaka ya nchi na hivyo hautazimwa kijeshi, unaweza kutulizwa kwa muda tu ila utaibuka tena na tena.
 
..DRC iliwahi kuruhusu majeshi ya Rwanda na Uganda yafanye operation dhidi ya waasi toka nchi zao lakini " tatizo " liko palepale.
DRC ni kubwa sana, hao waasi wana nafasi kubwa sana ya kujificha na kusogea sehemu nyingine kisha wakarudi baada ya majeshi ya hizo nchi kuondoka.
 
..DRC iliwahi kuruhusu majeshi ya Rwanda na Uganda yafanye operation dhidi ya waasi toka nchi zao lakini " tatizo " liko palepale.
Sasa hivi kinachotakiwa ni mapatano kati ya serikali ya DRC na M23 halafu huo mzozo ukiisha DRC ishirikiane na Rwanda na Uganda ili kulisafisha hilo Pori na kuwakamata Magaidi ya ADF na FDLR na kuyavunja Makundi madogo madogo ya Waasi kama Mayi mayi na Wazalendo
 
Kagame ana matatizo yake ila DRC ndiyo yenye matatizo makubwa zaidi katika kushindwa kumalizika kwa huo mgogoro.
Hebu tujaribu kidogo kuweka tofauti, hata huko DRC. Sidhani kuwa itakuwa sahihi kulinganisha aliyokuwa akifanya Mobutu, Kabila Sr, na Kabila Jr. katika mgogoro huo.
Ndiyo, hata hawa waliopo madarakani sasa wanatakiwa kuweka juhudi zaidi kumaliza mgogoro huo, lakini hilo haliwezi kuonekana kwamba hawafanyi kitu kama walivyo kuwa watangulizi wao.
 
Mbona huwa mnasema jeshi letu ni imara kuliko la Rwanda, sasa inakuwaje wanaingiza ubaridi tena? Au jeshi letu ni dhabiti kwenye kudhibiti rais wasio na silaha ambao hawaikubali ccm?
sasa hapo umejibu nini sasa? tumia akili angalau kidogo

wewe unaona ni akili ncho mwanachama wa EAC kupigana na nchi ya EAC ? KAGAME anapigana congo DRC ambayo ni nchi mwanachama wa EAC .sasa EAC ina maana gani kuwepo?ni bora ikasambaratika tu
 
Sasa hivi kinachotakiwa ni mapatano kati ya serikali ya DRC na M23 halafu huo mzozo ukiisha DRC ishirikiane na Rwanda na Uganda ili kulisafisha hilo Pori na kuwakamata Magaidi ya ADF na FDLR na kuyavunja Makundi madogo madogo ya Waasi kama Mayi mayi na Wazalendo
hapa shida ni kwamba hilo kundi la M23 ni la watusi asili ya Rwanda ,burundi na uganda wanatafuti kujitenga na DRC.kwa hiyo kagame anawatetea wenzake kama alnavyokiri kwenye hiyo clip
 
Hata kikosi cha SADC ambacho Tanzania amechangia jeshi hawajaenda DRC kupambana na M23, kama wanafanya hivyo ni kinyume na mission iliyowapeleka ya peacekeeping.
Hapana. Kikosi cha SADC ni cha mapambano na M23, ndiyo matakwa ya DRC walio waalika kwenda huko; tofauti kabisa na kikosi cha Kenya ambacho walidai wanakwenda kupambana, lakini walipofika Goma, 'mission' ikabadilika. Ndiyo maana Tshekedi na serikali yake walipoligundua hilo, wakaamua kuachana nao na kuwaamuru waondoke.

Kikosi cha SADC kipo ku'enforce peace', siyo ku-peacekeep.'

Ndiyo maana unaona sasa makombora yakirushwa na kuua askari SADC: Afrika Kusini na Tanzania sasa. Kabla ya hapo hukusikia kikosi cha Kenya, au hata Monusc walioishi Kongo kwa miaka zaidi ya 25 wakishambuliwa na waasi hao.
 
Na Kagame siyo wa mchezo mchezo. Ni Putin wa Afrika huyu, akiamua kumung'oa mama jua halizami.

PK aliwahi kumwambia JK, I will hit you!. JK hakutia neno.
Rwanda na Tanzania ni mbingu na ardhi yule hawezi kupigana na jeshi la Tanzania watamchakaza vibaya sana
Nchi yenyewe sawa na mkoa wa Tabora
 
Hiyo vita sio ya kuisha leo wala kesho provided M23 wana support ya nchi jirani. Adui (makundi yote ya waasi) wakizidiwa wanauwezo wa kupotea haraka kama walivyo na uwezo ku-mobilise jeshi haraka hali ikitulia na kulianzisha tena.

Tanzania na wasaidizi wengine waipe Congo ultimatum msaada wa kijeshi uende sambamba na serikali ya Congo kuwekeza heavily kwenye jeshi lao kulinda mipaka yao na kuli-control hilo eneo. Awawezi kuli-control hilo eneo ifike wakati tuache fate ichukue mkondo wake kama ni annexation ya eneo let it be aitokuwa nchi ya kwanza kumegwa kwa sababu ya serikali kushindwa ku-control eneo.

Bila ya Congo kutoa road map ya adhma yao ya kuli-control hilo eneo miaka 20 baadae bado tutakuwa tunapeleka askari wakati wenyewe huko Kinshasa wako busy kuboresha mikorogo na kukata mauno.

Ifike hatua lazima Tanzania ione seriousness ya Congo kutaka kulinda himaya zake yenyewe kabla ya kuji-commit kuwasaidia miaka zaidi ya 20 ya kuwasaidia inatosha kama wenyewe hawana mpango wa kuweka strong military presence huko. Kwani sisi nani alitusaidia Amini alipoitaka Kagera si wenyewe tulilinda eneo letu.

Let them annex it kama wa-Congo wameshindwa kulilinda eneo lao inatosha, watasaidiwa mpaka lini.

Iła M23 lazima nae atiwe adabu kipindi hiki kwa kuuwa askari wa Tanzania, lazima ajue sumu aionjwi.
Inaonekana askari wetu wanamalizwa sana huko tunafichwa idadi tu
 
Sijajua wanajeshi wetu wanafia nini kule DR congo wakati sasa imejulikana bila shaka kwamba wanapigana na wanajeshi wa Rwanda ambayo ni nchi mwanachama wa EAC.

SOLUHISHO ya vita ile ni kuiwekea vikwazo RWANDA na kuifukuza EAC haraka iwezekanavyo.

Mama yetu mpendwa nakuomba uwaondoe haraka watoto wa taifa letu wanaopigana na M23 kule DRC.damu yao inamwagika kwa sababu gani?


View: https://www.youtube.com/watch?v=HHtxvhSPgAQ&t=124s&pp=ygUWdGhlIHBlb3BsZSAgd2hvIGFzayBtZQ%3D%3D

nchi yako unayoiona iko salama haitakua salama muda wote!
nadhani unauelewa mdogo juu ya foreign affairs
na huelewi chochote juu ya sera ya mambo ya nje ya nchi hii
 
Back
Top Bottom