Uko sahihi 100%
Na kibaya zaidi na ambacho hakisemwi ni kwamba makabaila ndo wanokoleza mgogoro kwa manufaa yao.
Angalia msaada wanopewa M23 ambao wajumuisha vifaa cya kisasa kabisa.
Nimeongelea jambo hili lakini nahisi Goma na Kivu yote vitakuwa chini ya M23 na Rwanda bado watuhumiwa kuwa wapo nyuma yao.
Jiulize inakuwaje watu wązito wamehudhuria juzi maadhimisho ya mauaji ya Kimbari?
Bill Clinton, mwakilishi wa Israeli, majasusi waandamizi wa barani Ulaya na Marekani, makampuni ya kigeni na hata wawakilshi wa Ukrainę walikuwapo.
Hivyo mgogoro huu si wa kuhusu mipaka tu bali pia wahusisha wenye dunia na suala zima la siasa za kijiografia.