Hapana. Kikosi cha SADC ni cha mapambano na M23, ndiyo matakwa ya DRC walio waalika kwenda huko; tofauti kabisa na kikosi cha Kenya ambacho walidai wanakwenda kupambana, lakini walipofika Goma, 'mission' ikabadilika. Ndiyo maana Tshekedi na serikali yake walipoligundua hilo, wakaamua kuachana nao na kuwaamuru waondoke.
Kikosi cha SADC kipo ku'enforce peace', siyo ku-peacekeep.'
Ndiyo maana unaona sasa makombora yakirushwa na kuua askari SADC: Afrika Kusini na Tanzania sasa. Kabla ya hapo hukusikia kikosi cha Kenya, au hata Monusc walioishi Kongo kwa miaka zaidi ya 25 wakishambuliwa na waasi hao.