Nimwombe Rais Samia awaondoe haraka wanajeshi wetu kule DRC Congo. Mnapigana na nchi ya EAC

Sijui nani amewashauri kushiriku kuingilia huo mgogoro mgumu hivyo!
 
Tatizo la DRC halitaisha kama DRC yenyewe haitakuwa serious kulimaliza, hata wapelekwe mamilioni ya wanajeshi.
 
Unamteteaje mtu ambaye hayuko tayari hata kutetewa na haoenekani kuwa na nia thabiti ya kumaliza matatizo yake?
 
Watusi bwana mijinga sana.Wanajeshi wa Tanzania wako Msumbiji, Lebanon, Central Africa Republic n.k hizo ni kazi zao kufa hata wakibaki makambini wanauza maduka watakufa.Mbona wanajeshi wa Rwanda wanakufa Hapo Msumbiji? Wanajeshi wa Tanzania wakiwa chini ya Munusco mwaka juzi waliokufa wengi zaidi ya hao watatu.Huyu Mama sio poyoyo kama huyo slim wenu huko Kigali.
 
Kagame ana matatizo yake ila DRC ndiyo yenye matatizo makubwa zaidi katika kushindwa kumalizika kwa huo mgogoro.
 
Hata kikosi cha SADC ambacho Tanzania amechangia jeshi hawajaenda DRC kupambana na M23, kama wanafanya hivyo ni kinyume na mission iliyowapeleka ya peacekeeping.
 
Uasi wa Tanganyika Rifles ni tofauti sana na uasi unaoendelea DRC kwa miongo mingi, uasi wa DRC unahusisha ukabila, rasilimali na mipaka ya nchi na hivyo hautazimwa kijeshi, unaweza kutulizwa kwa muda tu ila utaibuka tena na tena.
 
Uasi wa Tanganyika Rifles ni tofauti sana na uasi unaoendelea DRC kwa miongo mingi, uasi wa DRC unahusisha ukabila, rasilimali mipaka ya nchi na hivyo hautazimwa kijeshi, unaweza kutulizwa kwa muda tu ila utaibuka tena na tena.
 
..DRC iliwahi kuruhusu majeshi ya Rwanda na Uganda yafanye operation dhidi ya waasi toka nchi zao lakini " tatizo " liko palepale.
DRC ni kubwa sana, hao waasi wana nafasi kubwa sana ya kujificha na kusogea sehemu nyingine kisha wakarudi baada ya majeshi ya hizo nchi kuondoka.
 
..DRC iliwahi kuruhusu majeshi ya Rwanda na Uganda yafanye operation dhidi ya waasi toka nchi zao lakini " tatizo " liko palepale.
Sasa hivi kinachotakiwa ni mapatano kati ya serikali ya DRC na M23 halafu huo mzozo ukiisha DRC ishirikiane na Rwanda na Uganda ili kulisafisha hilo Pori na kuwakamata Magaidi ya ADF na FDLR na kuyavunja Makundi madogo madogo ya Waasi kama Mayi mayi na Wazalendo
 
Kagame ana matatizo yake ila DRC ndiyo yenye matatizo makubwa zaidi katika kushindwa kumalizika kwa huo mgogoro.
Hebu tujaribu kidogo kuweka tofauti, hata huko DRC. Sidhani kuwa itakuwa sahihi kulinganisha aliyokuwa akifanya Mobutu, Kabila Sr, na Kabila Jr. katika mgogoro huo.
Ndiyo, hata hawa waliopo madarakani sasa wanatakiwa kuweka juhudi zaidi kumaliza mgogoro huo, lakini hilo haliwezi kuonekana kwamba hawafanyi kitu kama walivyo kuwa watangulizi wao.
 
Mbona huwa mnasema jeshi letu ni imara kuliko la Rwanda, sasa inakuwaje wanaingiza ubaridi tena? Au jeshi letu ni dhabiti kwenye kudhibiti rais wasio na silaha ambao hawaikubali ccm?
sasa hapo umejibu nini sasa? tumia akili angalau kidogo

wewe unaona ni akili ncho mwanachama wa EAC kupigana na nchi ya EAC ? KAGAME anapigana congo DRC ambayo ni nchi mwanachama wa EAC .sasa EAC ina maana gani kuwepo?ni bora ikasambaratika tu
 
hapa shida ni kwamba hilo kundi la M23 ni la watusi asili ya Rwanda ,burundi na uganda wanatafuti kujitenga na DRC.kwa hiyo kagame anawatetea wenzake kama alnavyokiri kwenye hiyo clip
 
Hata kikosi cha SADC ambacho Tanzania amechangia jeshi hawajaenda DRC kupambana na M23, kama wanafanya hivyo ni kinyume na mission iliyowapeleka ya peacekeeping.
Hapana. Kikosi cha SADC ni cha mapambano na M23, ndiyo matakwa ya DRC walio waalika kwenda huko; tofauti kabisa na kikosi cha Kenya ambacho walidai wanakwenda kupambana, lakini walipofika Goma, 'mission' ikabadilika. Ndiyo maana Tshekedi na serikali yake walipoligundua hilo, wakaamua kuachana nao na kuwaamuru waondoke.

Kikosi cha SADC kipo ku'enforce peace', siyo ku-peacekeep.'

Ndiyo maana unaona sasa makombora yakirushwa na kuua askari SADC: Afrika Kusini na Tanzania sasa. Kabla ya hapo hukusikia kikosi cha Kenya, au hata Monusc walioishi Kongo kwa miaka zaidi ya 25 wakishambuliwa na waasi hao.
 
Na Kagame siyo wa mchezo mchezo. Ni Putin wa Afrika huyu, akiamua kumung'oa mama jua halizami.

PK aliwahi kumwambia JK, I will hit you!. JK hakutia neno.
Rwanda na Tanzania ni mbingu na ardhi yule hawezi kupigana na jeshi la Tanzania watamchakaza vibaya sana
Nchi yenyewe sawa na mkoa wa Tabora
 
Inaonekana askari wetu wanamalizwa sana huko tunafichwa idadi tu
 
nchi yako unayoiona iko salama haitakua salama muda wote!
nadhani unauelewa mdogo juu ya foreign affairs
na huelewi chochote juu ya sera ya mambo ya nje ya nchi hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…