Nimwombe Rais Samia awaondoe haraka wanajeshi wetu kule DRC Congo. Mnapigana na nchi ya EAC

Congo imekuwa na vita muda mrefu sana hata kabla Kagame na Museveni hajawa watawala wa nchi zao.
 
Na Kagame siyo wa mchezo mchezo. Ni Putin wa Afrika huyu, akiamua kumung'oa mama jua halizami.

PK aliwahi kumwambia JK, I will hit you!. JK hakutia neno.
Ww mzee kikwete alimjibu kiswahili zaidi uliza operation aliyo fanya kukimbiza wakimbizi mbona mpaka huyo fala pk alinyoka.Kama kweli yy ni mwanaume aingie bongo tutamzingua mamaae zake.
 
Congo imekuwa na vita muda mrefu sana hata kabla Kagame na Museveni hajawa watawala wa nchi zao.

WAKONGOMANI tangu APRIL 1, 1966 walikuwa tayari wameshaanza kukiwasha wao kwa wao. Hapo PK na M7 walikuwa bado wanasoma SHULE ZA MSINGI 😁
 
Kuna hii conspiracy
Ya kuwa Uganda itakuwa chini ya tusi empire baada ya museveni kupigwa chini na Kijana wake kushika mikoba

Huku kagame kule.kijana, congo kasikazini m23, burudi wataweka mtu wao. Huku Kuna Akina biteko. Bahima empire inajijenja taratiibu
 
Na Kagame siyo wa mchezo mchezo. Ni Putin wa Afrika huyu, akiamua kumung'oa mama jua halizami.

PK aliwahi kumwambia JK, I will hit you!. JK hakutia neno.
Acha Uongo..

Alimjibu "Sio kwamba sijui wanayopanga juu yetu ila nimeamua kukaa kimya"..

Kisaha akaanzisha operation kimbunga..
Kagame hakuwahi jibu wala kuongea tena..

Acha kumfananisha Putin na vitu vya kijinga..
 
Na Kagame siyo wa mchezo mchezo. Ni Putin wa Afrika huyu, akiamua kumung'oa mama jua halizami.

PK aliwahi kumwambia JK, I will hit you!. JK hakutia neno.
Je alim hit?ni mkwara tu hana lolote huyo kimbaumbau
 
Ndio uelewe sasa hata hiyo hoja ya mabeberu kusababisha vita ili kuiba madini ya DRC haina mashiko sana.
Haina mashiko kwa mtu aliyevaa mawani ya mbao, na kusahau mikakati ya kupambana na China juu ya mali hizo hizo katika eneo hili. Tunaangalia maswala ya kidunia kirahisi rahisi kwa kutumia 'one dimensional view' na kusahau mikakati pana zinazotumiwa na hawa watu.
Hivi kwani ushiriki wa hao mabeberu katika eneo hilo umeanza leo na mgogoro huo wa Kagame na M23?
 
Damu yao inamwagika sababu ya Pesa, wanalipwa wale we unataka warudi waje kufanya kazi gani? Wameajiriwa kuua na kufa.
 
Wanachokivuna Congo ni matokeo ya kulumbatia serkali mbovu kama sisi tunavyokumbatia CCM leo, hatuchekani sana naona tu Wafu tunazikana sema wao wametangulia.
 
Clip zipo, zinanesha akimkaripia Kikwete kwenye media. Siyo story za vijiweni
Ndiyo zipo. Lakini unakumbuka kilichompata huyo huyo aliyekaripia na wala asijibu chochote baada ya hapo?
Nkuruziza alipotaka kupinduliwa, ulisikia huyo huyo aliyekuwa mbele ya njama hizo akikohoa baada ya kujuwa kwamba Tanzania ipo tayari kumtia adabu akiendelea na mpango huo?
Udoho wa nchi siyo sababu, angalia umahiri wa jeshi lake. Kwani Irael kubwa?
Rwanda ya Kagame siyo Israel hata kwa mbali sana, pamoja na kuwa wanapenda sana kujifananisha hivyo. Israel wenyewe na umahiri wao, bila 'sponsor' wao wakuu Marekani na Ulaya Magharibi hali yao ingekuwa matatani sana katika eneo hilo.
 
Hauko sahihi. Hicho ni Kikosi maalumu (Force Intervention Brigade - FIB) ndani ya walinzi wa amani wa UN (MONUSCO) kikiwa na jukumu la kupambana na waasi kama M23 (Enforcement under chapter 7 of the UN Charter).
Sijui kama wewe atakuelewa, maana nilishamweleza hataki kuelewa!
 
Congo imekuwa na vita muda mrefu sana hata kabla Kagame na Museveni hajawa watawala wa nchi zao.

..Mhhh!!

..kuliwahi kutokea massi huko nyuma, lakini kulikuwa na utulivu wa kiwango fulani wakati wa Mobutu.

..Laurent Kabila alitawala kwa amani kwa kipindi kifupi sana, kabla hajavamiwa na waasi waliofadhiliwa na Rwanda, na Uganda.

..Ni ukweli usio na mashaka kwamba waasi wanaofadhiliwa na Rwanda na Uganda wamesababisha vifo na maafa makubwa kuliko wakati wowote ule baada ya uhuru wa Congo.
 
Hopefully watafata ushauri sahihi zaidi hapa, umemaliza kila kitu mkuu
 
I agree na wewe... wenye nchi hawako serious ndio maana wanatishwa na majirani kila siku.
 
Songwe ni mkoa wa kawaida sana kibiashara unazidiwa hata na Iringa.

..amani ktk nchi jirani ni neema kwa nchi yetu.

..kuna biashara kubwa kati ya Kenya na Tanzania kutokana na amani iliyoko ktk nchi zetu majirani.

..sasa fikiria tukiwa na majirani wengine zaidi ya Kenya wenye amani na mafanikio ya kiuchumi nchi yetu itafaidika kwa kiwango gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…