Nina haja ya dhati Lamomy wa JF kwenye maisha na huduma yangu daima

Nina haja ya dhati Lamomy wa JF kwenye maisha na huduma yangu daima

Namshukuru Mungu kwa ajili ya yako na yangu, kwa wasaa huu muhimu, ambao ni zawadi kutoka kwa Mungu kwetu sisi sote.

Tumeipewa zawadi hii bure na tuitumia bure, na kwahivyo yatupasa kuitumia vizuri kadiri tuwezavyo na kwa uaminifu, huku tukimshukuru yeye pekee daima, kila wakati tunapopata wasaa wa kufanya hivyo.

Namsalimu sana mtumishi, msaidizi wangu mpendwa sana na kipenzi cha haja ya moyo wangu Lamomy popote alipo.

Namuombea kwa Mwenyezi Mungu ulinzi mkali sana wa kiroho na kimwili uambatane nae daima kila mahali anapotekeleza majukumu, kazi na mahangaiko yake ya kila siku.

Milango yangu ya kimwili na kiroho iko wazi daima kwajili yake, na saa zingine inalala wazi usiku na mchana ikitazamia ujio wake wakati wowote maishani mwangu katika Roho na kweli ya Mungu.

Namuomba Roho Mtakatifu ahuishe nafsi yake Lamomy ilainike na ipate kuskia sauti ya wito wa Mungu kwake dhidi yangu.

Afungue moyo wake uweze kutambua na kujua vema nia, haja, makusudi na madhumuni yangu mema sana kwake na yenye baraka, neema, sifa na utukufu wa Mungu daima na milele....

Lamomy katika dhiki na faraja daima na milele.

Kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
Jambo la KHERI Uchumba wenu ukazaa ndoa mkaishi kwa AMANI na UPENDO kama mlivyoelekezwa kwenye Mafundisho ya Dini yenu.

Mvumiliane kwenye nyakati ngumu, mkumbuke kufanya ibada maana maombi hufungua mengi.

Inshallah nakutakia kheri
 
Kuwa makini mkuu usije ukawa unatongoza mke wa mtu, pia jaribu kusoma tabia zake huyo bidada usibabaishwe na uzuri wake iwapo tabia si njema. Muhimu hakikisha ni mtu mwenye tabia njema, mwenye kujistiri, awe anajua kujishusha mbele ya mumewe. Mbali na hapo utajitafutia matatizo bure .

Nakutakia kheri
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Kumekucha

Hivi makamanda wenzangu mbona hamnipendi? Au ndio mko busy na kuipambania katiba mpya?
Kila siku mimi napendwa na vijana wa Mama Kizimkazi!!! Why? Makamanda mnaniangusha [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
CCM wananibeba hivyo ooh!!!

Kwako baba mtumishi Tlaatlaah
Nashukuru kwa kunipenda ingawa sijui umenipenda na umevutiwa na kitu gani na mimi? Sio kesi hata mimi NAKUPENDA km Yesu alivyolipenda kanisa. UPENDO WA AGAPE
Mahusiano na ndoa ni jambo jema, hata vitabu vya Mungu vinatuasa mtu mume na mtu mke waungane wawe mwili mmoja ili waijaze dunia. Ndiomana hata Mungu alivyomuumba Adam hakuona sahihi akamletea msaidizi ambaye ni Hawa ( Ambao ndio sisi kina Lamomy)
Ahsante kwa upendo na mapenzi yako makubwa uliyoonyesha kwangu.
Najua mpaka kuamua kuja na uzi km huu ulichukua muda mrefu kujipanga na kujiandaa hukukurupuka!!! Kuna kitu kilikusukuma moyoni mwako. [emoji120]

Sasa baba mtumishi pamoja na yote hayo mwenzio mimi mpenzi wa mtu na mpenzi wangu yupo humu humu tena mwana CCM mwenzio. Nampenda kuliko maelezo.
Sina haja ya kumficha anaitwa Countrywide mwenyewe nimezoea kumuita Kantry nampenda chugga man wangu. Samahani kwa kusema haya.

Mwisho nikuombe usikate tamaa kutafuta yule ambaye atakuwa chaguo lako na utakayempenda kwa dhati ya moyo.
Nasikia uchungu kukujibu hivi lakini ndio hivyo siwezi kumuacha nimpendaye kwaajiri ya kumfurahisha mtu mwingine.
Damu ya Yesu ikulinde baba mtumishi.
Aimen [emoji120]
Ila Wanawake Eeeeht nasikia uchungu kukujibu hivi?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wakati kajibu mtext mrefu hatari hivi unajua text za uchungu zilivyo. Km ulikuwa na Nia ya kumkataa ungeandika lines 2 tu kwisha hbr ss maneno kibao uwenda ilikuwa ushatengeneza matumaini ya Jibu zuri moyoni kwake.?
 
Watumishi wa Mungu hatujibu km nyie wa mataifa πŸ˜‚
 
Namshukuru Mungu kwa ajili ya yako na yangu, kwa wasaa huu muhimu, ambao ni zawadi kutoka kwa Mungu kwetu sisi sote.

Tumeipewa zawadi hii bure na tuitumia bure, na kwahivyo yatupasa kuitumia vizuri kadiri tuwezavyo na kwa uaminifu, huku tukimshukuru yeye pekee daima, kila wakati tunapopata wasaa wa kufanya hivyo.

Namsalimu sana mtumishi, msaidizi wangu mpendwa sana na kipenzi cha haja ya moyo wangu Lamomy popote alipo.

Namuombea kwa Mwenyezi Mungu ulinzi mkali sana wa kiroho na kimwili uambatane nae daima kila mahali anapotekeleza majukumu, kazi na mahangaiko yake ya kila siku.

Milango yangu ya kimwili na kiroho iko wazi daima kwajili yake, na saa zingine inalala wazi usiku na mchana ikitazamia ujio wake wakati wowote maishani mwangu katika Roho na kweli ya Mungu.

Namuomba Roho Mtakatifu ahuishe nafsi yake Lamomy ilainike na ipate kuskia sauti ya wito wa Mungu kwake dhidi yangu.

Afungue moyo wake uweze kutambua na kujua vema nia, haja, makusudi na madhumuni yangu mema sana kwake na yenye baraka, neema, sifa na utukufu wa Mungu daima na milele....

Lamomy katika dhiki na faraja daima na milele.

Kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
Ni dume hilo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Back
Top Bottom