Nina Mgogoro kwenye ndoa, kila pesa anayopata Mke wangu anaenda kujenga kwao. Naomba msaada

Usifundishe wanao wa kike hii tabia.
Maisha yalivyo changamoto ndo maana mabinti wanadanga kutafuta kulelew...
Sikia soma mwanzo upate kuelewa Mungu alimweka mwanaume kuwa kichwa cha familia sio mkia, kuna up and downs za kimaisha msaada unapewa pale unahitaji ila sio kila saa. Nainawezekana isiwe mke ndio anakupa pesa ni washkaji familia sio lazima mke ndio maana maisha bila baba hayasongi kabisa .

Endelea tu kudanganywa kuwa hela alizopata ni zako single mother sio rahisi mtu kuwa ujue na usione wenzako walicheza sebene Leba , huijui leba ,so heshimu sana wanawake wenye kunitolea kuwaza watoto.

Na uache upuuzi, mnajaza wasichana wawatu mnakimbia kusubiri 50% kwenye ndoa. Wanaume wote wangekuwa kama wewe maisha yasingekuwa hivyoo.

Unadharau wanadamu eti wamekuwa single mothers mxiuu hata mkeo ni single mother kwa hali hii nipo serious haya
 
Madeni yanaua, hapo deni ni zaidi ya Tsh.50m, tafuta namna ya kujikwamua kwenye huo mzigo (si kulipa bali kujiweka safe side). Wakati anakopa ulimuuliza mortgage aliyoweka ni ipi? Isije ikawa mnaishi kwenye nyumba ya madeni
Sheria ya Tanzania mke anaweza kukopa kwa dhamana hata ya msharaha wa mumuwe😂😂.

Pia amekopa fasta million 47 sijui ana mshahara kiasi gani ?
 
Wazee hawapo? Je hao washenga huna habari nao? Vipi kuhusu wazazi wenu? Usimweke mkeo humu ni sawa na wewe kuvua nguo mbele ya mkweo wa kike. Futa hii kitu ulio weka.
Acha ushamba we mzee. Mkewe aliyemuanika humu unamfahamu jina? Mleta mada umemtambua? Wanaodhalilishwa umewatambua?

Hii sio Facebook kwamba unatumia real name, hizi fake ID.
 
Acha ushamba we mzee. Mkewe aliyemuanika humu unamfahamu jina? Mleta mada umemtambua? Wanaodhalilishwa umewatambua?

Hii sio Facebook kwamba unatumia real name, hizi fake ID.
Sigara ngumu sibishani na wewe.
 
Sikia soma mwanzo upate kuelewa Mungu alimweka mwanaume kuwa kichwa cha familia sio mkia...
Kunywa maji kwanza upunguze presha maana maneno yanakutoka hata kilichoandikwa hujaelewa.

1. Acha kukariri mimi wala sio mwanaume ni mama tena mwenye watoto wengi wa kiume na wa kike.

2. Baba ni nguzo ya kiuchumi ya familia among other things, lakini mfumo wa maisha umebadilika baba huyo huyo alipe ada, anunue chakula, ajenge nyumba, awekeze kwaajili ya watoto, akupe mama hela ya mahitaji ya kike, bado hamjatoka out wazazi na muda mwingine kama familia.... bado majukumu ya kijamii ya hapa na pale.

Muda huo mama upo tu MY MONEY IS MY MONEY huyo baba si atatembea anaongea njiani?

Na atajikuta anaishia kubangaiza, ila penye ushirikiano na mgawanyo wa majukumu hata kufikia uhuru wa kifedha ni rahisi, watoto wenu hawatokua na haja ya kusaidiana majukumu na wake zao maana familia imeshatoka huko.

3. Mtoto ni zao la starehe siku hizi vijana hawaoi kwa sababu mbalimbali lakini sababu moja wapo ni ndoa kuwa kama mzigo majukumu ni mengi so bora mtu apige mechi za hapa na pale mimba ikitokea anakula kona au anatoa tu matunzo

Nawahurumia vijana wanaojitafuta na wanatoka familia za kawaida, kuoa itawachukua muda sana maana nayo imekua ni uwanja wa vita na kujiongezea majukumu
 
Wanawake hua hawana ufikili mzuri
Kwa bahati mbaya hua hawaelewi pia
Acha tu mkuu kwakua ishatokea
 
Kwa sababu wewe unaona ambacho yeye haoni...wewe tulia Tu ...subiri mda ufike ajifunze mwenyewe....
Nenda nae taratibu...ukifika wakati anagombea nyumba na ndugu zake ndo umwambie nilikuonya Sana ...unaona??..

Kwa sasa subiri Tu mda utatoa majibu
Mkuu mm ni mtu tofauti sana spending kusubiri yeye atatangulia keenye nyumba akawasubiri ndg zake, my takni kuwa she will go.. dintaish naye
 
Huyo mkeo na ww wote ni wapuuzi,27 mil nyumba ya Mzee anayesubiri muda wake mmeshindwa kuimaliza?na ukute ni bush.Lawama ni zako mkuu hukuwa Mshauri mzuri au mkeo kakukalia chapati
 
Ndugu yangu hapo wewe unawaza kuhusu familia yenu yeye anawaza kuhusu familia yao ,,,,hautoboi pambana mwenyewe kesi ni ngumu hiyo yeye hawez ona maono unayoyaona wewe.
 
Kwanza nyote mnashida. Uliona wapi mtu anachukuwa mkopo kwenda kujenga nyumba ya wazazi? Unaruhusu mkeo anachukuwa mkopo kwaajiri ya kujengea mama mkwe. Halafu hela za kulipa mtakuwa mnazitowa kwenye mshahara wenu? Unatuzinguwa na story za pwagu na pwaguzi.
 
😄😄Pole sana chief wew apo akili mkichwa hauna mke apo chakufanya wapambanie wanao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…