Nina Mgogoro kwenye ndoa, kila pesa anayopata Mke wangu anaenda kujenga kwao. Naomba msaada

Kwenye swala la pesa siyo mke wakp tu ila binadamu akipata pesa hubadalika, Why do people change when they have money?
 
We ni hovyo, tafuta kibunda. Achana na pesa za mkeo.
 

Chai

"akakopa banki 27M lakini nyumba haijaisha"
 
sijaona unacho lalamika, kwanza mkeo anakupenda ndiyo mana amekushirikisha kuna wengine wanakopa kimya kimya na wanawapa wanawowafanyia masagi kimya kimya!
 
Kama anajenga kwa pesa yake ni sawa,huo mkopo atalipa yeye..wewe pesa yako jenga hiyo yako,ingekua ni mimi ningemwacha ajenge kiroho safi
Ni kweli mkuu yeye amuache cha muhimu aombwi pesa ya ujenzi wala pesa ya kulipa deni. kingine na yeye akope pesa ajenge nyumba yake au na yeye awajengee wazazi wake nyumba.
 
Mkuu wanawake nao wana haki ya kujenga makwao kama wanaume wanavyo waboreshea wazazi wao kijijini, lakini inategemea na mira na tamaduni, mfano kwa sisi Mwanamke akishaolewa ana kuwa sehemu ya familia ya Mwanaume na kujenga au kuwajengea wazazi nyumbani kiijin ni vigumu, kwasababu mtoto wa kike hapati mirathi, mfano kwenye kugawana aridhi mtoto wakike hapati.
 
Mlikuwa mkoani,je mkeo ni mkimya? Nadhani mpaka inafika hii hatua kuna sehemu uligusa na hajaongea.

Binadamu akichoka kabisa huwa haongei na hilo ni jambo linapikwa kuhusu madhara sijui maana itategemea na mienendo yenu huko nyuma ulimjali vipi na ulifanya nini wakati hana
 
Kaka pesa ya mke huwa sio ya familia .hongera umejua unaishi na shetan nakushauri Anza ujenzi wa nyumba na ww kisirisiri ambayo hata mkiachana asiijue kabisa .pia nasisitiza PIMA WATOTO WOTE DNA .Utanishukuru
 
Sasa mkuu huyo Mwanamke siku wazazi wake walifariki na mirathi ikigawanywa unazani hiyo nyumba ataimiliki yeye Mwanamke, na kama kajenga kwenye kiwanja cha familia , wazazi waki Afrika ukiwajengea nyumba kwenye maeneo yao elewa kwamba kama mpo watoto kumi kwenye mirathi mnagawana sawa, na Wazazi wetu kuandika wosia ni ngumu, wanajua wakiandika wosia utaleta chuki kwa watoto.
 
Jambo ambalo unatakiwa kufahamu siku zote, mshahara wa mke siyo mshahara wako!
Ila mshahara wako ni mshahara wa mkeo!
Kwa mantiki hiyo siku zote Mwanaume ishi kana kwamba ni wajibu wako kumtunza mkeo na watoto wako! Familia ni ya Mwanamme siyo ya Mwanamke.
Hata hivyo kwa hili la kumjengea Mzazi wake nyumba siyo kosa la kukufanya ujute kuoa!
 
Afadhari wanawake muongee maana kuna wanaume ni wanawake hadi kuwazidi wanawake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…