Nina miaka 27, bado nina ndoto ya kuwa Daktari (Médical Doctor)

Nina miaka 27, bado nina ndoto ya kuwa Daktari (Médical Doctor)

Zamani nilidhani madaktari wanamaisha mazuri sana pengine kuliko career zote...kumbe hapana, bora uwe katibu mwenezi wa ccm tu, huitaji kusoma sana but maslai yake utalisha ukoo mzima.
 
Kombi yoyote yenye P iheshimiwe tu. Jamaa yangu alipiga 1.8 pale Tanga Tech na kwenye PCM kanyoosha A tatu. Form six Ilboru akagonga div III. Mwingine one ya 9 form form four ila div 4 form 6. Bahati nzuri wale walikuwa ni vipanga wakaamua kwenda Diploma DIT mambo ya maabara. Walinyoosha vibaya hadi wakamaliza degree zao kwasasa wote wako kwenye green pastures.
Sema nilisikiaga open university wanatoa foundation course inayo kuwezesha kwenda kusoma degree ya md na course zngne kwa mwaka mmoja sema cjafatilia sn
 
Mkuu Angalia Sababu zao na matokeo yao angalia mazingira na mtoa mada ya matokea pia
Utapata Jibu
Hivi unajua mtu akitumia miezi hata 3 anatoboa hiyo PCM Vizuri kiufupi kufaulu ni Kucheza na mbinu Mimi Advance nilisoma kwa Mwezi 1-2 mfululizo na nikapata kitu Safi so kwa mtu anyesoma kwa njia ya kusolve Maswali yaani mtu anayesoma msuli paper hawezi shindwa kutumia miezi 5 kupata One

Zamani watu walikuwa wanafeli kwanza MAZINGIRA magumu na walikuwa hawana resources
 
Mkuu Angalia Sababu zao na matokeo yao angalia mazingira na mtoa mada ya matokea pia
Utapata Jibu
Mazingira ya sasa ya elimu yameimarika, hivyo mtoa mada anaweza tu kufanya vyema akitia nia na jitihada.
 
Hivi unajua mtu akitumia miezi hata 3 anatoboa hiyo PCM Vizuri kiufupi kufaulu ni Kucheza na mbinu Mimi Advance nilisoma kwa Mwezi 1-2 mfululizo na nikapata kitu Safi so kwa mtu anyesoma kwa njia ya kusolve Maswali yaani mtu anayesoma msuli paper hawezi shindwa kutumia miezi 5 kupata One

Zamani watu walikuwa wanafeli kwanza MAZINGIRA magumu na walikuwa hawana resources
Ok mkuu nikuulize maswali machache....
Kutoka Olevel mpaka advance ulitumia Mda gani kusoma au kuunganisha...
Ulikaa nyumbni kwa muda gani kabla ya kuunga Vamce
 
Zamani nilidhani madaktari wanamaisha mazuri sana pengine kuliko career zote...kumbe hapana, bora uwe katibu mwenezi wa ccm tu, huitaji kusoma sana but maslai yake utalisha ukoo mzima.
🤣🤣🤣
 
Lengo
Sema nilisikiaga open university wanatoa foundation course inayo kuwezesha kwenda kusoma degree ya md na course zngne kwa mwaka mmoja sema cjafatilia sn
Kazi Kama udaktari , ualimu , kilimo hizo ni kazi za jamii ukiwa na tamaa Sana lazima utakimbia mapema katika game

Nadhani Kazi anayofanya Mwalimu ni ngumu Sana as the same daktari na mkulima haya ndo makundi muhimu katika nchi yetu so ukiwaza maokoto na sio Huduma lazima utadata sana
 
Kumbe sipo peke angu aisee.. nilimaliza form six pcb 2017 nikala viv 2 ya point 12 nikiwa na physics D, chemistry C na biology E kwa shinikizo la kutoka familia duni kuhofia kukosa mkopo na competition iliyokuepo mwaka wetu kwny kozi za afya nikajikuta nasomea ualim wa physics na chemistry japo ndoto zangu ilkua MD, binafsi kuna muda nataman sana nirud kufukuzia ndoto zangu ila majukum na tushaanza kishika vi miambili miatatu inakua ni ngum jurud shulen
Polee mkuu lakini bdo una nafasi kubwa ya kuendelea Tena kwako wew una apply tu moja kwa moja kwa sababu una bachelor ya sc...Apply moja kwa moja MD
 
Kwa miaka 27 upo katika umri sahihi Sana , After six years utakuwa na 33 na kwa Huwezo wake Mungu utakuwa unaitwa doctor MD.

Fanya hivi sajiri mtihani kwa mwaka mmoja means ufanye mtihani mwakani mwezi wa tano then Kama upo dsm tembelea michikichini huko Utakutana na waalimu na wabobezi wa hizo Kazi za private Candidate .

Ukisoma kwa kumaanisha hata miezi mitano unatoboa vizuri tu so hapo nunua review zakutosha then vitabu na solve Sana Maswali Naamini hautokosa B tatu katika paper la six

Usisikilize maneno yenye negativity kuwa hautaweza au huwezi stay away with negativity
Fuata hili wazo bwanamdogo ww bado kinda
 
Lengo

Kazi Kama udaktari , ualimu , kilimo hizo ni kazi za jamii ukiwa na tamaa Sana lazima utakimbia mapema katika game

Nadhani Kazi anayofanya Mwalimu ni ngumu Sana as the same daktari na mkulima haya ndo makundi muhimu katika nchi yetu so ukiwaza maokoto na sio Huduma lazima utadata sana
KZi ya daktari ina lawama Nyingu Plus Fikra kubwa inayokubana wew kufanya kazi kuna watu wanadhani unaweza hata kufufua na hiyo ndo changamoto 😅😅
 
Kwa Miaka ya 2013 hasa shule zile za Kata mtu Akipigwa division 3 huyo kichwa kweli unakuta shule nzima wapo watatu au watano mfano 2014 shule yetu Ngoreme secondary walifaulu wanafunzi 10 (ones to three) Darasani wapo zaidi ya 90,,,, coz unakuta mtu anasoma kwa life gumu hakuna Twition Wala walimu wa kufundisha kwaiy kutoboa unakuta kipengere kweli anakomaa mwenyew. Kuliko mnjin ambapo unakuta mtoto ana Kila kitu ndo maana inakua Rahisi kufaulu.

Ila kwa Miaka ya saivi kuanzia 2020..... Form four imekua kama La Saba tu mtoto anae zingua Form 4 huyo kweli Hana akili Yani ni bumunda kweli,, ndo maana mtu unakuta amepata division 1 lakin kichwan hamna kitu kabisa tofouti na Elimu ya zamani ambapo mtu akifaulu means kupata division 1-3 huyo ni kichwa kweli lakin Leo watoto wanamaliza secondry lakin kichwan ni empty mno. Hadi degree na kwenyewe saivi imekua mdobwedo nilishangaa sana Kuna mdada alimaliza pale Udsm education lakin Cha ajabu yule demu kichwan hamna kitu kabisa binafsi nikwa najiuliza hivi huyo ndo anaenda kufundisha secondary kwa akili mbovu kiasi kile. Kwa kweli Elim ya Tz kadri siku zinavyo zidi kwenda ile Thamani yake inaisha kabisa Bora nchi za wenzetu ukiwa na Hela chukua mtoto mpeleke nje huko. Apate Elimu Bora huko anakua na exposure ya Maisha. Kuliko Huku Bongo.
Twition = tuition, kwaiy = kwa hiyo, kipengere = kipengele, mnjin = mjini. Ngoreme sec ilikuwa lazima mfeli. Mlikuwa vilaza na wewe kwa uandishi huu umetuwekea ushahidi usiotia shaka. Huna uhalali wa kusema huyo mhitimu wa UDSM yuko empty wakati wewe ni mhitimu kilaza wa Ngoreme sec.
 
Kwasasa hiyo kozi sio ngumu mazingira ya kusoma ni rahisi na mtaala wao wamepanuliwa goli ushindwe wewe tu.

Kitu pekee kwao kitawatesa ni GPA kufaulu ni rahisi mno ila wengi wanapata GPA za kawaida.
Ukweli mtupu
 
Hivi unajua mtu akitumia miezi hata 3 anatoboa hiyo PCM Vizuri kiufupi kufaulu ni Kucheza na mbinu Mimi Advance nilisoma kwa Mwezi 1-2 mfululizo na nikapata kitu Safi so kwa mtu anyesoma kwa njia ya kusolve Maswali yaani mtu anayesoma msuli paper hawezi shindwa kutumia miezi 5 kupata One

Zamani watu walikuwa wanafeli kwanza MAZINGIRA magumu na walikuwa hawana resources
Naona umeanza kutapika ujinga wako
 
Sema nilisikiaga open university wanatoa foundation course inayo kuwezesha kwenda kusoma degree ya md na course zngne kwa mwaka mmoja sema cjafatilia sn
Foundation course mpKa uwe umemaliza Form six na ukapata angalau Principle moja kama hukusoma Cha six hawawwz kukupokea
 
Unaongea nadharia mwanafunzi kilaza ambaye hasomi na Hana juhudi hawezi kuipata hiyo one .
Usibishe ukiwa hujafanya research Mkuu. Hichi kitu n kweli kabisa Elimu ya Tz ile Thamani yake haipo kabisa zamani mtu akifaulu namanisha miaka ya 90 mpaka 2014 au tuseme 2010 kwa shule za Government huyo ni kichwa kweli kuliko miaka ya Leo ambapo unakuta shule imefaurisha wanafunzi wote lakin wale ambao unakuta akili zipo ni wachache Mno uwezo ule wa kuyaelewa mambo n mdogo mno coz mwanafunzi anameza wew hata bila kuelewa anaenda kujaza kwenye mtihani anafaulu,,,, siyo ajabu kumkuta mwanafunzi mwenye division one haelewi Tenses,,, Sabab Elimu ya Leo imekua Biashara Yani fully kubrashi wanafunzi ile kufuatilia mwanafunzi asome hamna,
Siyo Kama zamani Elimu ilivyo kua inapokelewa na Jamii mtu alimaliza Secondary ana heshima yake akija mtaani unajua kabisa Kuna kitu kipya atatoa kwenye Jamii kuliko Leo mtoto anahitim form 4 akili Bado za kitoto haelewi chochote juu ya Maisha haya Yale masoma ya stadi za kazi hayapo tena Yani Elimu yetu ipo ipo tu ndo maana saivi tunakua na Consumers wengi mtaani hawana wanacho.produce tofouti na kutoa lawama Kila siku
 
Mimi ni kijana wa kiume miaka 27 'nilimaliza Form 4 2013 nikapata division 3 lakini nikakosa nafasi form 5
Since day one ndoto yangu ilikuwa ni kuwa DAKTARI +Business man 2014 nikachomoka Moshi Kuja Dar ku strugle

Nimepambana from 2014 up to this moment MUngu akanibariki kiuchumi kwa kiasi fulan 🙏🙏🙏

Sasa nahisi ni Muda mwafaka wa kutimiza ndoto yangu ya pili japo umri umenitupa mkono

Nimeona Bora nifanye mtihani wa form 5 kama private candidate (PC) kwa combination ya PCB mwakani.

1-Je, wapi naweza Pata center tulivu au mwalimu mzuri wa Physics, Chemistry na Biology ya F5&6?

2-Nitumie trick gani nimudu kusoma sababu ni miaka 10 imepita toka nimeachilia mbali masuala ya shule?
Advance utaenda kupoteza muda tu

Mziki wa kusoma PCB tena nyumbani tena una majukumu Kisha upate division one nzuri (ambayo itakuwezesha kupata chuo Cha udaktari) ni mgumu sana.

Watu wanapata one na wanakosa chuo Cha kusomea MD

Kuna competition kubwa mno katika program za afya na vyuo ni vichache

Njia sahihi kwako hasa ukizingatia umekaa muda mrefu bila kusoma pia una majukumu ni kwenda diploma tu

Sio lazima kusoma degree, hata ukiwa na diploma (clinical officer) ukichanganya biashara zako mambo yataenda.
 
Ok mkuu nikuulize maswali machache....
Kutoka Olevel mpaka advance ulitumia Mda gani kusoma au kuunganisha...
Ulikaa nyumbni kwa muda gani kabla ya kuunga Vamce
Yaani Mimi stori yangu haipashani Sana na ya mtoa Mada

Kwakuwa stori yangu Inasisimua Sana na nahitaji kuja kushare hapa na niandikia Kitabu nitahakikisha Kitabu changu kikiwa tayari na story kuwa tayari ntakutag uje usome .

Ila niseme mtu Kama ana ndoto yoyote anahitaji kuitimiza Basi aweke utayari na kuamini kuwa things are possible

Kiufupi mimi ndo wale vijana waliotoka mtaani kubeba zege na kujichanga taratibu ili kuipata Elimu so from zero to hero Inawezekana .

Yaani unaweza kuwa mbeba zege na ukaamua kuitafuta ndoto ya kuwa daktari , kuwa Mwalimu, mwanasheria au mfanyabiashara mkubwa .

Once I will share my testimony. through this platform.
 
Hongera Sana mkuu sema hii kitu inahitaji Subira na utambuzi wa kiakili
 
Back
Top Bottom