Nina mpango kwenda kutafuta maisha Marekani ila sijui naanzia wapi

Kiasi ganii mkuu? hapo ndio napataka.
Sijajua unaenda state gani ila sidhani kama inaweza kuzidi 2.5m nauli, issue sio nauli issue nikupata iyo visa mkuu. Kupata visa ya usa ni ngumu kama kupata bikra dar labda uende kimasomo au ushinde ile green card lottery au nenda zenji tafuta jimama la kizungu uanzishe nalo mahusiano likufanyie wepesi kwenye visa. All in all hakuna kinacho shindikana chini ya jua ukitia nia, mwenyewe ni ndoto yangu kwenda huko. Anyway am ready to be corrected.
 
Ufafanuzi mzuri sana mkuu hongera! itabidi nifatilie njia ya kwenda kimasomo naona itakua rahisi zaidi.
 
Hii nchi inavijana wengi wasio jielewa sana aiseee....
Watoto wa kuanzia 90's wamekosa ubunifu kabisa....
Nashangaa sana
Wanafikiri ni maisha ni kuhama tu
Biden amefanya yake huko na mpaka wa Mexico anaufunga kabisa ngoja tuone
Tatizo vijana hawa hawana ubunifu wangejifunza kwa vijana wa jirani tu wanavyopambana
 
Hongera kwa kuwa na nia ya kutaka kutoka hapo bongo ulipo, unajua jambo lolote linaanza na idea alafu ndio unakuja kuliweka katika uhalisia, itakuchukua muda au kipindi fulani mpaka wewe kufika huko unakotaka kwenda.

Maana wanasema pay the cost to be the boss. Na kumbuka huwezi itwa boss kama cost yake utailipa
 
Ahsante mkuu muhimu ni uthubutu tu na kuweka malengo basi.
 
Elimu yangu ni diploma ya famasia mkuu lakini nina advanced certificate pia.

Sawa,ila ungekuwa na degree ingekuwa vizuri sana maana huku US waliosoma na wenye elimu za juu ni wengi sana,so competition ni kubwa.Nipo huku mwaka wa nne huu nilikuwa na mpango wa kufungua kasehemu kwa ajili ya chakula so ungekuwa kidogo umegraduate ningekufikiria.
 
Je vipi kujiendeleza kielimu au napo kugumu mkuu.
 
Degree zipo chief, na kama hautafuti a chef necessarily basi tufikirie na wengine mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…