Nina mpango kwenda kutafuta maisha Marekani ila sijui naanzia wapi

Nina mpango kwenda kutafuta maisha Marekani ila sijui naanzia wapi

Wazo zuri. Ushaurii wangu kwako, nenda YouTube anza kufatilia hizi channel
- Denis Magessa

- Dnyota USA


- Hapa Nilipo

Tenga muda wasikilize wote kwa umakini sana. Na ujiongeze pia.
Yangu ni hayo kiongozi
Sawa mkuu nitafatilia nashukuru kwa mchango.
 
Achana na wazo la USA, Huko panataka sana, direct connection kama ni masomo au kazi, or else elimu kubwa ndugu,
Pambana uingie Kwa malkia, hii tafita passport, Mbeleni tafuta hela na visa. Tafuta mshkaji au ndugu, mwambie anakusaidiaje kuzama. Sio mtandaoni, ukipata hivo vtu tajwa, find a known physical person you know, Anaweza kusaidia hata nauli, and all the issues zama UK, kajitafute, zpo kazi nyingi unapita kwa interview ndogo tu.
Kila la kheri, kwa umri wako, achana na marekani, achana na kina dnyota. Wao wenyewe tunawaona hapa wanapiga picha appartments mara wanaimba, tugari wanamiliki tuharrier, tena gari kwa hela za mafara wachache wa bongo wanohaidiwa wanatoa mamilioni na hawaendi popote, jamaa. Anfuga rasta tu zakubond,
Jitafute mwenyewe it is too easy going abroad with personal effort and using your Relatives or friends wanaokufahamu, ziingatia hilo.
Nashukuru kwa mwongozo wako mkuu! inabidi nitanue wigo sasa nione wapi panafaa.
 
Pole sana, sio walioajiliwa wote wana maisha magumu, inategemea umeajiliwa wapi,
Tigo,voda, Helios tower, nssf,tra, TPA(kabla ya DP world), huko ni bata tu.
Nenda Ubalozi wa US omba visa, Ila mchakato ni mrefu, tafuta kazi kwenye taasisi za US, UN, Ulaya, hapa bongo, ni njia rais ya kwenda US, au upate scholarship kwenda US,
Ndio ila vitengo hivyo sio hadi connection ndio upate mchongo hapo.
 
Kwema wakuu! Niende moja kwa moja kwenye mada.

Nimekuwa nikitafakari sana juu ya hatima ya maisha yangu na hasa ukizingatia hali ya sasa kwa hapa Tanzania ni mbaya, kwani watu wanaishi maisha magumu sana, can u imagine mtu ameajiriwa lakini bado analalamika maisha magumu.

Hii inaonesha kwa nchi yetu ajira sio mkombozi wa kukutoa kwenye umasikini bali inakupa nafuu tu. hivyo imenifanya kuwaza zaidi wapi nikatafute maisha ambayo nitaweza kuishi maishi bora kwa maana duniani tunaishi mara moja tu, hivyo sipaswi kuteseka duniani maana ya mbinguni kuna hukumu yake pia.

Kwa kumalizia naomba watu mliowahi kwenda huko mnipe mbinu ya kufika huko majuu, ikiwa pamoja na gharama za nauli, inshort nataka muongozo na kama nijipange niweke akiba ya kiasi ganii hili niweze kutimiza malengo yangu ya kuishi maisha bora kabla sijaondoka duniani.

NB. Umri wangu ni miaka 25.
Siku hizi watu wenye kushiriki mapenzi ya jinsia moja huwa wanapata hifadhi nchi ya marekani na za magharibi, lakini kama haupo kwenye huo mkumbo pambana nyumbani tu hiyo marekani itakuja kwako badala ya kuifuata.
 
Siku hizi watu wenye kushiriki mapenzi ya jinsia moja huwa wanapata hifadhi nchi ya marekani na za magharibi, lakini kama haupo kwenye huo mkumbo pambana nyumbani tu hiyo marekani itakuja kwako badala ya kuifuata.
Ni kweli mkuu tena kwa sasa hali mbaya huko, lakini ngoja nione itakuaje.
 
Kijana inabidi awe na pasipoti ya kusafiria kisha afanye mchakato wa kupata ujuzi wowote mfano udereva wa malori makubwa aongeze na ujuzi wa kutumia mashine za forklift. Kisha kijana inabidi ajifunze lugha angalau kiingereza kwa ufasaha, muhimu zaidi ni awe na fedha angalau 10M. Baada ya hapo kijana aanze utaratibu wa kusaka Visa husika, ila kwa ushauri wangu anaweza anzia nchi tofauti na huko Marekani mfano kule Uarabuni kisha kule ata tengeneza njia ya kuelekea kule anataka.
Uarabuni NO.
 
Sawa,ila ungekuwa na degree ingekuwa vizuri sana maana huku US waliosoma na wenye elimu za juu ni wengi sana,so competition ni kubwa.Nipo huku mwaka wa nne huu nilikuwa na mpango wa kufungua kasehemu kwa ajili ya chakula so ungekuwa kidogo umegraduate ningekufikiria.
Ungemfikiriaje? Ungemuombea work/visa permit au?
 
Back
Top Bottom