Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

Habarini wakuu. Natumaini mnaendelea vizuri na maandalizi ya sikukuu.

Bila kuwachosha sana, nimeweza ku save jumla ya shilingi milioni 64 hadi sasa, kiasi hiki nimeweza kukisave kuanzia mwezi April mwaka huu kutoka kwenye mshahara wangu. Nipo mkoa wa Dodoma.

So far, nimefikiria kuwekeza katika mojawapo ya mambo yafuatayo:

1. Ninunue eneo la shamba kubwa maeneo ya Dodoma nje ya mji au Dodoma vijijini kisha nianzishe kama ranchi hivi ya ufugaji wa mbuzi.

Nimefikiria mbuzi kwa sababu kwa utafiti wangu wa muda mfupi nimeona kuwa mbuzi hawana complications nyingi kulinganisha na wanyama wengine wa kufuga, na pia kuna fursa zaidi kwa mbuzi nchini, na demand ambayo haijawa satsified.

Lengo la hii ni baadae niweze kuwa na kiwanda kabisa cha kuchinja na kuprocess nyama ya mbuzi, na kuweza hata kuuza ndani na nje ya nchi products za nyama ya mbuzi.

2. Nifungue park kwa ajili ya michezo ya watoto kwa Dodoma. Moja ya gaps ambazo nimeziona Dodoma ni kukosekana kwa eneo zuri la maana kwa ajili ya michezo ya watoto na watu kupumzika pia.

Hapa nafikiria ninunue eneo Dodoma then nilitengeneze vizuri na kuweka michezo ya watoto (indoor na outdoor) ya kutosha, pamoja na kutengeneza garden nzuri ya kuvutia kwa ajili ya watu na familia zao kupumzika na kupigia picha.

Kwa nje kwenye ukuta nawaza pia kuwe na frame kadhaa ambazo nitakodisha kwa watu waweke maduka ya vyakula, vinywaji, na vitu vya watoto.

3. Nifungue kiwanda cha maji ya kunywa yale ya kwenye dispenser kwa ajili ya matumizi ya majumbani na maofisini. Nimeona gap pia hapa kwa sababu makampuni yaliyopo hapa Dodoma kwa hii huduma hayatoshelezi mahitaji kwa kiasi kikubwa, mara nyingi sana unakuta yanapotea sokoni kwa muda fulani (no consistency of supply).

4. Ninunue kiwanja saizi ya kati maeneo ambayo sasa hivi ndo yanajengeka (eg Ilazo, NALA) halafu nipige vyumba vya low-cost (behewa style), niweke hapo vyumba kadhaa, then nipangishe nile kodi kila mwezi hata 50K kwa kila room. Baadae kadri ninavyopata mpunga zaidi, niongeze idadi ya vyumba zaidi na zaidi.

Wenye uzoefu wa biashara na ideas na mnaoifahamu Dodoma, niambieni hapo nianze na ipi kati ya hizo kwa mtaji huu nilionao (milioni 64), au hata idea nyingine ambayo sijaitaja hapo juu.

Mimi maisha yangu yote nimeajiriwa tu hadi sasa (nina umri wa miaka 35). Sijawahi kufanya buashara hata ya kuingiza shs 500. Nimeona ni bora pia niangalie upande huu wa business pia maana siwezi ajiriwa milele, na pia kama mjuavyo hizi ajira zetu, leo ipo kesho haipo hasa huku private sector.

Natanguliza shukrani.
Cryptocurrency
 
Hakuna biashara nnaiamini kama ya real estate. Nyumba ni asset ambayo haitokuja ku depreciate value. So hata ukijenga ukapangisha all is well.
Kwa maelezo ya mtoa mada biashara inayomfaa na rahisi kwake ni real estate tu maana hana uzoefu wa biashara na pili muda wake ni mchache kutokana na majukumu ya ajira yake.
Yaani akigusa tu biashara zingine kaumia
 
Mawazo yote yaliyotolewa ni mazuri
Ila Kuna wazo Moja nakushauri na hakikisha unalifanyia kazi,hata kama Kwa mtaji mdogo.
Fanya biashara ya NAFAKA,Fanya utafiti uone nafaka zipi dodoma zinauzika sana,na uhitaji ni mkubwa.
Jikite hapo mkuu,Utakuja kunishukuru baadae.

NAFAKA,NAFAKA,NAFAKA..mengine utafanya baadae, baada ya hiyo biashara kusimama.

Dm Kwa ushauri zaidi kuhusu biashara ya NAFAKA na....
Hili pia ni wazo bora ambalo lilisahaulika.
Yaani ukiachana na biashara ya real estate hii ni biashara namba 2 yenye faida kubwa na risk yake ni ndogo.
 
Hongera sana kwanza kwa kukusanya hiyo 65m. Ushauri wangu kwanza achana na wazo la ku invest Dodoma.

Nenda Dar chukua viwanja viwili maeneo ya Goba au madale jenga apartment zako mbili hata za vyumba vitatu vitatu. Trust me unakula hela ukiwa umekaa.

Shida ya hizi investment zingine inabidi ukimbizane sana lkn investment ya nyumba ukishamaliza ujenzi hela inakukuta umekaa.
[emoji123][emoji1306]
 
Ushauri wa bure...anza lodge vyumba 10.....au 15 ukiweza hela kila siku ina nguvu sana sana x 100....baada mwaka utaamua kuongeza au kwenda michezo watoto ....nzuri bila pressure! Baadae sana nenda vijumba kupangisha.....baada miaka 5 utatoa mrejesho.....Tafuta eneo zuri....!! Ongeza pesa kidogo ajili finishing .......all the best
Milioni 64 inajenga vyumba 4 tu,hiyo ya vyumba 10 hela haiwezi kutosha
 
Mkuu kuhusu hiyo ya mbuzi kwa kweli inalipa
Kuna jamaa alikuwa diaspora wa usa amerudi home Uganda kanunua eneo kubwa sana nje ya Kampala kama 70 miles

Jamaa kwa sasa yuko mbali namfuatilia sana kwenye account yao ya Instagram
Nilikuwa nahitaji mbuzi wale wakubwa wanaofika mpaka kilo 100 wanaoitwa Boer toka SA

Kwa sasa anao ndio nawafuatilia ila mpaka niende mwenyewe
Kwa sisi bado sana ufugaji kuliko wenzetu

Unaweza kujifunza kitu kwake
View attachment 2456407
Kuna rafiki yangu Mganda jana nilikuwa naongea naye akanisimulia hii stori ya huyu jamaa.
Amefikiria nje ya box
 
Habarini wakuu. Natumaini mnaendelea vizuri na maandalizi ya sikukuu.

Bila kuwachosha sana, nimeweza ku save jumla ya shilingi milioni 64 hadi sasa, kiasi hiki nimeweza kukisave kuanzia mwezi April mwaka huu kutoka kwenye mshahara wangu. Nipo mkoa wa Dodoma.

So far, nimefikiria kuwekeza katika mojawapo ya mambo yafuatayo:

1. Ninunue eneo la shamba kubwa maeneo ya Dodoma nje ya mji au Dodoma vijijini kisha nianzishe kama ranchi hivi ya ufugaji wa mbuzi.

Nimefikiria mbuzi kwa sababu kwa utafiti wangu wa muda mfupi nimeona kuwa mbuzi hawana complications nyingi kulinganisha na wanyama wengine wa kufuga, na pia kuna fursa zaidi kwa mbuzi nchini, na demand ambayo haijawa satsified.

Lengo la hii ni baadae niweze kuwa na kiwanda kabisa cha kuchinja na kuprocess nyama ya mbuzi, na kuweza hata kuuza ndani na nje ya nchi products za nyama ya mbuzi.

2. Nifungue park kwa ajili ya michezo ya watoto kwa Dodoma. Moja ya gaps ambazo nimeziona Dodoma ni kukosekana kwa eneo zuri la maana kwa ajili ya michezo ya watoto na watu kupumzika pia.

Hapa nafikiria ninunue eneo Dodoma then nilitengeneze vizuri na kuweka michezo ya watoto (indoor na outdoor) ya kutosha, pamoja na kutengeneza garden nzuri ya kuvutia kwa ajili ya watu na familia zao kupumzika na kupigia picha.

Kwa nje kwenye ukuta nawaza pia kuwe na frame kadhaa ambazo nitakodisha kwa watu waweke maduka ya vyakula, vinywaji, na vitu vya watoto.

3. Nifungue kiwanda cha maji ya kunywa yale ya kwenye dispenser kwa ajili ya matumizi ya majumbani na maofisini. Nimeona gap pia hapa kwa sababu makampuni yaliyopo hapa Dodoma kwa hii huduma hayatoshelezi mahitaji kwa kiasi kikubwa, mara nyingi sana unakuta yanapotea sokoni kwa muda fulani (no consistency of supply).

4. Ninunue kiwanja saizi ya kati maeneo ambayo sasa hivi ndo yanajengeka (eg Ilazo, NALA) halafu nipige vyumba vya low-cost (behewa style), niweke hapo vyumba kadhaa, then nipangishe nile kodi kila mwezi hata 50K kwa kila room. Baadae kadri ninavyopata mpunga zaidi, niongeze idadi ya vyumba zaidi na zaidi.

Wenye uzoefu wa biashara na ideas na mnaoifahamu Dodoma, niambieni hapo nianze na ipi kati ya hizo kwa mtaji huu nilionao (milioni 64), au hata idea nyingine ambayo sijaitaja hapo juu.

Mimi maisha yangu yote nimeajiriwa tu hadi sasa (nina umri wa miaka 35). Sijawahi kufanya buashara hata ya kuingiza shs 500. Nimeona ni bora pia niangalie upande huu wa business pia maana siwezi ajiriwa milele, na pia kama mjuavyo hizi ajira zetu, leo ipo kesho haipo hasa huku private sector.

Natanguliza shukrani.

Si bora ungeendelea kusave tuu.Naona kama hiyo inalipa zaidi ya biashara.kama ndani ya miezi 8 umesave 64m
 
Jenga Lodge!!! Hyo hela inatosha Sana,Tena hata lodge mbili,ulifanya hivyo matunda utayaona mapema sana
BIG NO, ni biashara inayofifishwa na ushindani na mabadiliko ya kiushindani. Lakini pia inahitaji management yenye ubunifu na utulivu. Lakini pia sioni kama lodge itampeleka kwenye lengo lake. It's too general busines (kwa mimi navyoona).
 
Binafsi naona fanyia kazi wazo la kwanza. Cha muhimu pata eneo kubwa kiasi acre 100-200, chimba visima uwe na uhakika wa maji (anza hata na kimoja), jenga mabanda vizuri.

Katika hilo eneo, baadaye unaweza kuongeza na option za kuweka mabwawa ya samaki (pia demand yake kwa Dodoma itakuwa kubwa tu. Above all. GOOD MANAGEMENT. Ikibidi jenga ofisi yako yenye full furnished utakayomuweka mtu professional na ww kuwa mgeni wao kila Ijumaa.
 
Si bora ungeendelea kusave tuu.Naona kama hiyo inalipa zaidi ya biashara.kama ndani ya miezi 8 umesave 64m
Nasave hadi lini mkuu? Nature hya kazi ninazofanya ni za miradi ya miaka 5-7. Hapa nilipo mradi unaisha 2026, from there kinachofuata ni majaliwa, either niwahi kutoka kabla mradi haujaisha au nibahatike kupata mradi mwingine huu unapoisha.

Sasa hata nikifanikiwa maisha hayo hadi lini? Way forward ni lazima nianzishe kitu changu cha kunitengenezea pesa nje ya ajira, hilo halikwepeki mkuu hata nikisave vipi..!!

Hatua ya kusave inaenda vizuri hadi sasa, ila sasa hatua inayofuata ni lazima ni invest kuzalisha hii pesa mkuu!! Yaani hiki kitu kinaninyima usingizi daily nakaa nawaza hata hadi saa kumi alfajiri mara nyingi tu, wife anashtuka mara nyingi ananikuta niko awake anashangaa vipi wewe mbona hulali...?

Kusave peke yake hakusaidii mkuu, ni lazima ni invest!!
 
Binafsi naona fanyia kazi wazo la kwanza. Cha muhimu pata eneo kubwa kiasi acre 100-200, chimba visima uwe na uhakika wa maji (anza hata na kimoja), jenga mabanda vizuri. Katika hilo eneo, baadaye unaweza kuongeza na option za kuweka mabwawa ya samaki (pia demand yake kwa Dodoma itakuwa kubwa tu. Above all. GOOD MANAGEMENT. Ikibidi jenga ofisi yako yenye full furnished utakayomuweka mtu professional na ww kuwa mgeni wao kila Ijumaa.
Asante sana mkuu, umeiweka vizuri sana. Hilo wazo la kwanza, ulichokizungumza kwenye hii comment yako ndo vision ambayo niko nayo, hii kitu imenivutia sanaaa!!
 
Kuna rafiki yangu Mganda jana nilikuwa naongea naye akanisimulia hii stori ya huyu jamaa.
Amefikiria nje ya box
Nimecheki jamaa video zake kwa Youtube channel yake, jamaa yuko njema aisee. Ila alianza na mtaji wa kutosha pia, na alikua na vision kubwa. Ameni inspire sana.
 
Kwa maelezo ya mtoa mada biashara inayomfaa na rahisi kwake ni real estate tu maana hana uzoefu wa biashara na pili muda wake ni mchache kutokana na majukumu ya ajira yake.
Yaani akigusa tu biashara zingine kaumia
Kweli mkuu. Mimi napenda sana kuwashauri watu wengi kuhusu kuwekeza kwenye ardhi. Swala la atapata wapi eneo zuri ni akili ya mnunuaji na umakini. Ila land is everything kwenye investment.
 
Hii kibongo bongo ambapo uaminifu ni F, na watu wanacheza sana na vitabu vya biashara anaweza akawa anaripoti TRA kila mwaka hasara wakati in fact anatengeneza hela, naweza ishia kupata hasara na kugombana na watu juu.
Bongo apa zipo kampuni nyingi sana zipo ki ushirika but taswira ya nje tunaona kama ya mtu fulani…kumbe ndani yake kuna mikono mingi ya watu…

Kwenye makampuni mengi kuna kuwa na wahasibu ambao kazi yao kulinda maslahi ya washirika….

Kuhusu TRA ni issue ya serikali….haiusiani na ushirika.
 
Back
Top Bottom