Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

Dooooohhhh...!! Balaa.
Asante kwa angalizo mkuu
 
Kwanza nikupe hongera mkuu kwa kuweza kukusanya mtaji, Mimi nitakushauri mambo machache ya kufanya

1. Kwa kuwa hujawahi kufanya biashara yoyote ile , Ili kuepuka kupoteza mtaji fanya biashara ambayo haita risk mtaji wako kwa kipindi Cha miezi isiyopungua 6 Ili kupata uzoefu wa hesabu za mapato na matumizi yatokanayo na biashara, mfano anzisha tu kagoli ka tigopesa au uwakala wa bank ( kuwa makini na eneo utakalochagua) hapa test tu na mtaji wa 4m lengo ni kuzoea biashara na namna hesabu zinavoenda huku mtaji wako ukiwa salama



2. Option nyingine wekeza kwenye real estate ( tafuta maeneo yenye potential kwa baadae mfano maeneo ambayo lami itapita siku za usoni tafuta hata heka kadhaa za karibu na barabara kisha tulia zako ( kuwa makini na road reserve), lami ikipita hayo maeneo yatapanda almost mara 4 au tano ya bei uliyonunulia, Kuna maeneo jamaa alinunua eka kwa 250k saivi wadau wanapataka kwa milion 8 na jamaa hataki kuuza


3. Usiingie kwenye kilimo,ufugaji, uchimbaji, au ujenzi huko utapoteza pesa (kama interest yako Ipo kwenye kilimo, au ufugaji hakikisha unatumia faida itakayopatikana ) hivi vitu hupotezaga pesa ndani ya sekunde

4. Kuna nyuzi zangu mbili niliziandika siku za nyuma nikitaka partner mwenye mtaji wa around 3m to 6m na ni 0 risk ukiwa tayari zipitie tunaweza fanya kitu kwa mtaji wa million 6 tu

Hongera
 
Asante mkuu, nitaingia field kwa utafiti, maana mimi pia sina taarifa za kutosha kuhusiana na biashara ya lodge.
Taratibu za lodge wala si ngumu na unaweza kuzimudu hakika..

Mfano:
1: Ramani ya nyumba yenye vyumba sita au Name kwa mfumo wa apartment hii inaleta muonekano kama motel hivi.

2: Fence kali ya kuvutia na mapambo ya miti natural plants with surrounded cctv cameras hadi hapo reception na lazima uchimbe kisima cha maji au ikiwa supply ya maji ya dawasco ipo sawa unachimba kile kisima cha uhifadhi maji pamoja na tanks kadhaa juu ya Hilo Shimo unajenga kwa mfumo wa kajumba au chumba chenye andaki hipa ndio pataonekana kama sehemu ya mapokezi mtu akiingia getini pia unaweza ukadizaini kama counter flani ya vinywa ukauza kwa wateja.

3: Kuhusu furniture unaweka zile zenye hali tofauti ili ikurahisishie kwenye kupanga bei na kuweza kupanga bajeti yako ya uendeashaji kwa urahisi kwa maana ya matumizi ya kila siku wakati wakazi za wahudumu na mishahara.

3: Jitahidi kuweka paking nzuri na isiyo ya kubana ili kuepusha misongamano ya magari bila kusahau kasehemu kapembeni kwa ajili ya mapunziko na mazungumzo kwa wateja wasafiri na hata watalii pia.

4: Kiwanja hapa kwenye hili nakushauri zingatia vile vilivyopo kwenye mazingira ya watu ili kuvutia wateja kwa wingi na usalama zaidi kwakua haitakuwa na mushikeri za uvamizi kwa wageni ila ujitahidi kuweka ukaribu na askari ili linapotokea tatizo kwako iwerahisi kuliweka sawa na kuendelea na biashara na hii ni msaada hata kwenye matukio mengine kadhaa yanayotokea nyakati za biashara.
 
Tafuta eneo weka guest house hata room chache za kuanzia kwa uko ulpo man utakuwa unaongezea kadiri siku ziendavo. Man hiyo hainaga mlolongo ni fulu fedha. Ila codes za kazi unapaswa kuzijua
Cheki wazo la huyu mdau Naona limo konki pia mno. Ujue biashara Ni eneo, mtaji na msimamizi. Eneo Ni market. Hasahasa msimamizi ndio kila kitu. Sasa wewe upo jobu kaloji kwenye mikoa ambayo Ni municipal like Mpanda. Unakomaa hata na self tano room za Mana. Nadhani kila room unaweka 10-15/20 hukosi milioni kwa mwezi.

Loji iko POA pia uangalizi wake Ni kamera. Chumba Cha show time kuwepo, uza na gandomu ikiwezekana weka dada mzuri mweupe mwenye nyamanyama na sio kimbaumbau, yaani ambaye anafanya mtu anaenda kualalapo.
 
Mkuu mm ni jobless ili jarbu huku

1.biashara ya nafaka hapo Dodoma alizeti (hao unaweza kununua na mashine ya kukamulia ukapata mafuta na Mashudu utatauza kama chakula cha mifugo), karanga,mahindi na ufuta ukiwa na center unayafata mazao hukohuko shambani...

2.nenda sehemu inaitwa Mvumi misheni kule kuna hospitali ya macho kumechangamka sana umeme umefika kafungue phamacy kubwa ya kisasa ifanye kazi 24hrs

3.kaweke mashine ya kusaga na kukoboa hukosi 60k kwa siku kijiji cha Mvumi makulu (kwa kina palamagamba kabudi) na hata Mvumi misheni

4.hii acha nibaki nayo

5.Hii pia acha nibaki nayo
 
Acha utapeli
 
Asante sana kwa mawazo kuntu mkuu. Nimependa sana reasoning ya ushauri no 1. Nazicheki hizo nyuzi zako.
 
Hakuna biashara nnaiamini kama ya real estate. Nyumba ni asset ambayo haitokuja ku depreciate value. So hata ukijenga ukapangisha all is well.

Tatizo la nyumba unazika pesa na faida inakuja kuonekana baada ya miaka mpka 7,8 na kuendelea mbele hapo unadhani kibongobongo hiyo ni hasara chukulia nyumba ya M50 kali unapangisha 500k kwa mwenzi hapo Ela inarudi baada ya miaka 9 hapo ikiwa imepangishwa non stop na kitu ambacho hakiwezekani pia kodi nimechukulia kodi ya 500k ambayo ni kubwa ila kikawaida ni 200k mpka 300k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…