Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

Kama hujui cha kuwekeza usiwekeze. Ni suala la muda tu, hiyo hela itapotea due to lack of Education and experience. Merry Christmas.
 
Kwa mshahara wako wekeza kwenye real estate!! Dodoma nyumba za kupanga anahama mtu saa 6 kamili then anahamia mwingine saa 6:05!! Jaribu kutafuta maeneo ya chuo haswaa ndo kuna hela!
Hahahaha!! Asante sana mkuu kwa ushauri
 
Kama hujui cha kuwekeza usiwekeze. Ni suala la muda tu, hiyo hela itapotea due to lack of Education and experience. Merry Christmas.
Kwa hiyo zikae tu benki hadi lini? Nimetaja hizo ideas nne ambazo nazifikiria. Any thoughts?
 
Umasikini ni mbaya sana kila unacho ambiwa utaona ni chai, muhimu tuendelee kupambana.

Mkuu jaribu kupitia mawazo ya wadau ambayo wanakushauri ufanye, wazo utakalo liko poa basi liendee kwa haraka zaidi.

Mkuu binafsi yangu napenda nikuongezee mawazo mawili kama ikikupendeza unaweza chagua moja ama ukafanya yote mawili. Kuna mdau hapo juu ame kushauri ufungue duka la dawa za binadamu na uzuri zaidi amekutajia mpaka location, hii kitu iko poa sana. Sasa wewe ifanye kwa ukubwa zaidi fungua na maabara kabisa, mtu anapima na kupewa dawa hapo hapo. Hii kitu inalipa sana, kwa kuwa umeajiliwa muweke mkeo asimamie shoo.

Fungua duka la pembejeo za kilimo na dawa za mifugo, tafuta location kisha weka hii kitu. Ndani ya mwaka rudi kutoa ushuhuda wako.

Mkuu kila la kheri.

 
Fact
 
Asante sana mkuu kwa ushauri mzuri
 
Mi mwnyw namshaur labda angekopa thn aongezee ndo ajenge lodge kali
Sio muumini sana wa kukopa kibiashara mkuu, hasa ukizingatia kuwa bado sijawahi kufanya biashara hata ya shs 100, hivyo nina wasiwasi sana kusema nichukue mkopo then niuweke kwenye biashara mpya.

Kama hela inahitajika kuongezwa, nina uwezo wa kuset aside hadi 8 milioni kila mwezi na kukamilisha ujenzi wa hizo lodge baada ya kipindi cha miezi kadhaa.
Lakini asante sana kwa ushauri wako, naweza kuuchukua with some modifications.
 
Hahahaha...!! Kila biashara inshitaji utafiti mkuu.
Analysis paralysis😂😂
Yeah, mnakaa kuchambua na ku 'analaizi' tu bila kufanya vitendo, matokeo yake mnakwama kwenye ku analyse tu mnakuwa kama mmepalalaizi.

Unachotakiwa ni kucalculate risk iliyopo, kama inahimilika unafanya utekelezaji bila kusita. Changamoto zingine utazikuta humohumo na utatafuta namna ya kuzitatua ukiwa tayari kwenye biashara.
 
Mkuu unalipwa kiasi gani hadi uweze kisave M64 tena kuanzia April tu apo hii itakuwa chai ☕️
Naheshimu mawazo yako pia. Endelea kuamini hivyo hivyo tu, wala haina shida. Nina uwezo wa ku save 8milion kila mwezi, ambayo ni 2/3 ya my net-income.
 
Ni kweli kabisa mkuu, nakubaliana na wewe 100%.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…