Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

Production ndio kila kitu. Kwa hiyo wazo la mbuzi ni zuri. Retail haina maana yoyote. Halafu retail is highly taxed in any country kuliko production.
Asante sana mkuu kwa hii insight, nitai consider sana wakati nafanya maamuzi.
 
Ngoja nkuambie, sijui km umeshaambiwa..kimbia haraka na 50m kawekeze UTT ama zile Bonds za serikali utanishukuru.

hyo ingine chagua wazo moja hapo lisilo na mtaji mkubwa na anza na 5m. Tuliza akili yako kabisa.
Asante sana kwa wazo mkuu..!!
 
Ni 64m mkuu, sio 63m.
Mshahara wangu kwa mwezi ni 14m, pamoja na marupurupu mengine mengi tu. Kuna uzi kwenye stories of change nimeelezea kwa kirefu nikiwezaje kufikia kulipwa mshahara huo. Kwa wastani na save kila mwezi milioni 8 kupitia akaunti ya malengo. Nimejiwekea nidhamu kubwa sana ya kusave ambapo na save karibu 2/3 ya net-income yangu kila mwezi.
Tanzania hii hii? Mshahara 14m per month? Au ni Ubunge! Au ulipata contract kutoka nje ya nchi? Hongera sana lakini, maana ni wachache mno tena mno wanapata mshahara zaidi ya milion 6 kwa mwezi kwa Tanzania yetu
 
Hili pia ni wazo bora ambalo lilisahaulika.
Yaani ukiachana na biashara ya real estate hii ni biashara namba 2 yenye faida kubwa na risk yake ni ndogo.
Mazao yanashuruba Sana unatakiwa ingie kijijini mwenyewe ukakutane na vijana uwape hela ukusanye mzigo kwa haraka

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Habarini wakuu. Natumaini mnaendelea vizuri na maandalizi ya sikukuu.

Bila kuwachosha sana, nimeweza ku save jumla ya shilingi milioni 64 hadi sasa, kiasi hiki nimeweza kukisave kuanzia mwezi April mwaka huu kutoka kwenye mshahara wangu. Nipo mkoa wa Dodoma.

So far, nimefikiria kuwekeza katika mojawapo ya mambo yafuatayo:

1. Ninunue eneo la shamba kubwa maeneo ya Dodoma nje ya mji au Dodoma vijijini kisha nianzishe kama ranchi hivi ya ufugaji wa mbuzi.

Nimefikiria mbuzi kwa sababu kwa utafiti wangu wa muda mfupi nimeona kuwa mbuzi hawana complications nyingi kulinganisha na wanyama wengine wa kufuga, na pia kuna fursa zaidi kwa mbuzi nchini, na demand ambayo haijawa satsified.

Lengo la hii ni baadae niweze kuwa na kiwanda kabisa cha kuchinja na kuprocess nyama ya mbuzi, na kuweza hata kuuza ndani na nje ya nchi products za nyama ya mbuzi.

2. Nifungue park kwa ajili ya michezo ya watoto kwa Dodoma. Moja ya gaps ambazo nimeziona Dodoma ni kukosekana kwa eneo zuri la maana kwa ajili ya michezo ya watoto na watu kupumzika pia.

Hapa nafikiria ninunue eneo Dodoma then nilitengeneze vizuri na kuweka michezo ya watoto (indoor na outdoor) ya kutosha, pamoja na kutengeneza garden nzuri ya kuvutia kwa ajili ya watu na familia zao kupumzika na kupigia picha.

Kwa nje kwenye ukuta nawaza pia kuwe na frame kadhaa ambazo nitakodisha kwa watu waweke maduka ya vyakula, vinywaji, na vitu vya watoto.

3. Nifungue kiwanda cha maji ya kunywa yale ya kwenye dispenser kwa ajili ya matumizi ya majumbani na maofisini. Nimeona gap pia hapa kwa sababu makampuni yaliyopo hapa Dodoma kwa hii huduma hayatoshelezi mahitaji kwa kiasi kikubwa, mara nyingi sana unakuta yanapotea sokoni kwa muda fulani (no consistency of supply).

4. Ninunue kiwanja saizi ya kati maeneo ambayo sasa hivi ndo yanajengeka (eg Ilazo, NALA) halafu nipige vyumba vya low-cost (behewa style), niweke hapo vyumba kadhaa, then nipangishe nile kodi kila mwezi hata 50K kwa kila room. Baadae kadri ninavyopata mpunga zaidi, niongeze idadi ya vyumba zaidi na zaidi.

Wenye uzoefu wa biashara na ideas na mnaoifahamu Dodoma, niambieni hapo nianze na ipi kati ya hizo kwa mtaji huu nilionao (milioni 64), au hata idea nyingine ambayo sijaitaja hapo juu.

Mimi maisha yangu yote nimeajiriwa tu hadi sasa (nina umri wa miaka 35). Sijawahi kufanya buashara hata ya kuingiza shs 500. Nimeona ni bora pia niangalie upande huu wa business pia maana siwezi ajiriwa milele, na pia kama mjuavyo hizi ajira zetu, leo ipo kesho haipo hasa huku private sector.

Natanguliza shukrani.
Kuna vingi hujasema hivyo hatuwezi kukushauri precisely.....

Unataka independent business venture will GUARANTEED income ... low/minimum Supervision?

High risk with high return required maximum/medium Supervision?

your specialty...

Areas of interest

Service, merchandise or manufacturing...?
 
Hii biashara ya lodge ni nzuri sana na inalipa vizuri kweli hata mimi nashauri hili ingawa sina taarifa sahihi ya bei za viwanja huko lkn kwenye hayo maeneo tajwa na mwandishi anaweza kuangalia ni wapi kumechangamka na kuanza na lodge moja kali ya kisasa na ikamlipa vizuri sana kisha baada ya miaka mitatu akafuangua park kali sana hadi ukashangaa..
Lodge gani ya mil.64? Labda Mara 2 yake
 
Ushauri wa bure...anza lodge vyumba 10.....au 15 ukiweza hela kila siku ina nguvu sana sana x 100....baada mwaka utaamua kuongeza au kwenda michezo watoto ....nzuri bila pressure! Baadae sana nenda vijumba kupangisha.....baada miaka 5 utatoa mrejesho.....Tafuta eneo zuri....!! Ongeza pesa kidogo ajili finishing .......all the best
Kwa Pesa gani ya lodge? Labda guest bubu
 
Mkuu kuhusu hiyo ya mbuzi kwa kweli inalipa
Kuna jamaa alikuwa diaspora wa usa amerudi home Uganda kanunua eneo kubwa sana nje ya Kampala kama 70 miles

Jamaa kwa sasa yuko mbali namfuatilia sana kwenye account yao ya Instagram
Nilikuwa nahitaji mbuzi wale wakubwa wanaofika mpaka kilo 100 wanaoitwa Boer toka SA

Kwa sasa anao ndio nawafuatilia ila mpaka niende mwenyewe
Kwa sisi bado sana ufugaji kuliko wenzetu

Unaweza kujifunza kitu kwake
View attachment 2456407
Mwakani inshaalah nitanunua ekari walau 3 kwa ajili ya kazi hii ya ufugaji
 
Kushauriwa ni Bure kuchukua au kuacha ni maamuzi binafsi.

Biashara ya Kukodisha Vitu

TV size KUBWA

Nunua Tv size kubwa kuanzia 65inch na 75 uwe nazo hata 11

65inch inauzwa 1.9m x 4 = 7,600,000

75inch 2.8m x 6 = 16,800,000

85inch 6.5m x 1 = 6,500,000

TOTAL : 30,900,000

Bei za Kukodisha TV kwa Event

65inch 100,000 per day
75inch 150,000 per day
85inch 200,000 per day

Kwa siku 65inch zikitoka zote = 400,000

75inch = 900,000

85inch = 200,000

Total per day = 1,500,000 per day

Kumbuka TV ulitumia mtaji wa 30,900,000 kwenye ule mtaji wako utakua umebaki na 33,100,000.

Hiii utaipunguza kidogo kununulia Standa za TV zako ambazo

Stand 1 ina cost 350,000 x 11 = 3,850,000

kwenye 33,100,000 - 3,850,000 = 29,250,000

Kuna Nyaya za kununua extension na vikorokoro vingine weka 1.25m utabaki na 28m.

Usafiri,na hidden cost ambazo hatujaweka Weka 1m.

Mfukoni utabaki na 27m (huu ni mtaji wa biashara ingine)

Kwahyo kwa biashara yako hiyo ya TV una uwezo wa kupiga pesa zaidi ya 10m kwa mwezi.

TV zitakua busy Alhamis,ijumaa,jmos na Jpli siku 4 ambapo kwa siku 4 utakusanya 6m.

ukipiga 6m kwa wiki 4 upate mwezi = 24,000,000 income ya mwezi mmoja.

Kwa miezi yako 6 tu,income utayokua umeipata Calculate mwenyewe.

Hii ninBiashara 1 unaipga huku huna stress umejificha zako ndani unaendelea kula Korosho unazitupia mdomoni moja moja tu. (watu wanaendelea kukuita muuza madawa ya kulevya)

Hii Clip Hapa chini ni 1 ya kati ya zile zinazoendelea kupiga kazi niliyoiongeza...

View attachment 2456518

Nakuja na idea nyingine ya ile hela ilobaki, ngoja niangalie kati ya ninazofanya ipi itakufaaa..
Kwamba Kuna watu wanakodi tv kwa ajili ya kuangalia mpira au Nini hasa? Maana Mimi niliko.sijawahi ona kitu Kama hiyo.
 
Kwamba Kuna watu wanakodi tv kwa ajili ya kuangalia mpira au Nini hasa? Maana Mimi niliko.sijawahi ona kitu Kama hiyo.
Tv huwa zinakodishwa kwenye kumbi za sherehe au yale matukio makubwa yanayojumuisha watu wengi kwenye kumbi maalumu. Kwa hapa mjini watu ambao wanafanya kazi za kurekodi video kwenye matukio huwa wanakodi hivyo vifaa.
 
Back
Top Bottom