Mkuu mi navyoona we bado haupo tayari na hata hiyo barua ulipeleka kwa shinikizo tu na ndo ulipoharibu. Ulitakiwa toka mwanzo uwaambie haupo tayari huyo Binti aendelee na mishe zake.
Kwa sababu kuvunja uchumba ni heri kuliko kuvundoa,bora umwache huyo binti awe huru. Wewe bado haupo tayari na kutokuwa tayari si dhambi. Mimi binafsi nishajifunza,kama moyo wangu unasita kufanya jambo hata kama linaonekana zuri kiasi gani,silifanyi. Na wewe kwa sababu moyo wako unasita sikushauri uliendee hilo jambo la ndoa.
Pia,mbona huyo binti bado mdogo sana mkuu, miaka 17? huo umri kumleta binti mjini akutane na wenye mji wao utalizwa mkuu,binti angalau awe na miaka 20. Miaka 17 hata akishika ujauzito manesi wataenda kumtukana na kukutukana wewe,huo umri bado jamani.
Mwisho,muoaji ni wewe,usifanye jambo la ndoa kwa shinikizo lolote. Najua familia zetu lazima waongee lakini ukijenga ndoa kwenye msingi wa kufurahisha familia,utaishia mateso maana itakuwa haujaoa kwa ajili yako bali kwa ajili yao,maisha yenyewe mafupi haya.