Nina wasiwasi na hii ndoa yangu. Nifanyeje?

Nina wasiwasi na hii ndoa yangu. Nifanyeje?

Mkuu mi navyoona we bado haupo tayari na hata hiyo barua ulipeleka kwa shinikizo tu na ndo ulipoharibu. Ulitakiwa toka mwanzo uwaambie haupo tayari huyo Binti aendelee na mishe zake.
Kwa sababu kuvunja uchumba ni heri kuliko kuvundoa,bora umwache huyo binti awe huru. Wewe bado haupo tayari na kutokuwa tayari si dhambi. Mimi binafsi nishajifunza,kama moyo wangu unasita kufanya jambo hata kama linaonekana zuri kiasi gani,silifanyi. Na wewe kwa sababu moyo wako unasita sikushauri uliendee hilo jambo la ndoa.
Pia,mbona huyo binti bado mdogo sana mkuu, miaka 17? huo umri kumleta binti mjini akutane na wenye mji wao utalizwa mkuu,binti angalau awe na miaka 20. Miaka 17 hata akishika ujauzito manesi wataenda kumtukana na kukutukana wewe,huo umri bado jamani.
Mwisho,muoaji ni wewe,usifanye jambo la ndoa kwa shinikizo lolote. Najua familia zetu lazima waongee lakini ukijenga ndoa kwenye msingi wa kufurahisha familia,utaishia mateso maana itakuwa haujaoa kwa ajili yako bali kwa ajili yao,maisha yenyewe mafupi haya.
Asante mkuu Kwa mawazo yako
 
Kwa story yako mbona kama wazazi wa binti ndio wanapush ajenda aisee.

Wanataka kutua mzigo gani?

Vipi mmepima afya?
Umefatilia historia yake na familia yake?
Vipi mahusiano ya familia yako na yake yakoje?

Weka ndani umpime, taraka zipo kiongozi, usijipe stress bure.
 
K
Kwa story yako mbona kama wazazi wa binti ndio wanapush ajenda aisee.

Wanataka kutua mzigo gani?

Vipi mmepima afya?
Umefatilia historia yake na familia yake?
Vipi mahusiano ya familia yako na yake yakoje?

Weka ndani umpime, taraka zipo kiongozi, usijipe stress bure.
Kwasas tupo iyo stage ya kupima
 
Fam
Kwa story yako mbona kama wazazi wa binti ndio wanapush ajenda aisee.

Wanataka kutua mzigo gani?

Vipi mmepima afya?
Umefatilia historia yake na familia yake?
Vipi mahusiano ya familia yako na yake yakoje?

Weka ndani umpime, taraka zipo kiongozi, usijipe stress
Familiar zana undugu ingawa ni wa mbali ila upo mkuu
 
K

Kwasas tupo iyo stage ya kupima
Kama una uwezo wa kuoa we oa tu, maana hapo kiukweli hoja huna ni hisia zako tu na huna ushahidi wowote wa kumtia binti wa watu hatiani.

Vipi ni bikra??
 
Habarini wakubwa,

Poleni na majukumu. Nianze kwa kuomba radhi kwa nitakaowakwaza.

Mimi ni kijana wa miaka 27. Baada ya majaribio ya muda mrefu ya kutafuta mke kushindikana, nilikata tamaa ya kuoa kabisa na nikaamua kubaki single.

Baada ya muda, dada yangu alinipatia binti mwenye miaka 17 na kunitambulisha naye. Kwa upande wangu sikuwa na jibu la moja kwa moja, ingawa familia yangu ilikuwa inaweka msukumo mkubwa ili nimuoe. Mimi bado sikuwa tayari.

Baada ya kuonana, alikuwa binti mzuri sana kwa muonekano, mashaallah, mtoto wa Kiislamu.

Baadaye dada yangu alinieleza nimpatie zawadi. Nikanunua mavazi ya Kiislamu kwa ajili yake pamoja na fedha, nikatoa zaidi ya laki mbili na nusu na pia nikawapatia nauli ya kurudi kwao.

Baada ya hapo niliendelea kuwaza kuchukua hatua gani, lakini moyo bado haukuwa tayari kwa sababu muonekano siyo kipaumbele changu, na pia nilikuwa sijajiridhisha kuhusu tabia yake na mambo mengine.

Binti aliporudi kwao, wazazi wake walimuuliza kuhusu mimi. Akawajibu kuwa ameridhika na mimi na yuko tayari kuolewa.

Changamoto ikaibuka upande wangu nilipoulizwa na dada yangu. Nilimwambia anipe muda zaidi nijifikirie kwa sababu hii ni hatma ya maisha yangu, na sikujihisi tayari.

Nilikaa zaidi ya wiki mbili, ndipo nikatoa majibu kuwa nakubali, lakini siwezi kuoa kwa wakati huo mwaka jana kwa sababu sikuwa vizuri kiuchumi na akili yangu haikuwa na utulivu wa kutosha. Wakakubali.

Baada ya hapo wazazi wa binti wakawa wanamuuliza dada yangu kuhusu hatua ya ndoa. Dada yangu aliwajibu kuwa nimekubali, lakini tunaomba ndoa iwe mwaka unaofuata.

Wazazi wa binti wakasema sawa, lakini kama ni hivyo nipelekewe barua ya posa ili binti atambulike rasmi kama mchumba.

Nilipata taarifa hiyo nikachukua muda kufanya maamuzi kwa sababu bado sikuwa na imani ya moja kwa moja na binti huyo.

Baada ya miezi miwili kupita, nikaandaa barua ya posa kupitia mshenga na nikatoa kiasi cha pesa akaipeleka kwa wazazi wa binti na wakapokea.

Baada ya hapo nikawa mchumba rasmi.

Sasa mwaka umeisha na sasa ni mwezi wa sita, wazazi wa binti wanaona bado nipo kimya, ingawa naendelea kumhudumia kwa fedha na mavazi japo si kwa kiwango kikubwa sana.

Kwa sasa wanataka nipeleke mahali ili hatua zifuate, lakini moyoni bado nahisi hofu. Natamani nimwambie mshenga tuachane kabisa, lakini bado nina wasiwasi. Ingawa yule binti anaonekana kunijali na kunitafuta, mimi bado sijajipa utulivu.

Najiuliza maswali mengi na majibu yake siyapati.

Naombeni ushauri, kaka zangu, dada, wajomba, bibi na babu zangu.

Asante sana.
Screenshot_20260607_152312_Chrome.jpg
Screenshot_20260607_152312_Chrome.jpg
 
Fuata kile moyo wako unakwambia, usiingie naye kwenye ndoa kwa shinikizo au kutaka kuwafurahisha watu fulani, inavyoonekana moyo wako na nafsi yako haviko tayari kumuoa huyo binti, kumbuka Ndoa inaweza kuwa pepo yako duniani au jehanamu yako, kupanga ni kuchagua
 
Achana na stori au banga za pisikali za mjini...
Jitwalie zako mwali maisha yaende, huyo bado hajavurugukiwa...

Nyakati kama hizi hazijirudii.. hii bahati inakujaga mara 2 tu kwenye maisha
 
Changamot yako ni mzur ki muonekano hla we auko vzr kiuchum waswas unawez wasogezea weny uchumi
 
yani kijana m bichi wa miaka 27 ulitafuta mke ukachoka?,,,, enweiiii kama moyo wako haupo tayali usiuforce kisije kikakulamba huko ndani
Kama dogo mkazi wa mjini mtaani aliotakiwa kuwaoa wamechakazwa wakachakaa so kusema amekosa wa kuoa hajakosea na huyo aliyetafutiwa anaonekana ametolewa bush ndani ndani huko.
 
Najiuliza maswali mengi na majibu yake siyapati.

Naombeni ushauri, kaka zangu, dada, wajomba, bibi na babu zangu.
Kabla ya ushauri tukuulize kwanza wewe ulikua unataka nini yaan ulikua unamtaka mwanamke yupi huyo hajakuvutia haya elezea mwanamke yupi unaemtaka wewe maana domo zito sister kakupigia assist still bado hautaki kufunga au unataka kuolewa wewe? Kua mkweli na muwazi kijana wewe unataka mwanamke wa namna gani ungeelezea sio mzuri tabia mzuri umbo wewe unataka wa aina gani? Haujui watu wawili wakiishi kwa muda mrefu kila kitu kinajiset hata km walikua hawapendani kwa dhati ila mambo yanaacha alama ambayo huwezi kuyasahau kamwe umewahi kujiuliza hilo kwamba yeye anaweza kukufanya wewe ushindwe kumsahau kwa jambo gani au ndio ile awepo asiwepo yeye hajakuvutia na chochote sasa ndio useme ana mapungufu gani ambayo mwanamke unaemtaka wewe hatokua na hayo mapungufu?

Nitakupa mfano nimewahi kuletewa mwanamke km wewe ila sikuwahi kuambiwa kwamba huyu mwanamke tumekuletea ni mwanamke wa kwako kwa hio walichotaka wao ni sisi wawili tupendane wenyewe binti alikua anajua mchezo mzima ila mimi nilikua sijui kitu chochote baadhi ya watu wa karibu pia walikua wanaelewa kila kitu ila mimi sikua najua kitu chochote kwa hio ukaribu wangu na yeye mimi nikauweka kwenye category ya urafiki wakati binti yeye ameniweka kwenye category ya mume mtarajiwa kuna kipindi tulikwadhana sana ndipo wale waliotengeneza hiko kitu wakagundua kua mimi sina mpango na yule binti tukatenganishwa na binti akahamishwa haraka sana

Sasa baada ya muda zile memories za kua pamoja hua zinarudi hapo ndio shida inapoanza unagundua kwamba yule ndie aliekua ananipenda kweli huko nilipokuja sio kwenyewe ila mitamaa yangu tu ya mwili na kutokutuliza akili ndio shida inaanzia hapo ila kwa wanaokutafutia kitu hakuna anaekutafutia wewe kitu kibaya sawa unaweza ukasema sikubariani na alienitafutia maana nataka nijitafutie mwenyewe kuna kitu moja ambacho haukielewi unaweza useme hiki sio sahihi kumbe ndicho sahihi kuna wakati utafika utakaa chini na kujiambia maneno ya ndani laiti km ningejua nafasi ile nisinge ichezea laiti km ningejua nisingeacha muda ule unipite majuto huja mwishoni ndio maana walituambia majuto ni mjukuu sio mtoto utajuta ukishazeeka sio ukiwa kijana maana yake ni kwamba kwa miaka 27 tunakuongezea miaka 10 ukiwa na miaka 37 utaanza kumkumbuka huyo mwanamke ulietafutiwa huku ukiwa huna mwanamke wa kueleweka sababu unabonyeza bonyeza sana nyanya huku unataka kununua bilinganya

Sina kingine cha kuongeza ila tuambie huyo binti ulietafutiwa na humtaki ana kasoro gani ya kukuzuia wewe usimuoe hana matako?
 
Back
Top Bottom