Ushauri wa chaiTukupe ushauri gani tena?
Asante mkuu Kwa mawazo yakoMkuu mi navyoona we bado haupo tayari na hata hiyo barua ulipeleka kwa shinikizo tu na ndo ulipoharibu. Ulitakiwa toka mwanzo uwaambie haupo tayari huyo Binti aendelee na mishe zake.
Kwa sababu kuvunja uchumba ni heri kuliko kuvundoa,bora umwache huyo binti awe huru. Wewe bado haupo tayari na kutokuwa tayari si dhambi. Mimi binafsi nishajifunza,kama moyo wangu unasita kufanya jambo hata kama linaonekana zuri kiasi gani,silifanyi. Na wewe kwa sababu moyo wako unasita sikushauri uliendee hilo jambo la ndoa.
Pia,mbona huyo binti bado mdogo sana mkuu, miaka 17? huo umri kumleta binti mjini akutane na wenye mji wao utalizwa mkuu,binti angalau awe na miaka 20. Miaka 17 hata akishika ujauzito manesi wataenda kumtukana na kukutukana wewe,huo umri bado jamani.
Mwisho,muoaji ni wewe,usifanye jambo la ndoa kwa shinikizo lolote. Najua familia zetu lazima waongee lakini ukijenga ndoa kwenye msingi wa kufurahisha familia,utaishia mateso maana itakuwa haujaoa kwa ajili yako bali kwa ajili yao,maisha yenyewe mafupi haya.
Kwasas tupo iyo stage ya kupimaKwa story yako mbona kama wazazi wa binti ndio wanapush ajenda aisee.
Wanataka kutua mzigo gani?
Vipi mmepima afya?
Umefatilia historia yake na familia yake?
Vipi mahusiano ya familia yako na yake yakoje?
Weka ndani umpime, taraka zipo kiongozi, usijipe stress bure.
Kwa story yako mbona kama wazazi wa binti ndio wanapush ajenda aisee.
Wanataka kutua mzigo gani?
Vipi mmepima afya?
Umefatilia historia yake na familia yake?
Vipi mahusiano ya familia yako na yake yakoje?
Weka ndani umpime, taraka zipo kiongozi, usijipe stress
Familiar zana undugu ingawa ni wa mbali ila upo mkuu
Wewe hujampenda binti au hujamjua?
Kama una uwezo wa kuoa we oa tu, maana hapo kiukweli hoja huna ni hisia zako tu na huna ushahidi wowote wa kumtia binti wa watu hatiani.K
Kwasas tupo iyo stage ya kupima
Habarini wakubwa,
Poleni na majukumu. Nianze kwa kuomba radhi kwa nitakaowakwaza.
Mimi ni kijana wa miaka 27. Baada ya majaribio ya muda mrefu ya kutafuta mke kushindikana, nilikata tamaa ya kuoa kabisa na nikaamua kubaki single.
Baada ya muda, dada yangu alinipatia binti mwenye miaka 17 na kunitambulisha naye. Kwa upande wangu sikuwa na jibu la moja kwa moja, ingawa familia yangu ilikuwa inaweka msukumo mkubwa ili nimuoe. Mimi bado sikuwa tayari.
Baada ya kuonana, alikuwa binti mzuri sana kwa muonekano, mashaallah, mtoto wa Kiislamu.
Baadaye dada yangu alinieleza nimpatie zawadi. Nikanunua mavazi ya Kiislamu kwa ajili yake pamoja na fedha, nikatoa zaidi ya laki mbili na nusu na pia nikawapatia nauli ya kurudi kwao.
Baada ya hapo niliendelea kuwaza kuchukua hatua gani, lakini moyo bado haukuwa tayari kwa sababu muonekano siyo kipaumbele changu, na pia nilikuwa sijajiridhisha kuhusu tabia yake na mambo mengine.
Binti aliporudi kwao, wazazi wake walimuuliza kuhusu mimi. Akawajibu kuwa ameridhika na mimi na yuko tayari kuolewa.
Changamoto ikaibuka upande wangu nilipoulizwa na dada yangu. Nilimwambia anipe muda zaidi nijifikirie kwa sababu hii ni hatma ya maisha yangu, na sikujihisi tayari.
Nilikaa zaidi ya wiki mbili, ndipo nikatoa majibu kuwa nakubali, lakini siwezi kuoa kwa wakati huo mwaka jana kwa sababu sikuwa vizuri kiuchumi na akili yangu haikuwa na utulivu wa kutosha. Wakakubali.
Baada ya hapo wazazi wa binti wakawa wanamuuliza dada yangu kuhusu hatua ya ndoa. Dada yangu aliwajibu kuwa nimekubali, lakini tunaomba ndoa iwe mwaka unaofuata.
Wazazi wa binti wakasema sawa, lakini kama ni hivyo nipelekewe barua ya posa ili binti atambulike rasmi kama mchumba.
Nilipata taarifa hiyo nikachukua muda kufanya maamuzi kwa sababu bado sikuwa na imani ya moja kwa moja na binti huyo.
Baada ya miezi miwili kupita, nikaandaa barua ya posa kupitia mshenga na nikatoa kiasi cha pesa akaipeleka kwa wazazi wa binti na wakapokea.
Baada ya hapo nikawa mchumba rasmi.
Sasa mwaka umeisha na sasa ni mwezi wa sita, wazazi wa binti wanaona bado nipo kimya, ingawa naendelea kumhudumia kwa fedha na mavazi japo si kwa kiwango kikubwa sana.
Kwa sasa wanataka nipeleke mahali ili hatua zifuate, lakini moyoni bado nahisi hofu. Natamani nimwambie mshenga tuachane kabisa, lakini bado nina wasiwasi. Ingawa yule binti anaonekana kunijali na kunitafuta, mimi bado sijajipa utulivu.
Najiuliza maswali mengi na majibu yake siyapati.
Naombeni ushauri, kaka zangu, dada, wajomba, bibi na babu zangu.
Asante sana.
Kama dogo mkazi wa mjini mtaani aliotakiwa kuwaoa wamechakazwa wakachakaa so kusema amekosa wa kuoa hajakosea na huyo aliyetafutiwa anaonekana ametolewa bush ndani ndani huko.yani kijana m bichi wa miaka 27 ulitafuta mke ukachoka?,,,, enweiiii kama moyo wako haupo tayali usiuforce kisije kikakulamba huko ndani
Kabla ya ushauri tukuulize kwanza wewe ulikua unataka nini yaan ulikua unamtaka mwanamke yupi huyo hajakuvutia haya elezea mwanamke yupi unaemtaka wewe maana domo zito sister kakupigia assist still bado hautaki kufunga au unataka kuolewa wewe? Kua mkweli na muwazi kijana wewe unataka mwanamke wa namna gani ungeelezea sio mzuri tabia mzuri umbo wewe unataka wa aina gani? Haujui watu wawili wakiishi kwa muda mrefu kila kitu kinajiset hata km walikua hawapendani kwa dhati ila mambo yanaacha alama ambayo huwezi kuyasahau kamwe umewahi kujiuliza hilo kwamba yeye anaweza kukufanya wewe ushindwe kumsahau kwa jambo gani au ndio ile awepo asiwepo yeye hajakuvutia na chochote sasa ndio useme ana mapungufu gani ambayo mwanamke unaemtaka wewe hatokua na hayo mapungufu?Najiuliza maswali mengi na majibu yake siyapati.
Naombeni ushauri, kaka zangu, dada, wajomba, bibi na babu zangu.
kijana jipe mda kidogo wa kumfaham vzr unayetaka kumuoa mwsho wa siku usije kuolewaHuruma siyo malezi kabisa nivunje amri kumi ety kak
Utajua mwenyewe banaJamani demi mi ndugu Yako ujue