Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,151
- 44,120
Umejibu vizuri sana.Una uhakika kwa haya uliyoandika?matatizo makubwa tuliokuwa nayo Waafrika chini ya Jangwa la Sahara ni mfumo wetu wa kufikiri.
Wazungu wanatuita sub human being, binaadamu tuliokuwa hatajaubwa tukakamilika
Waafrika weusi tunatanguliza HISIA zetu katika kuwaza,kuamua,kulea Watoto wetu Katika kujenga hoja,nk
Naona hayo ndio yaliokukuta Wewe, HISIA za kupenda chama zimekufanya uwe mjinga
Nani alazimisha baina ya Wapinzani na Chama tawala!?
Nani amevurugika kama sio Chama Tawala, ..hao waliokimbilia Upinzani si wamerudi CCM,yuko Lowasa na wenzake?
Uchaguzi jinzi ulivyoendeshwa ni ushahidi tosha kuwa Chama tawala kimevurugika,kimechanganyikiwa
Mfumo mbovu gani umeshavunjwa,?..CCM imetawala Tanzania tangu tupate uhuru lakini bado hawajui ni mfumo gani waiendeshe Tanzania
CCM haijui Kama wao ni ma socialist,ma kommunist,wa Capitalist, wamechanganyika na hapa ndipo walipo feli
Kikwete alikuja na mfumo mzuri, sekta binafisi zilikuwa zimeshaanza kutia Sura,..
Huyu jamaa Magu kaondoa ule mfumo amekuja na wake ambao hata Nyerere ulimshinda..
Pale unapopeleka tenda zote kwa vyombo vya serikali maana yake huo ni usochalist,maana yake ni KUUWA sekta binafisi
mfumo ambao Dunia nzima umeukataa Hata hao waliouazisha
CCM imekaa Madarakani muda mwingi kiasi ambacho wamejisahau
wanaanza KUTEKA, KUTESA, KUPOTEZA wale wote ambao wanaokuja na MAWAZO na FIKRA mpya
Ili Tanzania ifanikiwe kimaendeleo ya KIUCHUMI, KIMAADILI inahitaji MAWAZO na MFUMO mpya wa kutuongoza
CCM must quit, CCM must go,56 years is enough..
Free Mazrui and all Political prisoners
Mama D,umeshaona wapi mtu anafungua kiduka, kibiashara chakeHaha mugah di mathew umeandika nini😀😀
Fuata taratibu hakuna atakaekugusa
Kama unabiashara inaweza kuwa ngumu sababu ulizoea kutokufuata taratibu... ila usikate tamaa, cha kufanya tafuta wataalamu wakushauri ufanye nini wakati unarudi kwenye mstari ili uweze kusurvive
Mama D,umeshaona wapi mtu anafungua kiduka, kibiashara chake
Lakini kabla hata hiyo biashara haijafanya kazi tayari amesha pangiwa Kodi gani alipe..,
Mfumo wa kukusanya Kodi,TRA,ni mbovu, sio Mfumo rafiki kwa mfanya biashara mwenye biashara ndogo..
Sasa unamwambia huyu jamaa afate taratibu
Taratibu gani zifuatwe wakati serikali inakusanya kodi kwa mfanya biashara,bila hata kujua biashara inamuingizia faida Gani?!
CCM imechoka,..iondoke Tu
Free Mazrui and all Political Prisoners
Kaduka kadogo kodi inakuaje?
Sijakuelewa
Wanaongelea sekta binafsi gani hiyo....Pale alipowateka akina MO, kumtesa na kumkejeli MANJI, na Wengine wengi.
Pale aliposema hadharani kuwa MATAJIRI wataishi kama MASHETANI.
Mleta mada yeye na Raisi wake wameshasahau hayo?
Nchi za Kiafrika chini ya Jangwa la Sahara, hatuwezi kujitawala.
Wazungu wanasema hivyo kila Siku,wanatuita sub human being.
Mmmh nilijua kuwa kichwa chako kizito kidogo,Wanachama wengi wa CCM wako hivyo
Nimekusudia kusema kuwa serikali inakosea pale inapokadiria Kodi Kwa mfanya biashara kabla duka au biashara halijanza kufanya KAZI..
Yaani ukienda tu ofisi za Tra na kuwambia kuwa unataka kufungua biashara fulani basi wao hapo hapo wanakwambia kwa biashara hiyo inabidi ulipe Kodi kiasi Fulani..
Mfumo huu nimeuona TZ Tu,ninavyojua mimi kodi inalipwa kutokana na mwenendo wa biashara husika
Hili la kukadiriwa kodi linajirudia sana TRA lazima walitolee ufafanuzi.Mama D,umeshaona wapi mtu anafungua kiduka, kibiashara chake
Lakini kabla hata hiyo biashara haijafanya kazi tayari amesha pangiwa Kodi gani alipe..,
Mfumo wa kukusanya Kodi,TRA,ni mbovu, sio Mfumo rafiki kwa mfanya biashara mwenye biashara ndogo..
Sasa unamwambia huyu jamaa afate taratibu
Taratibu gani zifuatwe wakati serikali inakusanya kodi kwa mfanya biashara,bila hata kujua biashara inamuingizia faida Gani?!
CCM imechoka,..iondoke Tu
Free Mazrui and all Political Prisoners
Haya acha nianze kukufahamisha Kwa njia nyengine..Kichwa chako wewe ndio kizito sana. Maelezo unayotoa nashindwa kuamini kama umeshawahi hata kuijua wachana na kufanya biashara kwakweli....
Ukiachana na biashara ndogondogo zetu wamachinga, TRA wako wazi kabisa kukuelekeza nini cha kufanya kama utatoa taarifa.
Fanya makadirio ya kodi wakilisha TRA, kama hujaanza biashara toa taarifa TRA na kama biashara ilikuepo lakini imesimama kwa sababu yoyote ile toa taarifa pia
Kama huelewi fika TRA watakuelekeza taratibu za kufuata, ila ukinyamaza itakugharimu
Kumbe hata hujui, ni zaidi ya trilioni 7 pamoja na The Cost Overruns ambazo haziepukiki katika miradi mikubwa kama hiyo.
Tatizo kubwa la Magufuli ni usanii, yeye ni mtu mwenye roho ya korosho hapendi kabisa kuona watu wanakuwa matajiri, amerudisha utaratibu mbovu wa zamani wa serikali kufanya biashara.
Ameanzisha Tasac ili kuua makampuni ya forodha pia anataka serikali ifanye biashara ya mafuta.
Tayari serikali hii imashaua makampuni mengi ya ukandarasi baada ya serikali kuamua kujenga kwa kutumia Suma JKT na TBA...!!!
Serikali pia inaua sekta ya usafiri wa anga baada ya kuamua kufufua shirika la ndege la Atcl japo linatengeneza hasara kiasi kwamba mahesabu yake hayaruhusiwi kukaguliwa na mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali CAG kwa amri ya rais kwa kile kinachoonekana kama kuficha siri ya hasara.
Wewe ata biashara utakuwa huna ndani ya Tanzania.Haya acha nianze kukufahamisha Kwa njia nyengine..
Mfumo wa kukusanya kodi ninachoona mimi ni mfumo kamdamizi,
Mfano, Wewe mama D Una biashara yako ya Vijora na Mimi nafanya biashara hiyo
Wewe unapata faida Laki tano Kwa siku, Mimi napata elfu hamsini kwa siku..
Ulipoenda TRA kuwambia kuwa unataka kufungua biashara ya Vijora walikukadiria kuwa ulipe Laki mbili kwa mwaka,na hivyo hivyo..
Kwa maana Hiyo,ndio maana nathubutu nasema kuwafumo wa kukusanya kodi si rafiki kwa mfanya biashara mwenye faida ndogo
TRA haikusanyi Kodi kulingana na faida anayopata mfanyabiashara,
TRA inakusanya Kodi kulingana na biashara gani anafanya mfanya biashara..
Nafikiri Sasa umefahamu,...
Najua watu wa kupiga makofi na kusifu hata kama Kuna kasoro kwenye system nyinyi mnasifu tu
CCM must go...
Free Mazrui and all Political Prisoners
Nakuona John, na a/c yako ya kike.Ukisoma ilani ya CCM halafu ukasikiliza Ile speech ya kufungua Bunge utaweza kujipanga kujua wapi uongeze nguvu.
Kwa upande wa mikopo midogomidogo SME Serikali imejipanga, wananchi tujipange, banks na taasisi za fedha wajipange pia
Maendeleo hayana vyama
Mkuu tindo lini utaondoks kwenye kifungo cha kifikra usiwe tegemezi?Anachosema sio anachomaanisha. Haamini katika sekta binafsi, bali anaamini katika sekta ya umma, simply huko anaweza kwenda kwa kustukiza na kuwatambua ili kusaka kiki za kisiasa.
Kwa taarifa yako hakuna muwekazaji serious atawekeza chini ya utawala wake, maana sio mtu anayejali sheria. Ukiona taifa ambalo hata mchina anakwepa kuwekeza jiulize sana.
Hapa sekta binafsi itaanza kurejea tena ilipokuwa, baada ya yeye kutoka madarakani. Rejea kilichotokea kwa wafanyabishara wa Bureau de change.