Ninamzidishia baba 500K kila nikitoa hela

hata haukosei mwaya maana ile ya mama ni yake na ile ya baba itatumika nyumbani so ile unayomuongezea inakua yake tu


ila hela zote hizo unatoa wapi mwenzetu ni freemason au 😂
Azidishe kwa mama maana majukumu yote ni mama kuanzia chakula hadi mavazi ya wajukuu. Wababa pesa yote inaishia kwenye ulabu na akienda nyumbani anataka chakula wakati hajachangia hata mia. Yy ni ulabu tu. Nimekaa uchagani najua historia ya wazee wetu was kichaga
 
Hongera Sanaa mkuu, Asilimia kubwa ya sisi vija baada yakuoa tu tunawasahau wazazi, Hii sio kwakupenda, ni uzito wa majukumu ya kifamilia n.k
Lakini ukiwakumbuka wazazi Baraka zinamiminika tele kwenye Kila kona ya michongo ya pesa. Binafsi ninacho wapa nikidogo sanaa pindi wakiniomba pesa ,Natamani siku ifike Nije kuwapa kiwango kama chako inshallah Mwenyezi Mungu anifikishe hapo Amen.
 
ni nyie wachqga huku kwingine mababa wako responsible
 
Nadhani mwenye Uzi haelewi maana K(thousands)
Kwamba ni 5k au 50k? Mtu wa kutoa 500k asingekuja kutoa Uzi wa kuomba ushauri.

Raha ya JF ni uwezo wa kuwa kitu chochote wakati wowote kadri unavyojisikia.
 
Bilashaka we utakuwa muhaya

Kwahiyo hata sisi tunaowasaidia wazaz wetu kimya kimya ruje hapa kusema vibunda tunavyowapa wazazi wetu?
 
 
Kapime dna kama kweli dady wako
Advs
Ukete majibu tuanze kukushauri
 
We mwanaume kabisa .Hongera sana ,Mzee atatunza na nyingine atatumia na familia nzima,Ile ya Mama inaishia KUTOA kwa wachungaji feki na mambo ya ajabu ajabu
 
Toa ndugu ulichonacho wewe bwana atakuona mpaka moyoni mwako
 
Kwani kulikuwa na haja ya kutaja kiasi?? Maana yaweza kuwa kubwa kwa baadhi ya jf members na inaweza kuwa ni ndogo sana na kituko kwa baadhi ya jf members pia.
 
Mama zetu wa kiafrika tunawajua Sisi tuache wenyewe, Mimi nikiwa na mchongo nikimtonya Mzee ananipa ABC fanya hivi fanya vile nikimpelekea Bi Mdashi Bi Maza Bi Mkubwa anasema emu nenda ukajadiliane na Baba yako, ushaelewa mpaka hapo? Yaan uende Chemba ukakae na Mzee mujadiliane Ila yeye kukupa ABC ni big NO Mzee si yupo? Haya nenda ukaongee nae mtamalizana huko, kwa ukijua kwa upande huo pia unaona Bora umalizane na Mzee huko huko Chemba na mambo mengine yaendelee kwamba Mzee emu kamatia na hii itakusevu kibingwa, hivyo ndio Wanaume hufanya kuwaokoa Wanaume wenzao ipo siku huko umepalaganyana na Mamsapu ukirudi home kusuluhisha Bi Mkubwa point yake ya Msingi ni hio emu nenda ukaongee vizuri na Baba yako akwambie nini cha kufanya, kwa hio unagundua Baba ana-play big role kwenye family, hopefully utakua umenielewa kwa kiasi chake
 
Unampa Mama kwa kupitia mlango wa Baba maana cha Baba kinaenda kwa Mama, sijui unanielewa vizuri hapo?

Baba yako anamhudumia Mama yako Wewe mpe Mama yako mara 3 Baba yako mpe mara 1 Ile mara 1 uliyompa Baba yako yote inaenda kwa Mama yako kwa hio inakua umempa Mama yako mara 4, sijui unanielewa?
 
Maisha kweli tunatofautiana mkongwe 1.5M kila mwezi, hapo we hujala na familia yako unazungumzia milioni nyingine, usafiri wa kazini, nauli za watoto shule, ma mtu huduma zake nyingine na vitu vidogovidogo, hizo ni huduma za costant, bado ada za shule, ukweni hakujatokea dharura, misiba kwa jamaa, marafiki... Ichango ya harusi, service ya usafiri.

Nishakula dona na dagaa langu kurusungu hapa, naperuzi JF nawatizama madigala, madon..

Mishani hatuwezi kuwa sawa.
 
Naona n

Sio kila baba
 
Kuna wazazi wengine huwa wanaweka hela unazowatumia au kuwapa
Na usidhani wazazi wote wanazila hizo hela
Wengine wanasubiri siku ukiyumba utashangaa na yeye anakuita kwa siri na kukuambia hizi za vocha weka mfukoni

What goes around.......
Kweli mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…