UMUGHAKA
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 3,149
- 14,407
Nsikuchoshe na Usinchoshe,Tusichoshane!
Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mtakaopitia huu Ujumbe,Tafadhali sana naomba mumfikishie Mh.Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kwamba ninaomba kwa ridhaa yangu mwenyewe niwe mmoja ya Walinzi wake Binafsi!
Sababu ya mimi kuomba kuwa mlinzi Binafsi ni kwasababu nahitaji kutumia nguvu,Akili na uwezo wangu alionipatia Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mtu ambaye nimekuwa nikimkubali kwa muda mrefu!
Hiyo moja,Lakini Pili,Nahitaji kumlinda Mh.John Heche kwakuwa amekuwa mstari wa mbele kuwasemea ukweli watanzania wengi ambao hawana uwezo wa kusema ukweli hadharani,Sote (wenye akili timamu) tunatambua kwasasa nchi hii nzuri yenye kupendeza ukiusema ukweli mbele ya watawala dhalimu basi unakuwa umeuweka uhai wako rehani!,Hivyo nitakuwa ninafuraha kama nitakuwa mmoja wa walinzi binafsi wa Mh.John Heche ili kutimiza hilo lengo tajwa hapo Juu!
Tatu,Mimi ni Mkurya mwenye akili timamu,shababi,Mwenye uwezo wa Kutosha (Physically & Mentally) hivyo nimeona ni muda sahihi kumuunga mkono Mkurya mwenzangu kuweza kulisongesha gurudumu mbele la kusema ukweli ili watanzania wazuri aliowaumba Mungu wafurahie nchi yao nzuri iliyobarikiwa kwa kuwa na rasilimali za kutosha!
Mengine nadhani nitaongea na Makamu mwenyekiti mwenyewe nitakapokutana naye,Siwezi kuyaweka hapa!
Hivyo popote mpatapo ujumbe huu watu wa Karibu na Heche,Tafadhalini mwambieni Kijana kutoka Mogabiri Tarime nina wiwa kuwa Mlinzi wake Binafsi!
Ni hayo tu!